issenye
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 3,781
- 5,205
Naomba wanajf tujadili tuhuma hizi.
CCM chakishutumu Chadema migomo vyuo vikuu
Na Mwandishi wetu
13th February 2011
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimekituhumu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),kuwa kimekuwa kikichangia migomo ya wanafunzi wa Elimu ya juu, na kuchochea vurugu zinazoendelea vyuoni.
Tuhuma hizo zilitolewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kilumbe Ng'enda alipokuwa akizungumza na Madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa, wa wilaya ya Kinondoni wa chama hicho juzi jijini.
Ng'enda alisema Chadema wamekuwa wanaleta migogoro na misukumo katika vyuo vikuu ili chama tawala CCM kiondolewe madarakani kwa migogoro hiyo.
"Vurugu hizi zina ushawishi mkubwa wa siasa hasa Chadema na hasa tukio la Arusha, walianzisha vurugu na wenyewe kukaa pembeni, hadi leo hakuna kinachoendelea baada ya wale watu kufa na kuzikwa, kikubwa waliambiwa wapumzike kwa amani," alisema.
Alisema CCM hakiwezi kung'olewa madarakani, na chama chochote bali kitajing'oa chenyewe, kwa kutokuwa na ushirikiano ndani ya chama.
Alisema kuwa chama kitahakikisha kinawapa vipaumbele wananchi kwa kuwatatulia shida zao zilizoko katika jamii, ili kukipa chama fursa ya kurudisha heshima yake katika kuogoza nchi.
Pia alimpongeza mgeni rasmi wa kikao hicho, Didas Masaburi Meya ya jiji la Dar es salam, kwa nia yake ya kujua ufanisi wa huduma za jamii katika manispaa zote tatu, katika ziara aliyokuwa anamalizia katika kikao hicho.
Dk. Masaburi katika ziara yake aliahidi mipira kwa kila kata, lengo likiwa ni kuweka vijana katika umoja wa chama, na kuwaingiza katika mpango wa ajira, katika kila kata wanazoishi, kama ulinzi shirikishi na usafi wa mazingira.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI