Shukrani kwa ukaribisho - Anna Tibaijuka

Hakikisha utakapokuwa unafanya kazi zako za Uwaziri uwe smart. Kurunzi la hapa ni kali sana. Humu wengi
wetu hatutumii majina yetu halisi, usije kushangaa siku unatoa statement ya uongo halafu anakuja hapa
msaidizi wako with evidence kukanusha au kuponda.

Take it!
 
Gombea urais mama, wanaume wengi wamechafuka na ufisadi, waliopo hatuwataki wanaotaka tuwape hatuwaamini. Okoa jahazi
 
Karibu sana mama.

Kwangu mama ni jina zuri la kumuita mtu ninamuheshimu kama wewe. Mwingine ningemwambia karibu Prof.

Mimi nakuahidi ushirikiano. Kati ya ushauri ambao nakupa ni huu

1. Pale ambapo swali umeulizwa lina maslahi mapana ya Taifa na majibu yake ni magumu " hasa pale linapogusa maslahi ya vigogo", mwombe Mungu akupe Hekima ya kujibu. Ni afadhali kubak kimya kuliko kujibu porojo ama siasa has kwenye maswala ya ardhi na makazi
2. Sina shaka na uzalendo wako. Kufa kwa ajili ya kusimamia kweli. Napo hapa mwombe Mungu Hekima.

Sasa maswali.
1. Wageni wengi sasa wanamiliki ardhi. Naamini si kosa wageni kuwa na ardhi ila kwa utaratibu maalumu kama kwa kupitia TIC. Kwa hali ilivyo sasa wengine hata huku uswahilini wamenunua na wanaishi. Wewe unalizunguziaje hili?

2. Wakati wa awamu ya kwanz ya uongozi wa nchi, Masaki na Oysterbay waliishi viongozi wa serikali. Hali si hivyo sasa. Pamekuwa uswahilini kwa tafsiri hapana hadhi ya kuishi viongozi wa serikali. Je, nini kilitokea ? Huo umuhimu hauonekani sasa?

3. Dokeza kidogo kuhusu Satelite cities in DSM. Ziko ngapi? Wapi?

Asante mama.
 
Mheshimiwa Prof Tibaijuka,nchi za wengine ardhi yote kwa matumizi ama matumizi ya baadaye zimepimwa na mifumo ya GPRS IKAWEKWA .Hapa Dar es Salaam nafikiri zaidi ya 75% ni makazi holela?Wizara yako kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Kilimo zina mpango gani kuhakikisha TANZANIA ILIYO NA MIPANGO-ARDHI SIYO TU MIPANGO MIJI INAWEZEKANA?Mawazo yangu ni kwamba kwa kutopima hata serikali inajinyima mapato ya survey ,na kulea umaskini
 
Mama Tibaijuka karibu saaaana JF. Naamini hapa utapa mawazo ya wananchi mbalimbali juu ya utendaji wa wizara unayoongoza na kubwa zaidi maeneo ambayo yanahitaji kuboreshwa.

Kwa bahati mbaya sana governance system yetu Tanzania hadi sasa haihusihishi 'research'. Imekuwa ni kawaida kwa viongozi kufanya kazi 'mezani' na kuja kututangazia! JF, kama utaitumia vizuri inaweza kukuweka karibu na wananchi ambao kimsingi ndio wadau wakubwa wa wizara yako.

Ninayo mambo mengi kuhusu ardhi lakini kwa leo ningetaka kupata maoni yako juu ya mambo machache japo mengine si ya ardhi, lakini kama mmoja wa kiongozi mwandamizi serikalini unaweza kutoa mchango pia:


1. Nini mawazo yako kuhusu MONSATO? Na kwa nchi kama Tanzania ambayo quality control system kwa karibu kila kitu is very weak, kuna kitu mkakati gani umewekwa ili kumlinda mwananchi wa kawaida kuhusu GMO?

2. Mwaka jana, wakati bunge la budget kulikuwa na zoezi la uvunjwaji nyumba kwenye maenezo ya fulani Dar es salaam kwa madai kwamba nyumba hizo zimejengwa kwenye maeonoe ambayo hayaruhusiwi. Zoezi limefikia wapi? Ni nyumba ngapi zimevunjwa na ngapi zimebakia? Na hizo zilizobaki zitavunjwa lini?

