Sheria ya rushwa ina tofauti na sheria nyingine?

Hekima Ufunuo

JF-Expert Member
May 28, 2009
220
11
Wana JF, ndani ya wiki hii kumekuwa na taarifa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu watu fulani fulani "kukamatwa" siyo kutuhumiwa. Kukamatwa kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa. leo ikatoka taarifa kuwa watu hao wanaruhusiwa kuendelea na kampeni za ndani ya chama wakati UCHUNGUZI unaendelea na ikithibitika hata kama wameshinda kura za maoni basi wataenguliwa.

Swali.
1. Sheria ya rushwa ni tofauti na nyingine za makosa ya jinai?
2. Kama jibu ni SIYO, mbona wezi wa kuku wakikamatwa wanakaa rumande mpaka upelelezi ukamilike?
3 Si wakubwa wetu waliotuambia kuwa sheria inasainiwa kwa mbwembwe ili iwamalize kabisa watoaji na wapokeaji wa rushwa ya uchaguzi? sasa mbona kinyume chake?
4. Ule umakini ulioonyeshwa na JK kwenye kuisaini sheria hiyo mbona haupo kwenye utekelezaji wake?
5.Kule Moshi yule aliyekamatwa kwa vitendo vya rushwa amekuwa wa kwanza, je akishapewa ubunge wa kuteuliwa ndipo takukuru watakapompeleka mahakamani?
6. Hivi takukuru wakimkamata mtu na ushahidi, watamhifadhi wapi? polisi au wana sehemu yao ya kumhifadhi? Kama ni Polisi mbona kwenye kwenda kukamata hawawashirikishi polisi?

Sioni dalili yoyote ya rushwa kuthibitiwa na hawa takukuru, kama kwenye kura za maoni usanii ni wa kiwango hiki, vipi itakapofikia fainali yenyewe?

Wana JF naomba mnisaidie, maswali haya yananipa kizungumkuti. Naomba tutafakari?

Rspe
 
Back
Top Bottom