Sheria ya kutokumshitaki Rais ndio Rushwa kubwa kuliko

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
SHERIA YA KUTOKUSHTAKIWA RAIS NDIO RUSHWA KUBWA KULIKO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Takukuru kazi yenu bado itakuwa ngumu ikiwa kuna sheria ambazo zinatoka Rushwa Kwa baadhi ya makundi ya Watu hasahasa viongozi.

Kuna Sheria na kuna Haki. Alafu kuna vyombo vya kusimamia sheria na Haki. Alafu muda huohuo kuna maadui wa Haki, Rushwa ikiwa mmoja wao.

Moja ya Sheria Mbaya zaidi kuliko, sheria yenye kutoa Rushwa, ni Ile inayosema Rais asishtakiwe. Hakuna Rushwa kubwa kama hiyo..

Hatuwezi sema Nchi inaongozwa Kwa Haki ilhali kuna sheria zinazonyima Haki ya usawa Mbele za sheria. Watu wote wapo Sawa Mbele ya sheria ingawaje haimaanishi kuwa wanalingana. Same but not similar.

Rais hawezi sema yeye ni MTU wa Haki au anapenda Haki huku akijua kuwa kuna Sheria zimempa Rushwa ya kutotendewa Haki kama wengine pale anapokosea.

Rais mpenda Haki lazima arekebishe hicho kipengele cha sheria zilizoadui na Haki kama hiyo ya kumkingia kifua asishtakiwe.

Sheria hiyo ndio msingi Mkuu wa Ufisadi, ukandamizaji, udikteta, ubabe usio na kichwa wala miguu.

Wanasheria, wapenda Haki na watu wote waungwana wanaowajibu wa kuifuta hiyo sheria Kwa gharama yoyote Ile.

Mahakama na Bunge, na vyombo vingine vya serikali vitakuwa katika hatari ya kufanya Ufisadi na Rushwa kupitia sheria hizi za Rushwa.

Mahakama haiwezi kutenda HAKI ikiwa kuna Watu ndani ya taifa hawashtakiwi. Itatenda Haki kulingana na utashi wa viongozi na sio kulingana na sheria za Haki zisemavyo.

Nilimsikia, Bw. Rostam akizungumzia kuhusu Mahakama kupokea maelekezo Kutoka juu Hali inayopingisha Haki. Hilo wala halihitaji ushahidi zaidi ya ule ushahidi wa sheria ya ajabu na ya Rushwa inayonyima Haki Kwa Rais na sasa baadhi ya watendaji wa serikali kushtakiwa.

Mahakama na vyombo vyote vya Haki na sheria haviwezi kukataa tuhuma hiyo Wakati sheria ya Rushwa ya kutoshtaki Rais na Baadhi ya watendaji wa serikali ingalipo. Uwepo wa sheria hiyo inathibitisha tuhuma hiyo ni kweli na wala sio tuhuma.

Fikiria Polisi au vyombo vya usalama ambavyo vitaweza kuvunja sheria Kwa ukaidi, ujeuri na Kiburi kwa kile wakiitacho kupewa maelekezo Kutoka juu. Juu walipo wasioshtakiwa, ambao Kwa tafsiri nyepesi wenye ruhusa ya kuvunja sheria ambazo waliapa kuzitii na kuzitumikia. Jambo la aibu ndani ya jamii yetu.

Sheria ya Rushwa(sheria ambazo ni adui WA Haki) kama ya kutoshtakiwa Rais, ndio unaleta lile genge la wahuni lisemalo; unanijua Mimi ni Nani?" Genge hilo kupitia sheria hiyo haliwezi kufanywa chochote.

Hata Huko Mahakamani kuwe na Mahakimu na majaji wenye weledi na uadilifu lakini hawawezi kufurukuta na watakuwa vibaraka wa wale wasioshtakiwa tuu. Watake wasitake.

Rais akishakuwa automatically tutaondoa vibaraka na Machawa ambao wanafanya hivyo ili kujikinga na hatari za kijinai zitakazojitokeza, watatumia kete Yao muhimu ya MTU asiyeshtakiwa kuishinikiza Mahakama au vyombo vya Dola.

Sheria hiyo inamshawishi Rais na viongozi wake kufanya Ufisadi Kwa sababu wanajua hawatafanywa chochote. Sio ajabu kupitia sheria hiyohiyo viongozi Baada ya kuingia madarakani tuu miaka Mitano ni mingi unawakuta wakiogelea katika bahari ya ubilionea ambao moja Kwa moja ni Ufisadi unaotokana na sheria za Rushwa zinazoiminya Haki.

