Shutuma za CCM dhidi ya CDM ni za Kweli?

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,781
5,205
Naomba wanajf tujadili tuhuma hizi.

CCM chakishutumu Chadema migomo vyuo vikuu

Na Mwandishi wetu
13th February 2011

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimekituhumu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),kuwa kimekuwa kikichangia migomo ya wanafunzi wa Elimu ya juu, na kuchochea vurugu zinazoendelea vyuoni.

Tuhuma hizo zilitolewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kilumbe Ng'enda alipokuwa akizungumza na Madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa, wa wilaya ya Kinondoni wa chama hicho juzi jijini.

Ng'enda alisema Chadema wamekuwa wanaleta migogoro na misukumo katika vyuo vikuu ili chama tawala CCM kiondolewe madarakani kwa migogoro hiyo.

"Vurugu hizi zina ushawishi mkubwa wa siasa hasa Chadema na hasa tukio la Arusha, walianzisha vurugu na wenyewe kukaa pembeni, hadi leo hakuna kinachoendelea baada ya wale watu kufa na kuzikwa, kikubwa waliambiwa wapumzike kwa amani," alisema.

Alisema CCM hakiwezi kung'olewa madarakani, na chama chochote bali kitajing'oa chenyewe, kwa kutokuwa na ushirikiano ndani ya chama.

Alisema kuwa chama kitahakikisha kinawapa vipaumbele wananchi kwa kuwatatulia shida zao zilizoko katika jamii, ili kukipa chama fursa ya kurudisha heshima yake katika kuogoza nchi.

Pia alimpongeza mgeni rasmi wa kikao hicho, Didas Masaburi Meya ya jiji la Dar es salam, kwa nia yake ya kujua ufanisi wa huduma za jamii katika manispaa zote tatu, katika ziara aliyokuwa anamalizia katika kikao hicho.

Dk. Masaburi katika ziara yake aliahidi mipira kwa kila kata, lengo likiwa ni kuweka vijana katika umoja wa chama, na kuwaingiza katika mpango wa ajira, katika kila kata wanazoishi, kama ulinzi shirikishi na usafi wa mazingira.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Wanatafuta pa kujishikiza.
na pa kutupia Lawama!, Na wafanyakazi wakigoma itakuaje???
 
CCM kila mtu ni intelejensia...... Leo asb mwanangu kagoma kunywa chai na wali kiporo, watakua CDM.
 
Lisemwalo lipo kama halipo laja...............
Misemo mingine ishapitwa na wakati kabisa hivi mfano tukisema Mohammedi Shossi ni shoga hata kama sio shoga atakuja kuwa shoga?

Mohammed Shossi ni Shoga...lisemwalo lipo kama halipo laja..(utajibu hivyo?)
 
Nimepanda daladala na denti kagoma kuachia siti, nadhani chdm wanahusika. Unapokabiliwa na tatizo la kushindwa kuongoza basi tatizo lako watupie wengine ww ubaki unadunda kwa ulinzi wa polisi
 
aaaahhh nimeipenda hiyo
 
Nimepanda daladala na denti kagoma kuachia siti, nadhani chdm wanahusika. Unapokabiliwa na tatizo la kushindwa kuongoza basi tatizo lako watupie wengine ww ubaki unadunda kwa ulinzi wa polisi
mwizi kagoma kurudisha viatu alivyokwapua kwa sababu kashawishiwa na CDM, hata MAKAMBA hana pumba kama hizi,
Mwingine eti lisemwalo lipo/laja : Okey nasema kuna siku atajikuta anajinsia opposite....na asibishe kwa kuwa lisemwalo laja
 
Jamani mbavu zangu.
 
Msemo maana yake nini? Huna jipya! Watu tunapata shida, tunakosa mahali pa kulala, tunakosa maji hata ya kunywa wewe unasema tumeshinikizwa na CDM? Kama huna cha kuchangia ni bora unyamaze. Una roho mbaya sana wewe.
 
Naomba wanajf tujadili tuhuma hizi.

