Shule za serikali kidato 5 wachache waripoti baada kucheleweshwa mwezi mzima, wengi walishaanza shule binafsi. Mabweni na madarasa yamekamilika?

Halafu sasa hivi hata selection zilizofanyika hazieleweki,

Kana kwamba goli limeongozwa ufaulu ukazidi?!

Division 1 Shule zile best eti anapekwa Shule ya Kata ,
Tena nyingine unakuta ina Mwaka mmoja Au 2 tu tangu kuanzishwa.

Kama kuwakomesha vile?!

Wangekuwa wanaweka vigezo wazi wananchi waelewe,

Kwa nchi zenye wananchi wanajielewa kupata taarifa, ufafanuzi n.k ni mambo ya msingi Na muhimu.
 
Waziri mhusika ulikuwa ni mpango wako wa kujaza shule za binafsi kidato Cha 5? Ulichelewesha wanafunzi kuanza shule mwezi mzima kwa sababu ya ujenzi wa mabweni na madarasa.

Tunaomba utujibu ni shule ngapi madarasa na mabweni yamekamilika ndani ya mwezi mmoja na tayari yamepokea wanafunzi.
Ndiyo shida ya kuchanganya elimu na biashara
 
Hiyo miradi ya ujenzi haiwezi kukamilika kwa wakati kwasababu Wakurugenzi wa Halmashauri 'wameingilia' shughuli nzima ya ujenzi. Wanawasumbua sana Wakuu wa Shule na Kamati za Ujenzi mashuleni. Wanataka wao wasupply materials;kuanzia mchanga, nondo, kokoto, simenti na kila kitu. Waroho sana hawa DED persons.
 
Watoto wao walianza kidato cha tano mara tu baada ya matokeo mwezi 3 na 4 Feza schools, Marian, Mazinde Juu, Sant. Schools.

Halafu watoto wa wapiga kura wanasubiri shule za bure eti mwezi wa 8. Sidhani kama Kuna hata darasa wala mbweni lilolokamilika.
Hatari sana hii ishu
 
Back
Top Bottom