Shinyanga: Kiongozi wa CHADEMA aumizwa vibaya, akimbizwa hospitali

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Wakuu,

Habari nilizozipata punde ni kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA tawi la Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga (jina sijalipata vema) amechomwa mkuki usiku wa kuamkia leo mpaka utumbo ukatoka nje. Amekimbizwa hospitali muda si mrefu ili kuyanusuru maisha yake.

Mwandishi aliyechukua tukio hilo ameanza kusumbuliwa sana na watu wanaohisiwa kuwa viongozi wa CCM ili kuiharibu kamera yake.

Chanzo: Mashuhuda walio eneo la tukio

===========
UPDATE
===========

Sasa ametolewa theatre kupelekwa ICU. Vitu viwili mpaka sasa vinashangaza.

1. Pamoja na Polisi kupewa taarifa tangu saa 8 usiku hawajafika eneo la tukio, wala hakuna dalili za wao kufanya hivyo kwa ajili ya hatua zaidi.
2. Kuwepo kwa viongozi wawili senior wa CCM eneo la hospitali wakilazimisha kuingia chumbani kwa daktari aliyefanya operesheni. That was a bit unusual kwa hiyo ikaibua curiosity ya habari, waliposhtuka kuwa wamepigwa au wanapigwa picha, wakaanza kumsakama mwandishi aliyekuwepo eneo la tukio wakitaka kumnyang'anya kamera kwa nguvu.

Nitaendelea kuwajuza. Asante mod kwa kuweka breaking news kadri...
Nimepigiwa simu saa 11 alfajiri, nikajaribu Kimpigia simu mkuu wa kituo cha polisi, lkn kwa maelezo yake alikuwa Hana taarifa kuhusu tukio Hilo.

Polisi hawajafanyia kazi taarifa tulizowapa mapema, kwani viongozi wa CCM wamedhamiria kuhakikisha wanatumia vijana wao kwenye kata hiyo ili wafanye mauaji na ndio wameanza kazi.

MUNGU amsaidie kamanda wangu apone haraka na kata tuichukue saa 4 asubuhi.
 
CCM wanauana wenyewe kwa wenyewe kwa rushwa na kuua wapinzani kwa silaha. JK chochea tu kuni mbichi chakula kiive
 
Habari mbaya sana hii lakini hiyo ndio hali halisi kwamba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wa raia vimeshindwa kutimiza wajibu wake. Na hiyo ni baada ya kukubali kubinafsishwa kwa ccm hali inayopelekea ccm kufanya kila aina ya maasi bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria.

Nadhani huko tunakoelekea tutalazimika kutafuta mbinu za kujilinda sisi wenyewe, hasa tunapokuwa katika michakato ya uchaguzi kwani matukio ya kuvamiwa, kujeruhiwa na kuuwawa kwa viongozi wetu nyakati za uchaguzi yamekuwa yakiongezeka kila kukicha.
 
Wakuu,

Habari nilizozipata punde ni kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA tawi la Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga (jina sijalipata vema) amechomwa mkuki usiku wa kuamkia leo mpaka utumbo ukatoka nje. Amekimbizwa hospitali muda si mrefu ili kuyanusuru maisha yake.

Mwandishi aliyechukua tukio hilo ameanza kusumbuliwa sana na watu wanaohisiwa kuwa viongozi wa CCM ili kuiharibu kamera yake.

Chanzo: Mashuhuda walio eneo la tukio

Tunamuombea mungu ampe ahueni apone mapema kabla ya uchaguzi
 
Yote haya ni kwa sababu wale waliomuua mwenyekiti wa chadema wa usa river kwa kumchinja walitengenezewa mazingira wakatoroka sasa wauwaji wa ccm hawaogopi kufanya jambo lolote dhidi ya mtu yoyote anaowazidi katika medali za siasa.
CCM ni chama cha mauaji, mkishindwa sera mnamuua aliyewashinda kwa sera.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Inaonekana hii imeanza kuwa kawaida ya chaguzi zetu, ccm hawakuzoea hali ya kubanwa na kuzidiwa kisiasa na wapinzani, hii inawakera na kwa kuwa wana nguvu ya pesa wanahonga wenye njaa kuwadhuru wapinzani wao kwa vipigo au kwa silaha
 
Sasa ametolewa theatre kupelekwa ICU. Vitu viwili mpaka sasa vinashangaza.

1. Pamoja na Polisi kupewa taarifa tangu saa 8 usiku hawajafika eneo la tukio, wala hakuna dalili za wao kufanya hivyo kwa ajili ya hatua zaidi.
2. Kuwepo kwa viongozi wawili senior wa CCM eneo la hospitali wakilazimisha kuingia chumbani kwa daktari aliyefanya operesheni. That was a bit unusual kwa hiyo ikaibua curiosity ya habari, waliposhtuka kuwa wamepigwa au wanapigwa picha, wakaanza kumsakama mwandishi aliyekuwepo eneo la tukio wakitaka kumnyang'anya kamera kwa nguvu.

Nitaendelea kuwajuza. Asante mod kwa kuweka breaking news kadri...
 
Mungu amusaidie Kamanda apone haraka ili afanikiwe kuona ushindi wa Chadema ktk kata ya Mawaza
 
Mara zote nimekuwa nikisema, bila kuwa na viongozi wazalendo,wanaoipenda nchi yao, bila kujali rangi zao,dini zao,kabila zao wala upande wao wanaotoka taifa litaendelea kuwa la amani na mshikamano. Tatizo viongozi wa ccm ni janga kwa mustakabali wa taifa letu.kwao kuua ni kawaida kwa maslahi ya kisiasa!
 
poleni sana wana mwawaza, shinyanga na chadema kwa ujumla, hizi ni jitihada za ccm kuwatisha wananchi ili wasijihusishe na upinzani.
MUNGU AKIWA UPANDE WETU JE TUMUHOFU NANI?
 
Thread hii huwezi muona zomba wala ritz na wale manyinyiemu et al, wao wanayafurahia haya, kamanda makene asante sana, mapambano ndiyo yalivyo hasa kwa utawala unaokaribia kuondoka haya hayana budi kutokea, makanda tusonge mbele naamini Mungu wetu ni mwema anayaona haya, na atafanya kitu.
 
Mh sasa kama wanataka nchi kwa kuua watu mbona patakuwa hapatoshi!
 
Tumesema mara kadhaa kwamba hawa watu ni wakatili kuliko hata KANU na ZANU PF. Tulikuwa hatujaona ukatili wao kwa sababu palikuwa hapajotokea chama cha kuwatisha kuwatoa madarakani. Bahati mbaya walio nayo ni kwamba watanzania wa leo hawatishiki tena na kwa hakikia hawana uwezo wa kuwaua watu wote wanaotaka mabadiliko katika nchi hii. Huu unyama wanaouendeleza utasaidia tu kuharakisha kuondoka kwao madarakani.

Tunamuombea huyo kamanda huko Shinyanga Mungu amuponye.
 
Hii sasa ni Hatari sana!! Ila Mungu Yupo!!
 
Back
Top Bottom