Shibuda apania kugombea dhidi ya JK CCM, ajitoa ghafla

Tunamtaka Rais wa umri wa Obama, aliyezaliwa na MKULIMA wa jembe la mkono. Atoke mikoa ya Lindi, Rukwa, Morogoro, Tanga,... na mingine inayofanana na hiyo.


WC
Unaweza kutupa sababu kwanini umechagua mikoa hiyo na si mingine kama Kilimanjaro Mwanza Shinyanga Kagera Mbeya etc.
 
Asante mkuu ila kwa sababu umeanza kusema -Charity Starts At Home of Great Thinkers

1.Nchi hii siyo ya CCM wala haitakuwa ya Chadema, nadhani ni muda mzuri wa kupigania mabadiliko ya katiba, serikali iwe ya umoja, itokane na asilimia za kura walizopata kwenye chaguzi, kila chama kiwe na mkono serikalini, hivyo ni jukumu la vyama vya upinzani kuwaza hili kwanza na ilikuwa first assignment since 1992

2. Tukimaliza hapo tubadili katiba ya kumpunguzia madaraka rais (kuteua jaji mkuu, mkuu wa polisi, wakuu wa majeshi, director wa PCCB, n.k)

3. Tukimaliza hiyo kazi kubwa tuanze na tume ya uchaguzi ambayo ni ya CCM, ikwe ya kitaifa

Baada ya hapo ndio tuwaze uchaguzi wa rais tukiwa tumeshajenga taifa la wote kwa ajili ya wote.

Then tuanze kuwaza uchaguzi wa rais na Chadema wamsimamishe mgombea wao , ambao wa sasa unamtaka Baregu.

kwa sasa naamini vyama vya upinzani ukwemo wewe hamna anayewazia hayo mambo matatu hapo juu, yanasemwa yananyamaziwa na watu wanaenda kwenye chaguzi, kana kwamba kuna siku vyama vya upinzani vitapata rais! kuoitia tume hii na system hii!



Ok, lets assume kila kitu kiko sawa Tanzania ndio nakuuliza sasa;

1. Je kwa nini Baregu?

2. Una matarijio gani ya chadema kushinda urais,( I mean strategy)

Ishu ya sasa ya Baregu , iwe handled kwa haki na yeye atafanyika daraja la wengi kupata haki, si kila anayenyimwa haki kama baregu akimbilie urais, kuna wengi wa design ya Baregu watakuja nchi hii na solution ni tupigane haki ipatikane.

However, kama chama watamtaka nani wa kuzuia??

Binafsi naungo mkono hoja hii, kuliko thread origin. Sababu kubwa ni kwamba mfumo uliopo sasa hivi siyo wa watu (watanzania), bali ni wa wachache ndani ya chama (CCM). Taasisi nyingi watoa maamuzi huteuliwa na Rais ambaye naye inapofika wakati wa uchaguzi husimama kama mgombea chini ya usimamizi wa wale wale aliowateua ama yeye au aliyetangulia wa chama chake (kwa mazingira ya sasa chini ya CCM). Hivyo, hata ikawa vipi wananchi tukawa na mapendekezo ya wagombea/mgombea atakayefaa kwa umma. Bado haitatosha kufikia adhima hiyo maana atapata misukosuko ya ujanja ujanja wa mfumo huu uliowekwa kwa manufaa ya kundi dogo.

Hivyo, basi ni hatua muhimu sasa hivi, kuanzia upinzani (vyama vya upinzani) hadi CCM wenyewe kama wana nia ya kupata viongozi wa kutumikia umma kwa moyo wote, basi tuandike Katiba mpya. Yenye kutoa mazingira bora kwa ustawi wa siasa na uchumi wa nchi kupitia michango ya watu waliojaliwa vipaji vya uongozi, na utaalamu wa kisayansi. Maana kwa sasa hivi wataalamu kutoka kada mbalimbali hawapewi fursa kuonyesha uwezo wao.

Maana uteuzi unafanyika kwa urafiki tu! Bila kuangalia tija ya mtu anayeteuliwa. Inakuwaje mawaziri ambao wanashirikia sekta nyeti kwa ustawi wa umma wateuliwe na mtu mmoja (Rais)? Ningependa binafsi uwaziri nao unagombewa na wananchi wawachague ili kupata watu walio makini. Hata hivyo, umma bado uko nyuma katika uelewa wa haki zao, na kiasi cha kuishia kuchagua wale wale vihio kwa kuhongwa chumvi na tisheti.