Sheria hiyo inaminya Haki zingine kama Uhuru wa vyombo vya habari na Uhuru WA kutoa Maoni. Vyombo vya habari huchagua habari za kurusha Kwa kuhofia kukutana na fagio la chuma la Fisadi, Kwa sababu Rais asiyeshtakiwa anauwezo wa kukifungia chombo cha habari na ikiwezekana kuwatia matatani Wahusika hata kama Hawana kosa.

Sheria hiyo ni Mbaya wala hakuna Lugha nzuri ya kuielezea. Ukiita ni sheria ya hovyo hautakuwa umekosea. Ni yahovyo kwa sababu ni adui wa Haki. Na MTU ambaye ni adui WA Haki ni MTU wa hovyo.

Logically, MTU anayeshtakiwa hawezi kumfanya lolote MTU ambaye hashtakiwi. Kumaanisha anayeshtakiwa atakuwa kibaraka au mtumwa wa asiyeshtakiwa.

Sheria ya Rais hashtakiwi ni sheria inayounda magenge ya wahalifu ambao hawaguswi wala kugusika kisheria. Ni kutengeneza na kuwekea mazingira familia Fulani ambazo zitabahatika kushika ngazi ya Urais kutogusika.

Sheria hiyo pia inajenga Utumwa Kwa Rais Mpya atakayeingia madarakani kwani hatafanya kazi Kwa Haki hata iweje labda aifute hiyo sheria. Rais anayeingia madarakani tayari anaandaliwa kuwa Fisadi na MLA Rushwa. Atakuta madudu ya mwenzake (Ma/ Rais w/aliopita) na marafiki zake, atashindwa kuwashughulikia Kwa sababu tayari kuna sheria inayowalinda, na endapo atathubutu kushughulikia angalau hata marafiki wa Rais aliyepita basi automatically atakutana na anguko ambalo hatanyanyuka Kamwe.

Sheria hii inafanya shirika la Usalama wa taifa kuwa shirika la usalama la Watu binafsi ambao wameshakuwa viongozi wa nchi. Hii inawapa tabu Vijana wa Usalama kutofanya kazi Yao Kwa ufanisi kwani badala ya kuitumikia nchi watakuwa wanatumikia Mabwana zao. Automatically huwezi kuwa na Uzalendo kwenye taifa ambalo Rais hashtakiwi. Hakunaga kitu kama hicho.

Utakuwa mzalendo labda ukiwa pekeako Huko kwenye familia yako lakini ukishakuja kitaifa huku utasombaa na mfumo wa Rushwa na kifisadi. Na endapo utaleta fyokofyoko basi utajikuta kwenye matata Makubwa.

Wanasema Haki haipotei lakini kimsingi Haki inapotea ikiwa waendesha nchi watakuwa wanaongozwa na sheria za Rushwa. Mara ngapi umesikia Watu kadhaa wakinyimwa Haki zao iwe za kisiasa, kijamii au kiuchumi, nini kilitokea?

Haki inapotea ikiwa jamii itakubali kuongozwa na viongozi wala Rushwa au wanaopewa Rushwa na sheria za hovyo.

Nilisikia habari za Bandari, viongozi wanalalamika kuwa Hakuna utendaji mzuri wenye ufanisi ndani ya Bandari. Wakaenda mbali zaidi wakasema, pale bandarini mbali na Teknolojia kuwa ndogo lakini changamoto kubwa ni Rasilimali Watu kuwa majizi, mafisadi na wala Rushwa hali inayozorotesha ufanisi wa Bandari.

Lakini lazima tujiulize, kwani hakuna sheria za kudili na watu wanaohujumu ufanisi wa Bandari? Jibu ni zipo sheria lukuki na zenye adhabu stahiki. Lakini tatizo kubwa ni lilelile, huwezi muadhibu au sheria haiwezi kufanya kazi Kwa Watu ambao wamejikinga na mwamvuli wa viongozi wasioshtakiwa.

Hivi utawezaje kumshtaki MTU ambaye unajua anaurafiki na Rais au kiongozi asiyeshtakiwa. Hata Hakimu au Jaji utamtia majaribuni. Ni ngumu Mno.

Mara ngapi umesikia wafanyabiashara au matajiri wakijiunga na vyama vya Siasa Kwa kufuata mkumbo ilimradi kujiwekea Usalama wa biashara zao. Huoni tatizo hapo? Huoni Rushwa hapo?

