SoC04 Maboresho mfumo wa elimu ili kupelekea Tanzania kuwa na uchumi mkubwa

Tanzania Tuitakayo competition threads

Youngstunna

JF-Expert Member
Jul 5, 2016
265
296
TANZANIA TUITAKAYO,MABORESHO MFUMO WA ELIMU ILI KUPELEKEA TANZANIA KUWA NA UCHUMI MKUBWA

Tokea kupata uhuru wa Tanganyika kumekuwa na maazimio tofauti ya kuboresha mfumo wetu wa elimu tangu mwaka 1967 kwenye azimio la Musoma ambao serikali ilikuja na sera ya education for “self relience’’ ambayo ililisisitiza universal personal education, ambapo elimu ya msingi ni lazima kwa kila mtoto,Tukaja mwaka 1995 ambapo serikali kupitia wizara ya elimu ilikuja na sera ya “Education and Training’’ ,Mwaka 2007 hadi leo kukawa na sera mbali mbali za kuboresha elimu lakini zote zimeshindwa kuandaa wasomi na wataalamu waliobobea badala yake zimezalisha wasomi walio na mchango mdogo katika kukuza uchumi wa taifa.

Ni ukweli usiopingika ya kuwa hatuwezi kupiga hatua katika nyanja mbalimbali za kiuchumi bila kuwa na mfumo bora wa elimu, mfumo huo bora utakua chachu ya uzalishaji wa tabaka la vijana na wasomi mahiri ambao watasaidia kuleta mapinduzi katika shughuli tofauti za uzalishaji kama kilimo,viwanda,madini,utalii afya na mengineyo hivyo basi kupelekea ukuaji mkubwa wa uchumi wetu kutoka uchumi wa kati hadi uchumi wa juu.

Kwa mfumo wa elimu uliopo sasa ni ngumu kwa Tanzania kama taifa kupata wasomi mahiri ambao wanaweza kusaidia kuleta maendeleo hususani katika kukuza uchumi wetu,Mfumo huu wa sasa unaendelea kutengeneza taifa la wasomi mbumbumbu au wasomi wasio na tija katika taifa .

Kuna mapungufu makubwa katika mfumo wa sasa, mapungufu hayo yamesababisha kutokea kwa wasomi wanaokariri badala ya kuelewa,wasomi wanaosoma ili kufaulu mitihani au wapate ajira,hivyo basi wasomi hawa wamechangia kwa kiasi kikubwa taifa kuwa tegemezi katika tekinologia hususani kwenye nyanja muhimu kama viwanda,madini,kilimo na afya.

Utegemezi huo umepelekea kusababisha serikali kutumia pesa nyingi katika kununua tekinologia ambayo ingeweza zalishwa humu humu ndani na wasomi wetu wenyewe ,Umesabisha serikali kutumia hela nyingi kulipa madaktari kutoka nje ,wakufunzi na wataalamu mbalimbali pesa ambayo huenda ingetumika katika kuboresha miundombinu ya nchi.

Yafuatayo ni mapungufu ya mfumo wa sasa

  • Mfumo wetu wa sasa umejikita zaidi kwenye elimu ya nadharia kuliko elimu ya vitendo kupelekea wanafunzi kushindwa kuelewa bali ukariri zaidi .
  • Mfumo wetu wa sasa umeshindwa kuandaa mitihani mahususi kwajili ya kupima uelewa wa mwanafunzi bali mitihani ya sasa upima uwezo wa kukariri wa mwanafunzi hivyo kupeleka wasomi waliofaulu vizuri darasani ila kichwani weupe.
  • Mfumo umefeli kumpa wanafunzi uhuru wakuwa wabunifu
  • Mfumo wetu umesababisha mwanafunzi kusoma taaluma ambayo haipendi kulazimisha mwanafunzi kuchagua masomo ambayo hayapo moyoni mwake ilikusudi tu afaulu
NINI KIFANYIKE ILI KUPATA TABAKA LA WASOMI MAHIRI AMBAO WATASAIDIA KATIKA KUPELEKEA TANZANIA KUWA NA UCHUMI WA JUU

