goodmother
Senior Member
- Jul 21, 2012
- 108
- 77
takribani miezi 2 iliyopita niliingia hapa jamvini kuomba ushauri wenu, nanyi bila hiyana mlinishauri kadiri mlivyoona inafaa nashukuru sana kwni ushauri wenu niliuzingatia na mimi nikachanganya na mawazo yangu, nilikaa na mume wangu tukazungumza tuakakubaliana kutengana kwa muda wa mwezi mmoja ili kupima mienendo yetu ikiwemo yeye kuacha tabia zake, na kuahakikisha kweli watoto wanaosemekana ni wakwake wakapime DNA. alikubali mapendekezo yangu akafanya vile na watoto wameonakana siyo wa kwake!! kwani nilmwomba kama kweli ni wake asiwatelekeze kama alivyokuwa anafanya hapo awali,, mimi sipendi mtoto ateseke kwa kweli na nilipoona mazingira ambayo hao watoto walikuwa wanaishi nilingiwa na huruma na ndiyo sababu ya kumwomba awahudumie kama kweli ni wakwake. amekubali kujirekebisha ikiwemo pia mimi kurekebisa mapungufu ambayo alinieleza niyarekebishe,. NASHUKURUNI SANA KWANI USHAURI WENU NDIYO ULIONIPA UJASIRI WA KUONGEA NAYE KWA UTULIVU NA YEYE KUNIELEWA KULIKO ILVYOKUWA AWALI NILIKUWA NANYAMAZA NA WAKATI MWINGINE KUGOMBANA NA KUSUSA !! NAOMABA MUNGU AWE KWELI AMEJIREKEBISHA. NAZIDISHA SHUKURANI KWENU.