Should men be kept away from the delivery room?

Bora umejibu mwenyewe NN
Nilitaka kumwambia Mpangwa1 atofautishe mambo 2
1. Ndoa
2. Mtoto/watoto
Haya mambo hayana uhusiano wowote, pia ndoa haina definition, labda kutumia definition ya imani za kidini ambazo anazo hazina mshiko kwa sasa.
Mimi niliingia labour ward nikiwa na umri mdogo sana (chini ya miaka 15) kimakosa nasisitiza kimakosa. Niliyoyashuhudia wakati huo, nadhani kila mtu (hasa mwanaume) aingie kwa hiari yake. Nilijifunza kuwa mazingira ya labour wards ndio yanafanya baadhi ya wakunga kuwa fyatu fyatu
Mpangwa1, unaona mimi sikuwa na ndoa na wala sikuwa nakwenda kuzaa na niliingia, any connection kwenye hoja yako?

Hata mie mwenyewe niliwahi kuingia delivery room, sikwenda kuzaa ila shost wangu alienda kujifungua.

Niliyoyakuta huko sikuweza kuamini japo mwanamke, toka siku hiyo nina uoga wa kuzaa asikwambie mtu. Kwa upande wa mwanaume kwa hiyari yake anaweza kwenda au lah!!I think is better u guys to go there labda inaweza kuwafanya kuwaheshimu wake zenu.
 
Rafiki yangu mmoja aliingia derivery room,baada ya kuona mtoto anaanza kutoka jamaa alizimia manesi wakaanza kumshughulikia tena, hakuweza kumuona mtoto mpaka kesho yake. Jamaa kaapa hatokanyaga tena delivery room.
 
Hata mie mwenyewe niliwahi kuingia delivery room, sikwenda kuzaa ila shost wangu alienda kujifungua.

Niliyoyakuta huko sikuweza kuamini japo mwanamke, toka siku hiyo nina uoga wa kuzaa asikwambie mtu. Kwa upande wa mwanaume kwa hiyari yake anaweza kwenda au lah!!I think is better u guys to go there labda inaweza kuwafanya kuwaheshimu wake zenu.

Subiri sasa zamu yako ndo utakuja utusimulie vizuri hapa ndani,mi nitaenda tu kama nitaambiwa nikienda itaongeza ladha ya kumegana tu!!
 
mi naona wasiwapige marufuku kuingia labour rooms, wawape uhuru wanaopenda kuingia waingie, wasiopenda wasiingie na wanaoingia wawe uhuru kuwepo mpaka watakapojisikia hawapo comfortable watoke wakasubirie nje..

ila kwa uzazi kama wa labour zetu hizi za kawaida za bongo, ambako wanawake kadhaa wako pamoja na kila mtu ana fanya kazi ya kujifungua kwa style yake na attitudes za manesi etc bora wasiingie let us spare them the embarrasment...

mume wangu baada ya kuingia labour attitude yake ilibadilika akawa makini sana katika kusaidia wakati wa process ya ku recover na katika malezi ya mtoto mchanga, tofauti na ilivyokuwa nilipojifungua mara ya kwanza ambapo hakushuhudia
 
Hata mie mwenyewe niliwahi kuingia delivery room, sikwenda kuzaa ila shost wangu alienda kujifungua.

Niliyoyakuta huko sikuweza kuamini japo mwanamke, toka siku hiyo nina uoga wa kuzaa asikwambie mtu. Kwa upande wa mwanaume kwa hiyari yake anaweza kwenda au lah!!I think is better u guys to go there labda inaweza kuwafanya kuwaheshimu wake zenu.

kweli mwaya waingie waone ni kiasi gani neno la mungu linatimia kwamba " tutazaa kwa uchungu" waone mateso tunayopata ..heshima mbele
 
Mi mwenyewe nilikwenda wakati binti yangu anazaliwa, nilikuwepo kuanzia zile preliminary process za kupima njia, kutundikiwa Drip ya maji ya uchungu, kuona kile kimkanda wanachovalishwa tumboni kilichokua connected kwenye mashine ya ku monitor mapigo ya moyo ya mtoto, mpaka chupa kupasuka nilikuwepo.

katika delivery process nilikuwepo mpaka nywele za mtoto zikawa ninaonekana lakini mtoto akawa anatoa kichwa kidogo na kurudisha, Nilitishika sana wanilisikia manesi wakisema kua mke wangu ameishiwa nguvu na hawezi tena kusukuma, kwa sababu uchungu ulikua masaa 9 kuanzia saa 3 asubuhu mpaka saa 2 usiku.
Hapo manesi wakanitoa nje na baada ya dk25 nikasikia mtoto analia.