Nchi haiwezi kuendelea hata siku moja ikiwa sheria zake hajalenga kutoa Haki. Ni sheria zilizolenga kutoa Rushwa ambayo ni adui WA Haki.

Niliona juzi TBC ikimuonyesha Mkurugenzi wa Shirika Hilo(TBC) Dkt Ayoub Rioba akiwa visiwani Zanzibar katika mchakato WA kuchukua Maoni ya wananchi katika tume ya kufanya maboresho ya utoaji wa haki Mahakamani na vyombo kama polisi na upelelezi(kama sijakosea). Ni hatua nzuri. Lakini itakuwa ni kazi Bure na upotezaji wa Pesa ikiwa mzizi Mkuu wa Haki hautaanzia juu kabisa walipo viongozi.

Sio kwamba Watu hawawezi tenda Haki Mahakamani, sio kwamba polisi hawawezi kufanya kazi Kwa ufanisi. Tatizo linaanzia juu kushuka Chini. Juu pakiwa Safi moja Kwa moja Chini kutakuwa Safi.

Ikiwa kuna sheria inamtetea Rais au kiongozi asishtakiwe hapo tafsiri yake hata baadhi ya watendaji wake hawatashtakiwa hata wakivunja Haki Kwa sababu wengi watapokea maelekezo Kutoka juu. Pia Boss lazima atetee watumishi Wake kama watumishi watakavyomtetea kwenye nyakati ngumu.

Pendekezo kuu Kutoka Kwa Taikon Master ni kuzichunguza sheria za Rushwa ikiwemo Hii ya kutoshtakiwa Kwa Rais na Baadhi ya viongozi, zifutwe. Kisha Watu wote wawe chini ya sheria. Alafu muone kama Maendeleo hayatakuja.

Muone kama kuna Panya buku atakayeiba Pesa za Umma.

Taikon Acha nipumzike sasa. Leo sitaki maswali.
Jumapili njema.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Uko sahihi kabisa huwezi kuwa na taifa lenye kubagua kwamba huyu ana haki zaidi ya mwingine wakati wote ni binadamu na wanaweza kutenda makosa muda wowote kwa kutokujua/kujua huku ni kutengeneza miungu watu wasiogusika na magenge yao. Ili taifa lipige hatua hatuna budi kuondoa Sheria kama hizo kwanza kinga ya nini kama nia ni nzuri mara spika nae ana kinga matokeo yake ufisadi umetamalaki kila kona
 
Ni kweli Kabisa
 
Ni rahisi sana kuibadilisha, hawa watawala huwa hawafikirii sana mambo hubadirika haraka sana, hawa hawa Wabunge wanaotetea uporwaji wa bandari na ardhi yetu kesho ndiyo watakao pitisha kwa 100% kubadilishwa kwa sheria ya kushitakiwa kwa raisi aliyehusika, wanajishahau sana watawala wanafikiri wataishi milele na power pia wanasahau wanafamilia zao hapa pia people will get back at them siku moja, hakuna jipya Duniani tumeona yakitokea Dunia nzima …
 
SHERIA YA KUTOKUSHTAKIWA RAIS NDIO RUSHWA KUBWA KULIKO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Takukuru kazi yenu bado itakuwa ngumu ikiwa kuna sheria ambazo zinatoka Rushwa Kwa baadhi ya makundi ya Watu hasahasa viongozi.
Kuna Sheria na kuna Haki. Alafu kuna vyombo vya kusimamia sheria na Haki. Alafu muda huohuo kuna maadui wa Haki, Rushwa ikiwa mmoja wao.

Moja ya Sheria Mbaya zaidi kuliko, sheria yenye kutoa Rushwa, ni Ile inayosema Rais asishtakiwe. Hakuna Rushwa kubwa kama hiyo..

Hatuwezi sema Nchi inaongozwa Kwa Haki ilhali kuna sheria zinazonyima Haki ya usawa Mbele za sheria. Watu wote wapo Sawa Mbele ya sheria ingawaje haimaanishi kuwa wanalingana. Same but not similar.

Rais hawezi sema yeye ni MTU wa Haki au anapenda Haki huku akijua kuwa kuna Sheria zimempa Rushwa ya kutotendewa Haki kama wengine pale anapokosea.

Rais mpenda Haki lazima arekebishe hicho kipengele cha sheria zilizoadui na Haki kama hiyo ya kumkingia kifua asishtakiwe.