Labda Bunge lituchagulie mawaziri au iwepo tume huru kufanya kazi hii ya kuteua mawaziri husika na si rais! Hadi hapo mfumo huu dhaifu utakaporekebishwa, hakuna awe Baregu na wengine atakayeweza kupata nafasi ya kuingia kwenye utumishi wa ukuu wa nchi maana ni ngumu kimfomo. Tuandike Katiba mpya yenye maslahi kwa taifa kupitia kutoa mwanya wa ushiriki katika siasa na juhudi za kiuchumi wa watanzani wenye uwezo muhimu (potentials).
 
Prof Baregu angetufaa. Nadhani ccm isengeamin vile hali ingebadilika. Maana prof Baregu ni mpiganaji na mwanaharakat wa kwel. MUNGU AMSAIDIE NA ATUSAIDIE WATANZANIA FANYA MAAMUZ SAHIHI..
 
Kati ya wagombea wanaotajwa kweli sijaona mgombea mzoefu kama Prof. Lipumba. Kwanza yeye ni msomi amebobea kwenye mambo ya uchumi zaidi hadi alipata kuwa mshauri wa mambo ya uchumi wa Mseven Uganda naona kwa vile ameshiriki chaguzi tatu ana uzoefu ataleta changamoto nzuri katika uchaguzi ujao tumpe nafasi kupitia Chama cha wananchi CUF.
Nawasilisha........
 
kutaka baregu agombee uraisi wakati mnajua kamisa uchaguzi una mizengwe kwenye nafasi hio ni kupoteza kichwa cha maana sana kwenye jamii yetu.mimi nataka prof baregu agombee ubunge kwanza hili akaongeze joto.

wapinzani wanatakiwa waungane kwenye nafasi ya uraisi na nafasi za ubunge wanatakiwa kila jimbo ambalo wanaona chama fulani kina wafuasi wengi basi kiungwe mkono.muhimu hapa ni bunge kwanza kulitawala baada hapo urais utapatikana tu.


Hii ni sahihi kabisa bwana Arsene Wenger..
Sifa anazotajwa kuwa nazo prof Baregu,pia wengine km akina Prof lipumba,Marehemu Profesa Leonard Shayo,akina Dr Mvungi,walikuwa nazo wakati wakigombea 2005.lakini waliambulia patupu.Nafikiri ni vizuri Prof Baregu akaanzia chini,Japo ubunge km sio udiwani,alafu baadae ndo tuongelee maswala ya IKURU(kiburi, tafsiri ya kihaya)....
 
Ni wakati mwafaka kwako kugombea na kuchuana na watu wengine kama wakina Jk ana wengine kibao. Baregu anafaa kwa kila idara na pia ni mzuri katika kutoa maoni yake na yeye ndiye anaweza kutoa mawazo huru kabisa

Uwezo wa kufaa katika Idara na kuwa mzuri katika kutoa maoni na kuwa na mawazo huru hakumfanyi aweze kuwa Rais mzuri! Umewahi kumsikia Baregu kwenye discussion panels kwenye TV Dr. Rwaitama huwa anamshinda kwa hoja!!
 
1. Constitutional right
2. Academician cum politician who happens to know political, economic and social problems facing the country.. through various research, publications of his own. My support to Lipumba na Baregu is based on this facts. My dream is to go away with pure politician e.g. JK, Malecela, etc, within the presedential circle ..they normally prefer status quo!
3. Sijawahi kusikia kama ni materialistics yaani mtafutaji wa pesa nyingi..hivyo ni unlikely kuwa na kampuni ikulu..
4. International recognized figure, mpenda mageuzi alianzia enzi za NCCR mageuzi he is doing fine with chadema..
5....
6....

hili ni tatizo kubwa sana, kwa ajili hawa pure politicians hawajui na wala hawana mbinu za kutatua matatizo yetu, all they have done in their life is campaigning
 