Nilivyokuja kumuuliza ilikuaje mbona nilipotoka tu mtoto alitoka, wife akaniambia walimwongeza njia kwa kisu. Tangu siku hiyo naheshimu sana wanawake na nimekua na mtizamo tofauti kabisa kwa wanawake.
Ila sipendi tena kushuhudia hiyo process. It is to dificult. Naona ni vyema wanaume walazimishwe kushuhudia angalau mara moja katika maisha yao, hii itawaadabisha wanaume wanaowanyanyasa wanawake.
 
Mi mwenyewe nilikwenda wakati binti yangu anazaliwa, nilikuwepo kuanzia zile preliminary process za kupima njia, kutundikiwa Drip ya maji ya uchungu, kuona kile kimkanda wanachovalishwa tumboni kilichokua connected kwenye mashine ya ku monitor mapigo ya moyo ya mtoto, mpaka chupa kupasuka nilikuwepo.

katika delivery process nilikuwepo mpaka nywele za mtoto zikawa ninaonekana lakini mtoto akawa anatoa kichwa kidogo na kurudisha, Nilitishika sana wanilisikia manesi wakisema kua mke wangu ameishiwa nguvu na hawezi tena kusukuma, kwa sababu uchungu ulikua masaa 9 kuanzia saa 3 asubuhu mpaka saa 2 usiku. Hapo manesi wakanitoa nje na baada ya dk25 nikasikia mtoto analia.

Nilivyokuja kumuuliza ilikuaje mbona nilipotoka tu mtoto alitoka, wife akaniambia walimwongeza njia kwa kisu. Tangu siku hiyo naheshimu sana wanawake na nimekua na mtizamo tofauti kabisa kwa wanawake.
Ila sipendi tena kushuhudia hiyo process. It is to dificult. Naona ni vyema wanaume walazimishwe kushuhudia angalau mara moja katika maisha yao, hii itawaadabisha wanaume wanaowanyanyasa wanawake.

October sina la kuongeza hapa ila nimejikuta machozi yananitoka

i feel it
 
thanks mvina unajua kama umeumwa uchungu sana at last mtoto akashindwa kutoka duuh ni balaa we acha tu asikwambie mtu unaweza tamani usizae tena ..ila sir god katuwekea siri sijui ni kusahau au...
 
thanks mvina unajua kama umeumwa uchungu sana at last mtoto akashindwa kutoka duuh ni balaa we acha tu asikwambie mtu unaweza tamani usizae tena ..ila sir god katuwekea siri sijui ni kusahau au...

Niliwahi kumuuliza mwalimu wangu wa biology nilitaka atusimulie hayo maumivu yakoje akanishauri nisuri hadi nikioa ndo ni muulize ma wife so still nasubiri.Heshima kwenu!
 
...kuna mengi delivery room kiasi kwamba ukiyajua yote hutathubutu kuchungulia...

kuna watoto wanaotanguliza miguu au makalio (breech), ...kuna kifafa cha mimba (Eclampsia), inawezekana mtoto ni mkubwa kuliko njia, nk nk...

Waliosema Mwanamke kujifungua ni 'mguu ndani, mguu nje' ya kaburini hawakukosea.

Mwanamke anayemng'ang'aniza mumewe Labour room kaamua tu kumtia adabu (mumewe)...

Hata kwa mikwaju siingii ng'oo!
 
wanaume waliowahi kuingia watupe maoni yao..hii itasaidia zaidi kujua kama waendelee kuona au wazuiliwe.

mie wangu aliingia kwa katoto ka mwisho, anasema anajuta kwanini aliingia na alitamani awaambie ma doc wanifanyie operation, na amaetokea kumpenda sana huyo mtoto mana alimshuhudia kuingia kwake duniani, ilimshtua/aliogopa mpaka akasema hawa wawili tulionao wanatosha na ile ctuation imemfanya awe na huruma zaidi, hata tukikutana na mama mjamzito mahali huwa anamuonea huruma sana na kusema Mungu amsaidie amalize safari yake salama....me kwa upande wangu nilifurahi alivyoshuhudia mana alinidekeza sana kwa wakati ule...lol
 
...ndivyo ilivyo, ...2nd born wangu alizaliwa kwa hiyo 'Breech', we acha tu. Wawili hawa wananitosha!
 
This mIraculous process has an effect on attitudes and behaviour not only of men but also women.Wanawake wengi wakishazaa huwa na heshima zaidi na upendo mkubwa kwa mama zao.

true kabisa, yaani mie nilivyomaliza tu kujifungua baby wangu wa kwanza nilijishtukia tu nauliza mama yangu yupo wapi, hapana heshimuni wanawake jamani, mie huwa namuheshimu sana mtu anaeitwa mama.

Similar Discussions

Back
Top Bottom