Karibu mama.
 
karibu sana mama. nina hakika tutachota mengi kutoka kwenye kisima chako cha busara na uzoefu wako!
 
Karibu sana jukwaani, Ninaacha dokezo ili Mheshimiwa Tibaijuka ujipange vizuri kabisa.Nikirudi hapa nitajielekeza zaidi juu ya migogoro ya ardhi na makazi katika maeneo ya vijiji vya Kakunyu,Mabare,Bubare ambako wanawanchi wamechomewa nyumba(makazi), kufukuzwa,kufurushwa,kudhalilishwa, na kupoteza utu wao, huko wilayani Missenye Kagera.Ninajua unajua.Maswali yangu yatajikita Missenyi.Sitaongelea Meatu mkoani Shinyanga na Muleba na kwingineko nchini.Najua unajituma kifikra, hutakuja na hadithi zilizomo ndani ya kitabu cha Duka la Kaya.Madamu tunaelekea mwishoni mwa msimu watakuja hapa wengi wa sampuli yako.Lakini....................... Nawashukru wanakupongeza na kukuita Iron Lady wa Tanzania.
 
Karibu sana mama kwenye forum yetu. Ningependa kujua ni kwanini mpaka leo amri ya kubomolewa jengo la ghorofa uliyoitoa haijaanza kutekelezwa na walioulizwa wanatoa majibu ya ubabaishaji, je kuna mgongano wa madaraka unaokwamisha agilo lako kutekelezwa?
 
Naomba kukushukuru na kukukaribisha tena jamvini Prof. Mama Anna Tibaijuka.

Naamini mwisho wa siku hutapokea amri kama ile aliyotoa Makamba wakati midahalo ya mwaka 2010 iliyoandaliwa na TBC1.
 
Last edited by a moderator:
Aisee, very impressed by the confidence u've shown....karibu sana mama!! Salam kwa Mr. President, nafahamu yupo bize lakini si mbaya endapo akitenga angalau siku moja katika kila baada ya miezi mitatu akawa anajitokeza hapa JF! Nikiri wazi kwamba ni jukwaa ambalo linaweza kumkosea adabu (toka kwa baadhi ya members) lakini inputs atakazopata zitakuwa na manufaa makubwa zaidi kuliko dhihaka atakazokumbana nazo!

Karibu sana mama Anna Tibaijuka....
 
Last edited by a moderator:
Aisee, very impressed by the confidence u've shown....karibu sana mama!! Salam kwa Mr. President, nafahamu yupo bize lakini si mbaya endapo akitenga angalau siku moja katika kila baada ya miezi mitatu akawa anajitokeza hapa JF! Nikiri wazi kwamba ni jukwaa ambalo linaweza kumkosea adabu (toka kwa baadhi ya members) lakini inputs atakazopata zitakuwa na manufaa makubwa zaidi kuliko dhihaka atakazokumbana nazo!

Karibu sana mama Anna Tibaijuka....
 
Last edited by a moderator:
Karibu sana na hongera kwa ujasiri wako.

Swali:
Ni mabadiliko gani ya ardhi na makazi ungependa yajumuishwe kwenye katiba mpya?

Asante
 
Nimeipenda sana hii huyu mama Makinda anatakiwa aigw huu mfano wa mama tibaijuka ili na yy athibitishe uwajibikaji wake kwa jamii ya watanzania.
Hongera sana Mama etu uliye makini. Tunaomba umshaur na Anna Makinda ajiunge, tuna maswal mengi ambayo nahisi yeye atakua na majibu.
 
Safi sana prof. I stand to be corrected kwamba prof. Tibaijuka ni verified member ambaye ni prof. Wa kwanza hapa jukwaani....zaidi naona dr kitila mkumbo but sijaona prof, so u opened the door for more professors to join jf as verified members....old but kidigitali zaidi, nimekupenda...viva mzazi
 
Back
Top Bottom