Shule za vipaji maalum zina mchango gani hasa katika Elimu ya Tanzania?

Kusoma ni juhudi. Ila kuziponda hizo shule na kusema hazina mchamgo sio sahihi pia. Wengi wa jamaa waliosoma kwenye hizo shule wapo vizuri sana kitaaluma. Tanzania ina watu 4 waliowahi kuwa maraisi, wawili kati ya hao wamesoma hizo shule. (Nyerere - Tabora & Kikwete - Kibaha), Sumaye -Ilboru.
Hao ni wanasiasa tu, sasa nenda vyuoni kwa wahadhiri, serikalini, makampuni binafsi kaangalie key staff hasa kwenye engineering na IT. Kaangalie wanasheria n.k.
Nakubaliana na mtoa hoja kwamba hizi shule siku hizi hazisikiki, miaka ya nyuma zilikuwa zinashindana zenyewe kwa zenyewe

Sisi kweli tuna viwango vya chini sana.

I mean, kwa hiyo mtu kuwa mwanasheria maana ni kwamba ana kipaji maalumu?

Kwa vile Kikwete kasoma sijui Kibaha hivyo naye ana kipaji maalumu? Seriously? Ana kipaji gani huyu kilicho maalumu?

Kuwa mhadhiri wa chuo kikuu ni kuwa na kipaji maalumu?S

SMDH!
 
Pugu inafifia kabisa but ina mchango mkubwa sanna katika taifa, Nyerere anaitwa mwalimu kwa sababu ya Pugu, Pinda kasoma hapo, jerry Slaa, Jaji Samatta, Ahmed Salim, Mkapa, na mawaziri wengi wa awamu ya tatu na ya nne,

nyerere ana elimu gan kwani mpaka umsifie hapa..hio diploma ya ualimu alonayo hata dada yangu anayo
 
nilikuwa nasoma kibaha form 2 nilifeli mtihani..
nikafungashiwa virago vyangu na maneno juu eti sina kiwango cha kusoma special school wakanipeleka tosamaganga.
nakumbuka necta form 4 nikapiga div 1:10...nikarudishwa tena kibaha walimu wote walionikejeli midomo chini.
necta form 6 nikachukua div 1:4...
lakini kiukweli ukisoma special umetoka kimaisha hakuna kufeli ni mwendo wa vipanga tu.
 
Na wewe kipaji?
 
Kwani wewe mleta mada una mchango gani baada ya kusoma shule za vipaji.jitambue kwanza wewe
 
Sisi kweli tuna viwango vya chini sana.

I mean, kwa hiyo mtu kuwa mwanasheria maana ni kwamba ana kipaji maalumu?

Kwa vile Kikwete kasoma sijui Kibaha hivyo naye ana kipaji maalumu? Seriously? Ana kipaji gani huyu kilicho maalumu?

Kuwa mhadhiri wa chuo kikuu ni kuwa na kipaji maalumu?S

SMDH!

Inategemea maana yako ya vipaji maalumu.
 
Albert Einstein, Stephen Hawking.....

Siyo Ridhwani Kikwete ambaye ni mwanasheria, siyo Petro E Mselewa ambaye ni mwanasheria, siyo mhandisi Stela Manyanya.....
Ndio maana nikasema inategemea na maana yako. Kama unadhani vipaji maalumu vipo kwenye sayansi tu basi sawa, ni mtazamo wako.
 
Kwani zilianzishwa lini naona wachangiaji wanataja shule kongwe, nadhani hizi zilianzishwa baada ya mfumo wa kuchangia gharama kuanzishwa mapema 1990's
 
Shule za vipaji maalumu zinatia motisha ya watu kusoma ili wakasomee hizo shule wala sio kuleta matabaka,,ndio maana ili uende izo shule ni lazima uwe na kiwango cha juu cha ufaulu
 
William Shakespeare, Mozart, Wole Soyinka, Charles Dickens, Beethoven.....
Acha illusions, upo TZ mkuu. Sio kwamba wale walioenda kwenye hizo shule hawana vipaji, bali ni mazingira ndio yamechangia wasiwe kama hao uliowataja. Hata vyuo vikubwa vya nchi zilizoendelea mf. Havard, MIT, Yale, n.k moja ya vigezo vya kwenda kule ni kufaulu mitihani kwa marks nyingi (ingawa pia kuna vigezo vingi vya ziada kwa kuwa wengi wanakuwa wamefaulu). Ingekuwa hizi shule na mfumo wetu wa elimu unasapoti ubunifu ndio ungewalinganisha na hao unaondelea kuwataja. Ni mtazamo tu
 
Shule za vipaji maalumu zinatia motisha ya watu kusoma ili wakasomee hizo shule wala sio kuleta matabaka,,ndio maana ili uende izo shule ni lazima uwe na kiwango cha juu cha ufaulu

Kwahiyo kiwango cha juu cha ufaulu ndio ukipaji?
 
Acha illusions, upo TZ mkuu. Sio kwamba wale walioenda kwenye hizo shule hawana vipaji, bali ni mazingira ndio yamechangia wasiwe kama hao uliowataja. Hata vyuo vikubwa vya nchi zilizoendelea mf. Havard, MIT, Yale, n.k moja ya vigezo vya kwenda kule ni kufaulu mitihani kwa marks nyingi (ingawa pia kuna vigezo vingi vya ziada kwa kuwa wengi wanakuwa wamefaulu). Ingekuwa hizi shule na mfumo wetu wa elimu unasapoti ubunifu ndio ungewalinganisha na hao unaondelea kuwataja. Ni mtazamo tu

Kwanza kabisa, mtu kupata alama za juu kwenye mtihani wa taifa siyo kipaji maalumu.

Pili, naona umezungumzia mazingira. Kwa taarifa yako, hayo mazingira hayashushwi toka mbinguni bali huundwa.

Watu walio na vipaji maalumu sioni kwa nini washindwe kuunda mazingira bora ya wao kujifanyia shughuli zao.

Unadhani hizo Harvard na MIT zilishushwa tu toka mbinguni halafu zikatua Marekani?

Usione vyaelea tu...vimeundwa na watu wenye vipaji maalumu na ndo maana hata matokeo yake kwa kiasi kikubwa yanathibitisha hilo.

Hivi vipaji vyetu maalumu vya NECTA ni vichekesho tupu.
 
Binafsi nazani shule hizi zilikuwa na lengo zuri kuandaa watu bora katika nchi na zipo nchi nyingi tu dunia lakinI kutokana na hii corrupt government mitihani inavuja walimu awafundishi shule hizi zinapoteza umaarufu na kuonekana hazina maana kabisa yaani Mimi nakerwa kwa kweli aiwezekani shule ilio kuwa na wanafunzi wengi walioingia advance kwa division two na three Leo hii wawe na distinctions nyingi kuliko shule maalumu ambapo watu wanaingia kwa ufaulu mkubwa
 
Back
Top Bottom