Sheria hiyo ndio msingi Mkuu wa Ufisadi, ukandamizaji, udikteta, ubabe usio na kichwa wala miguu.

Wanasheria, wapenda Haki na watu wote waungwana wanaowajibu wa kuifuta hiyo sheria Kwa gharama yoyote Ile.

Mahakama na Bunge, na vyombo vingine vya serikali vitakuwa katika hatari ya kufanya Ufisadi na Rushwa kupitia sheria hizi za Rushwa.

Mahakama haiwezi kutenda HAKI ikiwa kuna Watu ndani ya taifa hawashtakiwi. Itatenda Haki kulingana na utashi wa viongozi na sio kulingana na sheria za Haki zisemavyo.

Nilimsikia, Bw. Rostam akizungumzia kuhusu Mahakama kupokea maelekezo Kutoka juu Hali inayopingisha Haki. Hilo wala halihitaji ushahidi zaidi ya ule ushahidi wa sheria ya ajabu na ya Rushwa inayonyima Haki Kwa Rais na sasa baadhi ya watendaji wa serikali kushtakiwa.

Mahakama na vyombo vyote vya Haki na sheria haviwezi kukataa tuhuma hiyo Wakati sheria ya Rushwa ya kutoshtaki Rais na Baadhi ya watendaji wa serikali ingalipo. Uwepo wa sheria hiyo inathibitisha tuhuma hiyo ni kweli na wala sio tuhuma.

Fikiria Polisi au vyombo vya usalama ambavyo vitaweza kuvunja sheria Kwa ukaidi, ujeuri na Kiburi kwa kile wakiitacho kupewa maelekezo Kutoka juu. Juu walipo wasioshtakiwa, ambao Kwa tafsiri nyepesi wenye ruhusa ya kuvunja sheria ambazo waliapa kuzitii na kuzitumikia. Jambo la aibu ndani ya jamii yetu.

Sheria ya Rushwa(sheria ambazo ni adui WA Haki) kama ya kutoshtakiwa Rais, ndio unaleta lile genge la wahuni lisemalo; unanijua Mimi ni Nani?" Genge hilo kupitia sheria hiyo haliwezi kufanywa chochote.

Hata Huko Mahakamani kuwe na Mahakimu na majaji wenye weledi na uadilifu lakini hawawezi kufurukuta na watakuwa vibaraka wa wale wasioshtakiwa tuu. Watake wasitake.

Rais akishakuwa automatically tutaondoa vibaraka na Machawa ambao wanafanya hivyo ili kujikinga na hatari za kijinai zitakazojitokeza, watatumia kete Yao muhimu ya MTU asiyeshtakiwa kuishinikiza Mahakama au vyombo vya Dola.

Sheria hiyo inamshawishi Rais na viongozi wake kufanya Ufisadi Kwa sababu wanajua hawatafanywa chochote. Sio ajabu kupitia sheria hiyohiyo viongozi Baada ya kuingia madarakani tuu miaka Mitano ni mingi unawakuta wakiogelea katika bahari ya ubilionea ambao moja Kwa moja ni Ufisadi unaotokana na sheria za Rushwa zinazoiminya Haki.

Sheria hiyo inaminya Haki zingine kama Uhuru wa vyombo vya habari na Uhuru WA kutoa Maoni. Vyombo vya habari huchagua habari za kurusha Kwa kuhofia kukutana na fagio la chuma la Fisadi, Kwa sababu Rais asiyeshtakiwa anauwezo wa kukifungia chombo cha habari na ikiwezekana kuwatia matatani Wahusika hata kama Hawana kosa.

Sheria hiyo ni Mbaya wala hakuna Lugha nzuri ya kuielezea. Ukiita ni sheria ya hovyo hautakuwa umekosea. Ni yahovyo Kwa sababu ni adui WA Haki. Na MTU ambaye ni adui WA Haki ni MTU wa hovyo.

Logically, MTU anayeshtakiwa hawezi kumfanya lolote MTU ambaye hashtakiwi. Kumaanisha anayeshtakiwa atakuwa kibaraka au mtumwa wa asiyeshtakiwa.

Sheria ya Rais hashtakiwi ni sheria inayounda magenge ya wahalifu ambao hawaguswi wala kugusika kisheria. Ni kutengeneza na kuwekea mazingira familia Fulani ambazo zitabahatika kushika ngazi ya Urais kutogusika.