JIANDAE KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU 2010

Mwaka 2010 ni mwaka wa uchaguzi. Ni mwaka ambao wananchi watafanya maamuzi baada ya kufanya tathmini juu ya ni kwa kiasi gani malengo na matarajio ya Watanzania yamefikiwa. Ni muda ambao Watanzania wataamua ni kwa kiwango gani wamefikia maisha bora kwa kila Mtanzania kama walivyoahidiwa na Chama tawala, Chama cha Mapinduzi, CCM.
CHADEMA tunawaomba Watanzania wajiweke tayari kufanya mabadaliko kwani tunaamini kuwa ahadi zilizotolewa ilikuwa dhana tu na kwamba mabadiliko ya kweli hayawezi kufanywa na viongozi walewale, wa chama kilekile, chenye uoza uleule, wakiendeleza yale yale, eti kwa Ari , Nguvu na Kasi mpya. Tanzania inahitaji mabadiliko ya mfumo yatakayozaa ukombozi wa fikra.
CHADEMA tunaamini katika Nguvu na Mamlaka ya Umma. Tunaamini kuwa mabadiliko ya kweli na Uhuru wa kweli haviwezi kufikiwa isipokuwa kwa kufanya mabadiliko ya mfumo na kuwa na uongozi thabiti , uongozi wenye maadili, kuwa na viongozi wanajali na kuheshimu matakwa ya binadamu wenzao. Viongozi wanaomuogopa Mungu ili kupambana na ufisadi na uoza unakaribia kuliangamiza taifa hili.
Matatizo ya taifa hili yanamgusa kila mzalendo mwenye uchungu na unyonge wake na unyonge wa jirani yake. Hivyo ni jukumu lako ewe mzalendo wa nchi hii kuanza kujiandaa kwa tukio adhimu kabisa, tukio la uchaguzi, tukio la kubadilisha uongozi na hatimaye mfumo wa nchi hii.
Ni wajibu wako ewe mzalendo mwenye wito wa uongozi kushiriki kwa kugombea. Ni wajibu wako ewe mzalendo mwenye kiu ya uongozi bora kuwashawishi wenye wito wa kuongoza wagombee. Ni wajibu wa kila mzalendo wa nchi hii kuanza maandalizi ya kufanya mabadiliko ya nchi hii kwa kuchangia kwa hali na mali.
Hakuna ufalme uliodumu milele isipokuwa wa Mungu pekee. CCM imepoteza uongozi imebaki na utawala. Ni wajibu wetu sasa kuipumzisha kwani uchovu wa chama tawala ni angamizo kwa watawaliwa.
Chukua hatua sasa, anza kujiandaa leo! Mabadiliko ni mchakato. Ni vema kama mzalendo uanze kujiandaa ili kwa pamoja tujenge taifa lenye matumaini. Taifa lenye TUMAINI JIPYA. Tembelea Tovuti ya Chadema
 
Hii ni sahihi kabisa bwana Arsene Wenger..
Sifa anazotajwa kuwa nazo prof Baregu,pia wengine km akina Prof lipumba,Marehemu Profesa Leonard Shayo,akina Dr Mvungi,walikuwa nazo wakati wakigombea 2005.lakini waliambulia patupu.Nafikiri ni vizuri Prof Baregu akaanzia chini,Japo ubunge km sio udiwani,alafu baadae ndo tuongelee maswala ya IKURU(kiburi, tafsiri ya kihaya)....

Ni wapi hasa chini unapodhani panafaa kuanzia? Uenyekiti wa shina/kijiji au? Kuna nafasi mbalimbali za kukijenga chama ili hatimaye kiweze kuchukua utawala wa nchi. Hii ndiyo hatua ambavyo vyama hivi vyote vinapitia. Chadema kabla ya Mbowe kugombea urais sio hii ya leo! Na sio kweli kuwa wakati mbowe anagombea hakufahamu kuwa nafasi ya kushinda ilikuwa finyu mno na kuwa angepoteza nafasi ya ubunge ambayo uhakika wa zaidi ya 80% ulikuwepo. Huku ndiko kujitoa muhanga kwa ajili ya wengine (kuukataa ubinafsi).

Kinachohitajika ni kuwaaminisha wananchi kuwa utawala bila ya ccm unawezekana na pia harakati zaidi kushinikiza mabadiliko ya miundo mbinu inayofanya hizi harakati zisiende mbele iweze kupata nguvu kutoka kwa umma na sio viongozi peke yao! Wengi wetu hatukotayari kushiriki katika hizi harakati, haswa wengi wetu tulioelimika, tunaishia tu kubonyeza keyboard na kusubiri mambo ya badilike, kwa vipi yatabadilika?

Wakati mwingine hatujiulizi hata maswali mepesi, chadema au cuf ikigomea uchaguzi wakati nld, tlp, nccr n.k wanashiriki inakuwa na maana gani?

Chadema kama chama cha siasa chenye nia ya kushika madaraka ya nchi na kikiwa katika harakati za kujijenga zaidi ni lazima kisimamishe mgombea wa urais, na sioni sababu yoyote inayoweza kumfanya Prof. Baregu kama anajisikia asichukue form kuomba kuchaguliwa na chama chake.
 
Waberoya
Ni sawa kabisa unavyosema kwanza tupiganie katiba halafu ndipo tuwaze uchaguzi, ni kitu kinachowezekana lakini si kwamba hilo litatokea leo au kesho it takes time na elewa kwamba kubadili katiba ni mapambano kati ya watawala na watawaliwa, watawala au walio madarakani wataona ni njia ya kunyang'anywa walicho nacho kwa hiyo watafanya kila mbinu ili kuchelewesha mabadiliko na ujue wakati wanachelewesha si kwamba chaguzi zitasimama wao watakuwa wanaweka mgombea wao hata kama vyama vingine vitasusa kwa kila chaguzi. Kwa hiyo wakati vyama vya upinzani vikiweka mikakati ya kubadili katiba ni bora vikajiandaa na chaguzi zilizopo.

