Shinyanga: Mbaroni kwa tuhuma kumnajisi mtoto wake wa kambo

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,320
5,485
Mkazi wa Ndala Manispaa ya Shinyanga (26) (jina limehifadhiwa), anashikiliwa naJeshi la Polisi Mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kumnajisi mtoto wake wa kambo mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 11.

Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Shinyanga, George Kyando akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, alisema tukio hilo limetokea juzi Aprili 9, 2022, saa 8:30 mchana.

Alisema mtuhumiwa alimnajisi mtoto huyo wakati mama yake akiwa ameenda dukani, na kisha kumsababishia maumivu sehemu zake za siri na kutokwa damu.

"Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga tunamshikilia mwanaume mmoja mkazi wa Ndala Manispaa ya Shinyanga kwa kosa la kumbaka (kumnajisi) mtoto wake wa kambo," alisema Kyando.

Aidha, alisema upelelezi bado unaendelea, na kwamba mtuhumiwa akikutwa na hatia atafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Katika hatua nyingine Kamanda alitoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo wa Shinyanga kuacha kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.

Chanzo: Nipashe
 
Kesi ya mchongo kumfunga Baba maaana njia zote za kiza zimeshindikana watu wanataka Mali duniani hakuna haki
 
Mkazi wa Ndala Manispaa ya Shinyanga (26) (jina limehifadhiwa), anashikiliwa naJeshi la Polisi Mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kumnajisi mtoto wake wa kambo mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 11.

Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Shinyanga, George Kyando akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, alisema tukio hilo limetokea juzi Aprili 9, 2022, saa 8:30 mchana.

Alisema mtuhumiwa alimnajisi mtoto huyo wakati mama yake akiwa ameenda dukani, na kisha kumsababishia maumivu sehemu zake za siri na kutokwa damu.

"Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga tunamshikilia mwanaume mmoja mkazi wa Ndala Manispaa ya Shinyanga kwa kosa la kumbaka (kumnajisi) mtoto wake wa kambo," alisema Kyando.

Aidha, alisema upelelezi bado unaendelea, na kwamba mtuhumiwa akikutwa na hatia atafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Katika hatua nyingine Kamanda alitoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo wa Shinyanga kuacha kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.

Chanzo: Nipashe
Akatwe pumbu na uume wote tena hadharani
 
Back
Top Bottom