Shukrani kwa ukaribisho - Anna Tibaijuka

Mimi swali langu liko katika Utoaji wa Hati za Aridhi, je Wizara inajipanga vipi kuhakikisha Hati zinapatikana kwa urahisi bila usumbufu wowote ule?
 
Ndugai yupo sana humu, tatizo lao wanchungulia na kutoka. Ni ujasiri tu uliyomfanya huyu mamakufanya kama akina dr slaa, Kigwangala, the late Regia Mtema(RIP), nk. Tutoe wito tu kwa wengine kufanya hivyo
Karibu sana Mama hapa uvumilie yote utakayokutana nayo....mwambie na ndungai naye ajiunge...karibu sana Mama yetu.
 
Karibu sana mama,

Kuna majukwaa mengi humu, kuna jukwaa kinaitwa MMU tunajadili mambo ya familia si unajua msingi wa taifa bora ni familia bora
karibu sana kule sio huku kwenye siasa tu
 
Dada naomba updates za Kigamboni. Mimi nina kaeneo Vijibweni karibu .na kwa Dr Kibelloh. Muda umekwenda tangia tuzuiwe kuviendeleza viwanja vyetu.
 
Mama Tibaijuka hii inatia moyo sana.

Karibu sana kwani hii itasaidia kuwaonyesha wengine UMUHIMU WA MAWASILIANO YA KUPITIA HAPA JF ili ile issue ya kutaka JF ifungwe ionekane kuwa HIZO ZILIKUWA NI NDOTO ZA MAWAZO MABOVU.
 
Karibu saana mama! Ulichonifurahisha wewe sio muoga kama wengi wa kutoka chama chako! Hata namba ya simu sio issue kwako
 
imependeza kukubali ukaribisho. Jitahidi kujibu hoja zitakazoletwa
 
Mh wakati ukuta huwezi kupigana nao, hali halisi ndo hii instant communication,wahenga walisema ujana maji ya moto,ukikereka take it lightly and just be aware siku hizi magazeti mengi source yao ni hizi public forums na blogs.Naamini uwepo Wako utapanua uwigo wa E government,karibu mama.
 
Asante sana kwa kupokea ukaribisho wetu...nasema tena karibu sana.

Naomba kujua kuna utaratibu gani au sheria inasemaje kwa mgeni kununua/kumiliki ardhi ya Tanzania...?

Kuna maeneo na mashamba mengi tu maeneo ya Rufiji wamekuwa wakiuziwa wageni...na wengine kuwalaghai vijana wa kitanzania kwa sababu ya ignorance na umaskini wananunua au kuuziwa ekari za ardhi on behalf!

Hili unalizungumziaje mama?
 
Welcome our glandmother,we are sure that,you wll be with us in diffent issues especially conserning nation matter.Please be truthfull and transparance becouse Tanzania is our all,I love u and i apreciating you.Nyegera mkaile waitu.
 
Mimi swali langu Mama lirudi nyuma sana!

...Hivi ni nini kilichoua BAWATA? Wakati ule unaanzisha BAWATA na UWT-CCM ilikuwepo! Je ulihisi UWT haina dira ya kumkomboa mwanamke? Nini kimeongezeka ktk UWT ya leo ambacho kulikufanya uanzishe BAWATA kama mbadala? Nini maoni yako kwa UWT kubeba jina na assets za kitaifa wakati kuna wanawake wengine ambao si wana CCM?(Mfano Mama yangu Sekindole kule Mafinga Kinyanambo)
 
...Warmly welcome Prof....labda kwa kuanzia tu chukua pongezi zooote hizi unazopata humu JF na kuzi translate kwa viongozi wenzako serikalini.....ili waone kuwa hii JF si adui wa serikali bali ni sehemu ya watanzania (tena wasomi) wanaoguswa na matatizo yaliyopo TZ na wanaotaka serikali yao iwatumikie.....

...Pokea karibu zote hizi na kuzifanya kama challenge dhidi ya utendaji wako na viongozi wenzako wizarani.....huku ukijua kuwa haya yanayosemwa humu JF ni representation ya watanzania wote...haswaa wale wasiopata fursa ya kutoa dukuduku zao kwa viongozi wao.....
 
karibu sana prof
naomba unapochangia bungeni wahimize wabunge wenzio na mawaziri nao wajiunge humu
pamoja na spika na makamu wake
woga wao unamaanisha hawafanya kazi kwa hali na uwazi.
ujasiri wako nimeukubali,
 
Back
Top Bottom