Sheria hiyo pia inajenga Utumwa Kwa Rais Mpya atakayeingia madarakani kwani hatafanya kazi Kwa Haki hata iweje labda aifute hiyo sheria. Rais anayeingia madarakani tayari anaandaliwa kuwa Fisadi na MLA Rushwa. Atakuta madudu ya mwenzake (Ma/ Rais w/aliopita) na marafiki zake, atashindwa kuwashughulikia Kwa sababu tayari kuna sheria inayowalinda, na endapo atathubutu kushughulikia angalau hata marafiki wa Rais aliyepita basi automatically atakutana na anguko ambalo hatanyanyuka Kamwe.

Sheria hii inafanya shirika la Usalama wa taifa kuwa shirika la usalama la Watu binafsi ambao wameshakuwa viongozi wa nchi. Hii inawapa tabu Vijana wa Usalama kutofanya kazi Yao Kwa ufanisi kwani badala ya kuitumikia nchi watakuwa wanatumikia Mabwana zao. Automatically huwezi kuwa na Uzalendo kwenye taifa ambalo Rais hashtakiwi. Hakunaga kitu kama hicho.
Utakuwa mzalendo labda ukiwa pekeako Huko kwenye familia yako lakini ukishakuja kitaifa huku utasombaa na mfumo wa Rushwa na kifisadi. Na endapo utaleta fyokofyoko basi utajikuta kwenye matata Makubwa.

Wanasema Haki haipotei lakini kimsingi Haki inapotea ikiwa waendesha nchi watakuwa wanaongozwa na sheria za Rushwa. Mara ngapi umesikia Watu kadhaa wakinyimwa Haki zao iwe za kisiasa, kijamii au kiuchumi, nini kilitokea?

Haki inapotea ikiwa jamii itakubali kuongozwa na viongozi wala Rushwa au wanaopewa Rushwa na sheria za hovyo.

Nilisikia habari za Bandari, viongozi wanalalamika kuwa Hakuna utendaji mzuri wenye ufanisi ndani ya Bandari. Wakaenda mbali zaidi wakasema, pale bandarini mbali na Teknolojia kuwa ndogo lakini changamoto kubwa ni Rasilimali Watu kuwa majizi, mafisadi na wala Rushwa hali inayozorotesha ufanisi wa Bandari.

Lakini lazima tujiulize, kwani hakuna sheria za kudili na watu wanaohujumu ufanisi wa Bandari? Jibu ni zipo sheria lukuki na zenye adhabu stahiki. Lakini tatizo kubwa ni lilelile, huwezi muadhibu au sheria haiwezi kufanya kazi Kwa Watu ambao wamejikinga na mwamvuli wa viongozi wasioshtakiwa.

Hivi utawezaje kumshtaki MTU ambaye unajua anaurafiki na Rais au kiongozi asiyeshtakiwa. Hata Hakimu au Jaji utamtia majaribuni. Ni ngumu Mno.

Mara ngapi umesikia wafanyabiashara au matajiri wakijiunga na vyama vya Siasa Kwa kufuata mkumbo ilimradi kujiwekea Usalama wa biashara zao. Huoni tatizo hapo? Huoni Rushwa hapo?

Nchi haiwezi kuendelea hata siku moja ikiwa sheria zake hajalenga kutoa Haki. Ni sheria zilizolenga kutoa Rushwa ambayo ni adui WA Haki.

Niliona juzi TBC ikimuonyesha Mkurugenzi wa Shirika Hilo(TBC) Dkt Ayoub Rioba akiwa visiwani Zanzibar katika mchakato WA kuchukua Maoni ya wananchi katika tume ya kufanya maboresho ya utoaji wa haki Mahakamani na vyombo kama polisi na upelelezi(kama sijakosea). Ni hatua nzuri. Lakini itakuwa ni kazi Bure na upotezaji wa Pesa ikiwa mzizi Mkuu wa Haki hautaanzia juu kabisa walipo viongozi.

Sio kwamba Watu hawawezi tenda Haki Mahakamani, sio kwamba polisi hawawezi kufanya kazi Kwa ufanisi. Tatizo linaanzia juu kushuka Chini. Juu pakiwa Safi moja Kwa moja Chini kutakuwa Safi.

Ikiwa kuna sheria inamtetea Rais au kiongozi asishtakiwe hapo tafsiri yake hata baadhi ya watendaji wake hawatashtakiwa hata wakivunja Haki Kwa sababu wengi watapokea maelekezo Kutoka juu. Pia Boss lazima atetee watumishi Wake kama watumishi watakavyomtetea kwenye nyakati ngumu.