Kuhusu Tume huru ya uchaguzi ni kweli si huru na tunajua itakuwa biased kwa vile inateuliwa na rais itapendelea aliye iteua lakini hiyo vile vile isivikatishe tamaa vyama vya upinzani kutojiandaa na uchaguzi.

Umesema kwa nini prof. Baregu hilo ni pendekezo langu tu Mkuu nimemuona Baregu anasifa zote za kuwa mgombea kama Mbowe ataamua kutogombea lakini haizuii kama kuna mtu unayemuona anafaa zaidi kumpendekeza hata hivyo nimesema prof Baregu akuchukue fomu aingie kwenye kura za maoni ndani ya chama chake hivyo anaweza kupambanishwa na wana Chadema wengine anaweza ateuliwe au asiteuliwe. Hilo la matarajio ya Chadema kushinda nitajibu baadaye.

Kwanza Rais wa Tanzania anatakiwa kufahamu kwa undani kiini cha kuwa nyuma kimaendeleo na jinsi ya kujikwamua. President Obama ni profesa, Bill Clinton ni prosefa, Hillary Clinton ni profesa, Condelleza Rice ni profesa, wote hao wamarekani walikuwa wanajua nini America inahitaji, pia Profesa Baregu nae pia anajua Tanzania inahitaji nini ili kujikwamua, sio kama maprofesa wengine wanafuata ulaji binafsi, hapa Profesa Baregu anasema:

Cheki link ya Globalisation and africas challenges video clip part 1 na 2
Huyu mwanazuoni anaelewa matatizo ya Africa ikiwemo Tanzania, nini kifanyike ktk dunia ya sasa endelea:

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=bRiC1poArkM[/ame] Globalisation and africas challenges (part 2-2) na (part 1-1)
default.jpg
 
..akagombee ubunge tumpime jinsi anavyopambana akiwa bungeni.

NB:

..kwa mtizamo wangu napenda CCM wasiwe na majority bungeni. hiyo itapelekea Waziri Mkuu na serikali kuundwa na chama kingine other than CCM.
 
siasa zimemlostisha sana lipumba. yaani na uprofesa wake amepauka utadhani ...............

mwenzie sefu anaejea kundini kidogokidogo, kabla ya october mtamshuhudia akilamba kadi ya kijani!!!! mjini hapa!!!!!!!!!!!!!

mshaurini arudi kundini mambo yamnyookee uwaziri wa fdha na uchumi kwa huyu prof mbona uko waziwazi ?????????????
 
Baregu is much much better for President than any of those who may be offered by chama cha mafisadi.

Baregu is a clean man, without any blemishes of corruption and his Party Chadema has a clear mission to serve the interests of Wananchi.

He is not a rabid socialist and if his Party nominates him, and genuine patriots like Willibroad Slaa, Freeman Mbowe, Edwin Mtei, Tindu Lissu and John Mnyika back him and campaign for him, other Tanzanian patriots will join them and hopefully rescue our country further deterioration.

Baregu for President!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Baregu is much much better for President than any of those who may be offered by chama cha mafisadi.

Baregu is a clean man, without any blemishes of corruption and his Party Chadema has a clear mission to serve the interests of Wananchi.

He is not a rabid socialist and if his Party nominates him, and genuine patriots like Willibroad Slaa, Freeman Mbowe, Edwin Mtei, Tindu Lissu and John Mnyika back him and campaign for him, other Tanzanian patriots will join them and hopefully rescue our country further deterioration.

Baregu for President!!!!!!!!!!!!!!!!


.........and Zitto Kabwe............
 
Kati ya wagombea wanaotajwa kweli sijaona mgombea mzoefu kama Prof. Lipumba. Kwanza yeye ni msomi amebobea kwenye mambo ya uchumi zaidi hadi alipata kuwa mshauri wa mambo ya uchumi wa Mseven Uganda naona kwa vile ameshiriki chaguzi tatu ana uzoefu ataleta changamoto nzuri katika uchaguzi ujao tumpe nafasi kupitia Chama cha wananchi CUF.
Nawasilisha........

Hatuhitaji Mgombea Mzoefu tunahitaji Mtu mwenye uwezo wa Kushindana na si Kuongeza Uzoefu katika Kugombea
 
Natazma taarifa ya habari TBC daaaah Shibuda anatangaza live kuwa anamvaa JK kugombea u rais..haya yetu macho
 
Shibuda ngonjera, mashari na mipasho ndio vinamfaa! Hawezi kuwa kiongozi wa nchi inayohitaji mapinduzi ya kiuchumi! Dr Pombe, Dr Slaa ndio aina ya viongozi wanatakiwa Tanzania!
 
Back
Top Bottom