Boran Jakutay
Senior Member
- Apr 8, 2023
- 110
- 255
Mtoto mwenye umri wa miaka saba mkazi wa Mtaa wa Sido, Kata ya Ibinzamata, Manispaa ya Shinyanga, amechomwa moto mikono yake yote miwili na mama yake mzazi kwa madai ya kula wali uliokuwa umebaki.
Emanuel Kayange ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Sido, amekemea kitendo hicho, huku mtoto mwenyewe akisema mama yake huyo alichukua nailoni, akaiwasha na kumchoma.
Kamanda wa Polisi Shinyanga, Janeth Magomi, amethibitisha kutokea tukio hilo na kusema wanamshikilia mwanamke huyo anayefahamika kwa jina la Grace Godwin.
Chanzo: East Africa TV