Pendekezo kuu Kutoka Kwa Taikon Master ni kuzichunguza sheria za Rushwa ikiwemo Hii ya kutoshtakiwa Kwa Rais na Baadhi ya viongozi, zifutwe. Kisha Watu wote wawe chini ya sheria. Alafu muone kama Maendeleo hayatakuja.

Muone kama kuna Panya buku atakayeiba Pesa za Umma.

Taikon Acha nipumzike sasa. Leo sitaki maswali.
Jumapili njema.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kwneye mikutano yenu ya ndani huwa unayasema haya?

Ccm mnalia lia nini? Tulieni mnyolewe
 
Ni rahisi sana kuibadilisha, hawa watawala huwa hawafikirii sana mambo hubadirika haraka sana, hawa hawa Wabunge wanaotetea uporwaji wa bandari yetu kesho ndiyo watakao pitisha kwa 100% kubadilishwa kwa sheria ya kushitakiwa kwa raisi aliyehusika, wanajishahau sana watawala wanafikiri wataishi milele na power pia wanasahau wanafamilia zao hapa pia people will get back at them siku moja …
Kama Lowasa alivyojisahau hakuwa fikiria atakuwa mpinzani. Akanyoshwa sana.
 
Uchama sio mzuri.
Napenda nikijadili Jambo nijadili mada husika bila kuingiza uchama, udini au ukabila.
Ila sitazuia wanaopenda tofauti na Mimi.
Sasa chama chako ndio wanaopitisha yoote haya. Unatenga vipi jambo hili na chama? Hauko serioua au unakuja kupumzikia watu hapa
 
Ni rahisi sana kuibadilisha, hawa watawala huwa hawafikirii sana mambo hubadirika haraka sana, hawa hawa Wabunge wanaotetea uporwaji wa bandari na ardhi yetu kesho ndiyo watakao pitisha kwa 100% kubadilishwa kwa sheria ya kushitakiwa kwa raisi aliyehusika, wanajishahau sana watawala wanafikiri wataishi milele na power pia wanasahau wanafamilia zao hapa pia people will get back at them siku moja, hakuna jipya Duniani tumeona yakitokea Dunia nzima …

Wala hawajisahau. Wamegeuzwa vibaraka, wapambe, na Machawa. Huwezi kwenda kinyume na asiyeshtakiwa ilhali wewe unashtakiwa alafu ni Boss wako.
Sio wa kulaumu
 
Sasa chama chako ndio wanaopitisha yoote haya. Unatenga vipi jambo hili na chama? Hauko serioua au unakuja kupumzikia watu hapa

Kwa nini unataka niwe na chama? Naona unanilazimishia Mkuu.
Hao CCM kama ndio waliotunga sheria hiyo ya hovyo iweje ninyi msioccm mkubali kuongozwa na watu hao?

Msidhani kwenye nchi Hii kila MTU anavyama kama ninyi.
Ninyi cCM na chadema mnaile kasumba Mbaya ya kudhani ninyi mnahaki ya Watu kuwa kama ninyi Jambo ambalo sio HAKI.

Ni Sawa na hawa wenye Dini za Ukristo na uislam. Yaani mnadhani kila mtanzania anahizo mambo. Hapo ndio mnakwama.

Ooh! Huyo Rais Muislam, ooh huyo Mkristo yaani kama machizi hivi.
 
Kwenye maandika yako umekuwa uki- declare hivyo kuwa wewe ni Mwanachama wa ccm na hivyo unatoa maoni yako kukishauri chama chako. Mara kadhaa.
Leo unakikana?
 
Wala hawajisahau. Wamegeuzwa vibaraka, wapambe, na Machawa. Huwezi kwenda kinyume na asiyeshtakiwa ilhali wewe unashtakiwa alafu ni Boss wako.
Sio wa kulaumu

Kama bosi wako hashitakiwi Tanzania hata wao hawashitakiwi pia kwani Tanzania Mahakama na Bunge siyo huru …
 
Kwenye maandika yako umekuwa uki- declare hivyo kuwa wewe ni Mwanachama wa ccm na hivyo unatoa maoni yako kukishauri chama chako. Mara kadhaa.
Leo unakikana?

😂😂😂

Umeamua kusema hivyo, Sawa.
Mimi ni Mtibeli.
CCM, chadema na Ndugu zao wote ni Watoto wangu.
Ukristo na uislam na Ndugu zao ni Watoto wangu.
 
Back
Top Bottom