Shule za kata bado hali ni tete!

Bill of Quantity

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
1,233
405
Kiujumla aliyebuni wazo la shule za kata inabidi akae chini awaze tena kwa mara ya pili namna ya kuboresha elimu kuanzia shule za msingi ndipo za kata zitaendelea.

Shule nyingi za kata zilizoko nje ya majiji na miji, hali ni mbaya sana kwa kweli. Wanafunzi wanafika kidato cha nne ilhali bado ni hawako katika makali ya kukumbana na mtihani wa kidato cha nne, yaani CSEE!

Shule za kata kwa sasa zimekua sehemu tu ya watoto kwenda kukulia, sio kujifunzia na kupanda kwenda elimu ya juu!

Kwa data zilizoko mezani mpaka sasa ni kwamba, wanafunzi wengi huachia ngazi wafikapo kidato cha pili, sababu kuu ikiwa ni kutoelewa kabisa kinachoendelea darasani, lugha ngumu sana wajameni. Matokeo ya jumla unakuta kati ya watoto 50+, watano tu ndiyo wamefanikiwa kufaulu kwa division three tena ya mbali kweli.

  • Waalimu mpaka sasa hawatoshi kabisaa, achilia mbali serikali kutamba kuwa waalimu wa arts wametosha, lakini shule yangu ya kata iliyoko kijijini ina waalimu watano tu wa arts.
  • Serikali mpaka sasa ime-ban watoto wetu kusomea ualimu wa shule ya msingi katika ngazi ya kidato cha nne! waende wapi sasa?..
Hii labour force inayozalishwa na shule za kata bado ni shida tupu, serikali iliangalie hili kwa jicho lingine,

Shule za kata bado ziko matatani kuwa sehemu ya kukulia tu, siyo kuzalisha educative work force.

Karibuni tujadili hili janga.
 
Serikali imeban watoto waliomaliza kidato cha nne kusomea uwalim wa primary??? so wale waliomaliza kidato cha nne na kuchaguliwa kwenda kusoma diploma in primary education mwaka huu ilikuaje???
 
Serikali imeban watoto waliomaliza kidato cha nne kusomea uwalim wa primary??? so wale waliomaliza kidato cha nne na kuchaguliwa kwenda kusoma diploma in primary education mwaka huu ilikuaje???

waliochukuliwa kwenda ttc diploma ni wa daraja la 1-three,waliopata div 4,wameachwa helplessly.
 
Back
Top Bottom