Kiroboto10
Member
- Nov 30, 2023
- 71
- 296
Ndugu Waziri wa Afya Ummy Mwalimu,
International Center for AIDS Care and Treatment Program - ICAP, Mkoa wa Mwanza, shirika halijalipa mishahara ya watumishi wake kwa miezi 3 sasa. Hakuna taarifa kwanini hawajalipa mishahara kwa miezi 3. DAS na RACC (wasimamizi wa kazi na mikataba) hawatoi majibu kwa wafanyakazi.Pia, wakati wa kuajiri watumishi wa ICAP katika mkoa wa Mwanza, hawakutoa pesa za kujikimu kwa watumishi. Watumishi walisafiri kwa gharama zao.
Haijalishi mtumishi anatokea eneo na umbali gani, watumishi waliofaulu usaili walitakiwa kufika katika vituo vyao vya kazi kwa muda waliopangiwa. Mwaka umemalizika, pesa za kujikimu watumishi wa ICAP - Mwanza hawajarejeshewa na hakuna maelezo ya ziada au ufafanuzi wanapewa kutoka kwa waajiri.
Mkataba wa ICAP na mtumishi unasainiwa chini ya Mkurugenzi wa Halmashauri lakini mwajiri halisi na anayelipa mishahara ya watumishi ni ICAP - MSPH. Wilaya zote saba za Mkoa wa Mwanza, anayeendesha mradi wa UKIMWI na KIFUA KIKUU ni ICAP - MSPH. Zote hajalipa watumishi mishahara kwa miezi mitatu.
ICAP wanashirikiana na Tanzania tangu 2004 kupunguza maambukizi ya VVU wakati wa kujifungua na kuongeza kasi ya matunzo na matibabu ya VVU. International Center for AIDS Care and Treatment Program - ICAP inafanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Wizara ya Afya (Wizara ya Afya Tanzania )
ICAP wanafanya kazi na Wizara ya Afya kutoa msaada kujenga uwezo na usaidizi wa kiufundi (TA) kwa ajili ya programu za kitaifa za VVU na kifua kikuu (TB). ICAP imejikita katika msaada wa kiufundi kuimarisha na kupanua kinga, matunzo na matibabu ya VVU, tohara ya hiari ya matibabu kwa wanaume (VMMC), Pia, huduma ya utambuzi wa TB kwa watoto na huduma ya TB/VVU, na watoto wanaoanzishwa na mtoa huduma. upimaji wa VVU na ushauri nasaha. Mchezo huu ni utapeli, kuaminisha watu ICAP wanaweza kutibu Kifua Kikuu (TB) na UKIMWI wakati hata uwezo mishahara ya watumishi hawawezi.
Wizara ya Afya imetulia kama ujinwa mgonjwa kwa kuwa imeingia mkataba na ICAP, ikiamini huduma ipo na inaendelea vizuri ikifanywa na ICAP - MSPH. Mnahatarisha maisha ya wagonjwa wa Kifua Kikuu (TB) na UKIMWI, na pesa mfadhili anatoa. Tuelezeni, pesa zipo wapi? Wizara mnajua fedha zilipo? Au, Wizara ya Afya tuelezeni haraka, mnaingia, mkataba na matapeli, au Wizara inashirikiana na coordinators wa Mwanza kutafuna fedha za mfadhili.
Source: Twitter page ya, MMM, Martin Maranja Masese
View: https://x.com/IAMartin_/status/1730625620856438883?t=E6Q8hbd5gAU8ak2UMDtEvw&s=09