Shinyanga: Mama amchoma moto mwanawe kwa tuhuma za kudokoa wali

Boran Jakutay

Senior Member
Apr 8, 2023
110
255
Mtoto mwenye umri wa miaka saba mkazi wa Mtaa wa Sido, Kata ya Ibinzamata, Manispaa ya Shinyanga, amechomwa moto mikono yake yote miwili na mama yake mzazi kwa madai ya kula wali uliokuwa umebaki.

Emanuel Kayange ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Sido, amekemea kitendo hicho, huku mtoto mwenyewe akisema mama yake huyo alichukua nailoni, akaiwasha na kumchoma.

Kamanda wa Polisi Shinyanga, Janeth Magomi, amethibitisha kutokea tukio hilo na kusema wanamshikilia mwanamke huyo anayefahamika kwa jina la Grace Godwin.

Chanzo: East Africa TV
 
Watoto siku hizi hawasikii yaani walezi tuwe makini maana wanaweza wakakupeleka pabaya yaani hawaelewi chochote hata ukitumia kuongea na nini? Yaani
 
Sasa mama anamchoma moto mwanae nn??
Wizi, udokozi na ujambazi si ni maadili bora ya mtanzania?

Angekua shoga au msagaji hapo sawaa.
kazi ipooo na badoooo.
 
Back
Top Bottom