Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,258
- 20,712
Najua jambo hili linaweza kuwa gumu kwa wengi,hii ni kutokana na mazoea.Hebu tutoke kwenye mazoea. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Ni jambo la kawaida kusikia kauli kama "hivi we mtoto nikikuambia unilipe kwa jinsi nilivyokulea utaweza" au "we mtoto huna shukrani,nimekulea vyema hivi" au "sijui nikulipe nini kwa malezi yako kwangu" n.k,kauli hizi mara nyingi hutolewa na wazazi au jamii inayotuzunguka au na watoto,kwanini uwaze kulipa mtu fadhila kwa kufanya kazi aliyojitakia mwenyewe tena kwa raha zake bila kukushirikisha?Ooo sijui nikulipe nini mama/baba kwa kunilea ili iweje?. . . . . . . . , . . . . . . , . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Hivi kulea mtoto ni sadaka?Au ni hisani?Wakati unamtafuta mtoto unajua kabisa atakachohitaji na yeye wakati huo hayupo na hachangii kwenye mjadala wenu,kwa kifupi hausiki na mipango ya kumleta duniani,iweje leo kumpa yaliyo HAKI yake ifananishwe na msaada?Mnawanyanyasa watoto kisa malez,kwa nini? . . . . . . . . , . . . . . . . . , . . Kumlea mtoto ni LAZIMA na mtoto asihusishwe na ujinga wa kumtisha kuhusu malezi.Najua hii ni ngumu kwa wengi,kwani ndivyo tumekaririshwa kutokujaji haya eti tutapata laana,ujinga tu.Usiogope malezi ni haki ya mtoto yoyote na hatakiwi kutishiwa nayo.Tuache kufikiri kimazoea ala!!!!