Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,986
- 156,264
Shy-Rose Bhanji
Imekuwa ni desturi kwa baadhi ya WanaCCM kwamba kila ninapotoa maoni yangu ya kukikosoa chama changu au serikali wamekuwa wananishambulia kuwa ni sababu ya kukosa ubunge wa Afrika Mashariki. Sina chuki ya kukosa ubunge na hii naisema kutoka moyoni. Siku zote nimekuwa mkweli kwamba pale panapotakiwa kukosoa sijasita kufanya hivo na pale panapotakiwa kupongeza sijasita kufanya hivo.
Kwa vile ninanyanyaswa sana ni vizuri nilitolee ufafanuzi: Huo ubunge siyo kwamba nilikosa lakini ni kutokana na majungu, fitna na roho mbaya ya baadhi ya watu....vita niliyopigwa ni kubwa sana na Mungu tu ndo anajua. Ni kweli kwamba niliumia sana sana kwasababu sikujua nimemkosea nini Rais Magufuli mtu ambaye nilimpenda kwa moyo wangu wote. Isitoshe kazi yangu ya ubunge niliifanya kwa kujituma na kwa moyo wangu wote. Ulikuwa huniambii kitu pale lilipotajwa jina lake...nilifunga safari mpaka mikoani kumfanyia kampeni kwa pesa zangu mfukoni siyo kwamba anipe cheo, hapana ni kwasababu nilimwamini.
Na Naomba niwaulize hivi JK angemkata jina Magufuli baada ya kushinda kura za maoni ndani ya chama angejiskiaje? Hakika angeumia lakini nina imani angemsamehe kama vile mimi nilivomsamehe. Hizi ni nafasi leo zipo na kesho hazipo. Ni sawa na kuja duniani na kesho tunaondoka. Naomba sana sana msininyanyase kwasababu mnaniumiza moyo wangu