CCM chakishutumu Chadema migomo vyuo vikuu

Na Mwandishi wetu

13th February 2011

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimekituhumu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),kuwa kimekuwa kikichangia migomo ya wanafunzi wa Elimu ya juu, na kuchochea vurugu zinazoendelea vyuoni.
Tuhuma hizo zilitolewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kilumbe Ng'enda alipokuwa akizungumza na Madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa, wa wilaya ya Kinondoni wa chama hicho juzi jijini.
Ng'enda alisema Chadema wamekuwa wanaleta migogoro na misukumo katika vyuo vikuu ili chama tawala CCM kiondolewe madarakani kwa migogoro hiyo.
"Vurugu hizi zina ushawishi mkubwa wa siasa hasa Chadema na hasa tukio la Arusha, walianzisha vurugu na wenyewe kukaa pembeni, hadi leo hakuna kinachoendelea baada ya wale watu kufa na kuzikwa, kikubwa waliambiwa wapumzike kwa amani," alisema.
Alisema CCM hakiwezi kung'olewa madarakani, na chama chochote bali kitajing'oa chenyewe, kwa kutokuwa na ushirikiano ndani ya chama.
Alisema kuwa chama kitahakikisha kinawapa vipaumbele wananchi kwa kuwatatulia shida zao zilizoko katika jamii, ili kukipa chama fursa ya kurudisha heshima yake katika kuogoza nchi.
Pia alimpongeza mgeni rasmi wa kikao hicho, Didas Masaburi Meya ya jiji la Dar es salam, kwa nia yake ya kujua ufanisi wa huduma za jamii katika manispaa zote tatu, katika ziara aliyokuwa anamalizia katika kikao hicho.
Dk. Masaburi katika ziara yake aliahidi mipira kwa kila kata, lengo likiwa ni kuweka vijana katika umoja wa chama, na kuwaingiza katika mpango wa ajira, katika kila kata wanazoishi, kama ulinzi shirikishi na usafi wa mazingira.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

This is another Makamba in a making!Kilumbe Ng'enda.

Kweli CCM hakina watu. Sijui CCM inaokota wapi haya majitu yasiyokuwa na punje ya kufikiri.

  1. Hivi CHADEMA inahusikanaje na MIGOGORO ya vyuo vikuu????UDOM kaenda Mizengo Pinda akakuta uozo kuanzia kwa Maprofesa mpaka wanachuo. Hivi Pinda alipoagiza CAG akachunguze matumizi mabaya ya pesa hapo UDOM ina maana atakuwa anawachunguza CHADEMA??????????
  2. UDSM,DUCE,Mkwawa na kwingine ni MALALAMIKO ya malipo hafifu au yasiyokuwa na utaratibu mzuri. Hivi Tshs.5,000/= wanazolipwa wanachuo kuwa hazitoshi na wanataka zifike mpaka 10,000/= CHADEMA wanahusikaje???
  3. Migomo mingi ya Vyuo vikuu inasababishwa na BODI YA MIKOPO-HELB na siyo CHADEMA.
  4. Halafu jitu linabwabwaja kuwa CCM hakiwezi kuondolewa madarakani na kitaendelea kuongoza na kuwatatulia wananchi matatizo yao. HUYU MTU HAJUI HATA UPEPO WA KISIASA UNAVOVUMA HUKO ARABUNI NA UNAKUJA AFRIKA MASHARIKI. Ng'enda ajue kuwa CCM hawatabaki salama na kuendelea kuongoza milele. CCM wanatatua shida gani hasa ikiwa SWALA LA UMEME IMEKUWA NI MFUPA ULIOMSHINDA FISI. NG'ENDA AJUE KUWA NGUVU YA UMMA IKO MLANGONI!!!KAMA CCM MMEZOA KUIBA KURA,HATUTAENDELEA KUSUBIRI TENA KURA ZA WIZI BAALI TUTATUMIA NGUVU YA UMMA!!!
Kweli CCM ina watu ambao ni lalabongo sana na wanaachiwa kuropokaropoka mitaani na kupotosha umma. Pambaf kabisa!
 
Misemo mingine ishapitwa na wakati kabisa hivi mfano tukisema Mohammedi Shossi ni shoga hata kama sio shoga atakuja kuwa shoga?

Mohammed Shossi ni Shoga...lisemwalo lipo kama halipo laja..(utajibu hivyo?)[/QUOTE]

ngoja nikapate lunch badaye,maana hapo kwenye red pako bomba sana kwa watu kama shossi:clap2::clap2::clap2::clap2::clap2:
 
Kama kweli Chadema wanaweza kuwashawishi wanafunzi wagome na kweli wanafunzi wanagoma, basi huo ni ushindi kwa chama. Chama chochote kile kina wajibu wa kuwa na ushawishi kwa wanachama au mashabiki wake.

Tatizo la CCM kwa upande wao ni kushindwa kwao kuwashawishi wanafunzi WASIGOME!!!.. Huku ni kushindwa kubaya. Wanaamini kabisa kuwa wanafunzi wanachochewa na Chadema, halafu wao wanakaa kimya.

Sasa Chadema waende hatua moja mbele kuwashawishi wananchi wa TZ wagome kutawaliwa na mafisadi. Wataweza. Kama wameweza kwa wanafunzi...it is just a matter of time.
 
>>>>Shost upo? usipotee tunakumiss bro, hebu saidia kujibu hii issue ya lisemwalo lipo. kulinda heshma ya cuf na ccm.
 
Back
Top Bottom