Hii ni sawa ? kwamba kuna dini zinatakiwa kujua kuna wanafunzi wangapi mashuleni bila kueleza nini kinataka kufanyika? maana kama ni suala la waumini sio lazima kwenda shuleni unawapata kwenye nyumba zote za ibada inaweza pata takwimu, lakini hii ina malengo gani kusema kuna takwimu za wanafunzi wa dini hii na inakwenda kufanyika shuleni wanafunzi wote wanaona, shule hapo wanafunzi wanakuwa wamepata ujumbe gani?
View attachment 2986926

Source: Wenye Nchi Wananchi

Serikali wasitishe kabisa hili zoezi. Halina afya kwa utengamano wa taifa. Sensa nzuri ya waumini wa dini yoyote ile ni kule wanako abudu. Na kule utapata namba halisi, maana viongozi wao watakupa orodha ya waumini wao wote. Watakupa pia na status zao. Yupi yiko active na yupi yuko dormant.
 
Tukiwa shuleni, tulikuwa tunahesabiwa wanafunzi wa UKWATA (Protestants), TYCS(Katoliki), Wasababto na Waislam kwa kila darasa bila kuwepo na idhini ya kiserikali.

Sasa sijajua ni kwanini watu washangae sasa hivi wanafunzi kuhesabiwa tena kwa ruhusa na barua ya kiserikali.
acha kutetea udini wewe, hivi shuleni unawezaje kupata idadi kamili ya wanafunzi wa dini au dhehebu fulani? Let's say UKWATA, TYCS, CASFETA/TAYOMI, UHIMA na wengingine wengi wakati wanafunzi hubadilisha dini na dhehebu kwa uhuru wawapo shuleni/chuoni? Udini haukubaliki Tanzania/Tanganyika
 
Kwanini wasifanye sensa ya wanafunzi wa dini zote, au wa dini zingine hawana somo la dini?!!!
Hilo ndo lingeondoa sintofahamu inayojitokeza.
Ni sahihi kuweka Takwimu za shule bayana i.e. Shuleni wapo watoto kadhaa kwa mchanganuo wa Darasa, Jinsia, Umri, Dini n.k. Lakini ukishaanza kuwapitishia sensa ya kutaka wale wa dini fulani tuu; lazima utoe maelezo ya kina ni kwa lengo gani unataka wale wa Imani/dini hiyo tuu? Kwani hawamwamini Mwl.Mkuu wakionana naye watapata idadi wanayoitaka kwa kuangalia kwenye consolidated Register ya wanafunzi hapo shuleni au ni mpaka wafanye sensa hiyo wao wenyewe? Kuna nini? Ingelifaa Serikali isitishe jambo hili mara moja vinginevyo linaweza kuleta shida hapo mbeleni.Tuweni makini sana. Mambo ya Udini-udini hayajawahi kumwacha mtu salama.
 
Taratiiiibu Yale ya miaka ya 95 kipindi cha mkapa, yanarudi, Mara hatutaki mabucha ya nyama maeneo yenye wa Islam wengi!,?Mara tunataka watoto wa ki Islam wavae hijab shuleni(mpaka shule binafsi zililazimishwa), wakataka hata polisi na wana jeshi wa kike wavae hijab! Wazee wa usalama wakapinga
kwa manesi na maofisi mengine wali win. Ni full maushungi kwa kwenda mbele
 
Maybe ni taasisi X tu inafanya research kuangalia waislam waliopo shuleni na ambao hawapo mashuleni.

(Kuna baadhi ya waislamu hawaamini katika elimu Dunia; yaani wao ni madrasa tu)

So, through hiyo research labda itawasaidia hao reseacher kudevelop strategies kudeal na hiyo mindset.
Inafikirisha sana. Mbona Ipo sheria ya JMT inayomtaka mzazi awaepeleke bila shuruti watoto wake shuleni ikiwa ni mojawapo ya Hitajio la Haki za Mtoto?
Tuwe makini jamani isijekuwa wanatafutwa wale walio physically fit and Trainables ili wapewe "sponsorship" na kupelekwa huko... kupata mafunzo maalum halafu baadaye wakishafuzu warejee hapa na waje kuwarudi wale wa dini nyingine a.k.a Makafiri. Kumbuka walisha wahi kufanya hivyo na wakakamatwa na katika timbwili hilo wakakutwa na mavisu na mafunzo yasiyo katika Mitaala ya Tz. Hatujifunzi tuu??
 
Soma hapo namba 2.
Iwe iwavyo, utaratibu wa Serikali unadai kwamba katika masuala nyeti kama hilo, Barua inatakiwa isainiwe na Mkurugenzi Mtendaji (W)in Person na sio Kaimu mkurugenzi. Barua iliyosainiwa na Ag. DED ni batili.
 
Maybe ni taasisi X tu inafanya research kuangalia waislam waliopo shuleni na ambao hawapo mashuleni.

(Kuna baadhi ya waislamu hawaamini katika elimu Dunia; yaani wao ni madrasa tu)

So, through hiyo research labda itawasaidia hao reseacher kudevelop strategies kudeal na hiyo mindse

Maybe ni taasisi X tu inafanya research kuangalia waislam waliopo shuleni na ambao hawapo mashuleni.

(Kuna baadhi ya waislamu hawaamini katika elimu Dunia; yaani wao ni madrasa tu)

So, through hiyo research labda itawasaidia hao reseacher kudevelop strategies kudeal na hiyo mindset.
Why"maybe?"shuleni hawaendi waslamu na wakristo ila wanafunzi,waslamu na wakristo wanapatikana msikitini na kanisani,hizo research zifanyike huko na sio shule.
 
Kipindi hicho nasoma haya mambo yalikuwepo hasa advance school, unakuta karatasi zinapita Kwa lengo la kufahamu idadi ya waumini wa dini Fulani au dhehebu Fulani wako wangapi na hata walimu pia...binafsi naona si vibaya kabisa lakini lazima itolewe sababu ya kufanya hivyo, it's very simple kuwa tunataka idadi ya wanafunzi wa kiislamu kwasababu ya hivi na hivi na kama matumizi yake ni nje ya Shule basi lazima govt itoe vibali nk...sioni shida kama Kuna taratibu nzuri..
 
Hii ni sawa ? kwamba kuna dini zinatakiwa kujua kuna wanafunzi wangapi mashuleni bila kueleza nini kinataka kufanyika? maana kama ni suala la waumini sio lazima kwenda shuleni unawapata kwenye nyumba zote za ibada inaweza pata takwimu, lakini hii ina malengo gani kusema kuna takwimu za wanafunzi wa dini hii na inakwenda kufanyika shuleni wanafunzi wote wanaona, shule hapo wanafunzi wanakuwa wamepata ujumbe gani?
View attachment 2986926

Source: Wenye Nchi Wananchi
Watakuwa binamu za Mama kutoka Oman wanataka kujua idadi ya waislam Tanzania.
 
Back
Top Bottom