  • Kuanzisha aina tatu za shule tokea level ndogo kabsa ya msingi ambapo shule hizo ni
  • Shule za kawaida hizi ni shule kama zilizopo sasa hivi shule hizi zitatumika kama sehemu ya kuelewa vipaji vya watoto tokea wakiwa wadogo kabsa darasa la kwanza mpaka la tatu kutakua na mchakato maalumu wa kuchuja watoto ,wale watoto wenye vipaji maalumu iwe katika taaluma au michezo wataamishwa na kupelekwa katika shule maalumu,ambapo katika shule hizo ndio mchakato wakupata wasomi wabobezi utaanza ,hawa wengine waliobaki wataendelea na taaluma zao kama kawaida kwenye shule hizi za kawaida.
  • Shule za vipaji maalumu hapa ndipo mchakato wakupata wasomi mahiri utaanza shule hizi zitatengenezwa kwa mfumo ambao utamfundisha mwanafunzi katika vitendo zaidi kuliko nadharia shule hizi zitakuwa na maabara za kisasa , kutakua na maabara fizikia kemia,biologia,Shule hizi zitakuwa na walimu waliobobea na mahiri .pia kwenye shule hizi kutakua na karakana za kumuwezesha mwanafunzi kuwa mbunifu na kumpa uhuru wa mwanafunzi kubuni tekinologia mpya ,Shule hizi zitakuwa na maktaba kubwa za kisasa zenye vitabu vya kutosha ,Wanafunzi hawa watafuatiliwa kwa karbu sana nakuangaliwa wapi mwanafunzi yupo vizuri sana kama ni hesabu basi watapelekwa kwenye madarasa mahususi ya hesabu kama ni biologia basi watapelekwa kwenye madarasa mahususi ya baologia hivyo hivyo kwa masomo mengine,Shule hizi zitakua kubwa nzuri na za kisasa kwa kila mkoa kutakua na wastani wa shule mbili,na shule hizi zitakuwa na msingi ,sekondari hadi sendari ya upili baada ya hapo wanafunzi wataenda vyuo maalumu vya kisasa ambavyo kutakua na vyuo watani kimoja kila kanda ,kwa kufanya hivi tutapata wataalamu wenye weledi ambao utatumika katika kuleta mapinduzi katika nyanja zote za uchumi
  • Aina tatu ya shule ni shule za michezo hapa watachujwa wanafunzi wenye vipaji kutoka zile shule za kawaida hivi ni vipaji vya michezo ,hizi shule zitakua na viwanja vya kisasa na waalimu maalumu wa kufundisha michezo lakini hii itaenda sambamba na elimu ya darasani lakini pia wanafunzi wataangaliwa kwa karbu katika vipaji vyao kama mpira wa miguu mpira wa nyavu,kuogelea na michezo mbalimbali hii itasaidia kwa hapo baadae kupata wawakirishi mahili katika michezo duniani na kuongeza pato la taifa kwa kodi kama wakishiriki na kushinda tuwe na wanamichezo waliobobea kila idara
  • Kubadilisha mfumo mzima wa mitiani na kupunguza masomo yasio na tija mashuleni
  • Hapa kutakuwa na aina mbili za mitiani kutokea shule za awali kabsa hapa mtiani wa kwanza ni wa kuandika kama kawaida na mtiani wa pili ni wa kuuliza mwanafunzi maswali ana kwa ana,Mitihani ya kuandika itabeba alama sitini na mitani ya maswali ya ana kwa ana itabeba asilimia 40
  • Pia kupunguza wingi wamasomo kumpunguzia mzigo mwanafunzi hii ni kwa sekondari kuanzia kidato cha kwanza mwanafunzi asome wastani wa masomo matano matatu ya mchepuo atakao chagua kama ni sayansi,art au biashara alafu mawili yawe masomo ya uraia na elimu ya kumpyuta..mengine kama ya dini yataku ya ziada tu na wala yasiwe kwenye mtaala hii itasidia wanafunzi kuwa makini zaidi kwa kuwa na mzigo mdogo
  • Ili kupata hela kwaajili ya kuwezesha mfumo huu mpya wa elimu uanzishwe mfuko mpya ambao utakusanya michango ya hiari kutoka kwa wadau mbali mbali watakao guswa,pia serikali ichukue zile pesa za magawio kutoka taasisi mbalimbili zilielekezwe uku na pia serikali ipunguze matumizi yasiokua ya msingi kwenye shughuli zake kama posho nyingi zisizo na tija kwa watumishi kama wabunge na wakurugenzi,kupunguza safari za kiserikli zisizo na msingi.
 
Mfumo wetu umesababisha mwanafunzi kusoma taaluma ambayo haipendi kulazimisha mwanafunzi kuchagua masomo ambayo hayapo moyoni mwake ilikusudi tu afaulu
Una maana ya mfumo upi. Huu unakuwa ni mfumo wa elimu? Au hali zote kimaisha bro?

Shule za vipaji maalumu hapa ndipo mchakato wakupata wasomi mahiri utaanza shule hizi zitatengenezwa kwa mfumo ambao utamfundisha mwanafunzi katika vitendo zaidi kuliko nadharia
Hilo ni jema, na ninafikiri ndio haswaa linalotekelezwa na shule za ufundi. Maboresho yaanzie kwenye shule za ufundi zilizopo.


Lakini lipo suala moja umeligusia la kupunguza mzigo wa masomo kwa watoto maalumu. Lakini napenda kuenda na dhana ya kwamba kila mtu anachojifunza cha ukweli, kila kipande cha ukweli (fact) na uzoefu kinamsogeza mahala pazuri zaidi kimaisha.

Mfano si sawa kupunguza masomo ya lugha, kwa wanafunzi wa uinjinia kwa sababu wataihitaji katika kuandaa mipangokazi katika 'planning their projects'.

Ndio maana napendekeza shule za msingi zibaki hivyo, za msingi na zifundishe yote ya msingi. Watu waanze kugawanyika hapo sekondari kufuata miito yao sasa. Maana nikuiloze swali jingine mleta mada, unafikiri ni halali kumfanya mtoto wa miaka 6,7,8 achague/achaguliwe maisha yake na kuwekwa kipaji maalumu mapema hivyo? Akibadiliaha maoni baadae maana bado ni mtoto akiona ndege atajiita rubani, akaona video ya wanamaji atajiita mvuvi, mara aone muvi atamani kuwa steringi tutajuaje? Haingekuwa bora mtoto wa form three miaka 16,17 au zaidi hivi ndio ajiweke wakfu sasa??
 
Back
Top Bottom