sheria ya kugonga gari kwa nyuma

Kireka1980

JF-Expert Member
Mar 18, 2008
302
43
wadau kuna siku nilikuwa kwenye gari ndogo barabara ya Shekilango, kuna dala dala lilikuwa mbele yetu (Ubungo - msasani) Ghafla lilisimama katikati ya barabara na brake light hazifanyi kazi, ujanja hatukuwa nao tukaligonga kwa nyuma na sisi ndio tulioonekana na kosa. Hii ilinifanya kila mara niseme Ditopile alikuwa sahihi kumpiga risasi dereva wa daladala.
Wadau madereva wa daladala wanakera sana na ukiwa na hasira ..........
 
Ni kweli daladala wanakera kupita kiasi lakini sheria za barabarani ziko wazi ukisha mgonga mtu kwa nyuma wewe ndiwe mwenye makosa. Tatizo letu hatuzifuati sheria za barabarani kama ipasavyo ingawaje tunawalaumu madereva wa daladala. Unapashwa kuacha mita zisizopungua kumi kati yako na gari la mbele ili ikitokea mwenzako akafunga break ghafula, then inakupa nafasi na wewe kujitetea.

Lakini kama hiyo daladala taa za break zilikuwa haziwaki mlikuwa na utetezi mzuri. Je mlimsubiri trafik police kuja kupima hiyo ajali na kuyakagua magari yenu au mlikubali yaishe kishikaji?
 
Kwa foleni za dar mara chache sana watu huachiana meter 10. tunasogeleana mita hata 2 hazifiki kwa kuogopa mtu kuchomeka mbele yako kama ukiacha nafasi kubwa. lakini mkiwa speed ni vyema kuacha distance ya mita 10 kama inavyoshauriwa kuepusha mabalaa kama hayo ya ajali zinazoepukika.
 
...ndio sheria mkuu, sheria zimewekwa ili zifuatwe, sio zivunjwe. Matokeo yake ndio kama hayo, mkiwaiga wenye dala dala wote mnaonekana ni madereva wabovu!
At all times maintain a two-second gap from the vehicle ahead, no matter what speed you are travelling. When it is raining, a foggy night, or any combination of these, the gap should be doubled to four seconds.
 
Kaka kugonga kwa nyuma ni kosa iwe dala dala kasimama ghafla au break light hazifanyi kazi,,kosa ni lenu na ndivyo sheria ilivyo.
 
wadau kuna siku nilikuwa kwenye gari ndogo barabara ya Shekilango, kuna dala dala lilikuwa mbele yetu (Ubungo - msasani) Ghafla lilisimama katikati ya barabara na brake light hazifanyi kazi, ujanja hatukuwa nao tukaligonga kwa nyuma na sisi ndio tulioonekana na kosa. Hii ilinifanya kila mara niseme Ditopile alikuwa sahihi kumpiga risasi dereva wa daladala.
Wadau madereva wa daladala wanakera sana na ukiwa na hasira ..........

Ukigonga gari kwa nyuma hilo ni kosa lako, hata kama daladala lile lilisamama ghafla. Gari la mbele yako linaweza kusimama ghafla kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuharibika ghafla, na hiyo haikuruhusu wewe kuligonga.

Mojawapo katika mambo uliyotakiwa kuwa umejifunza kabla ya kupewa leseni ya kuendesha gari ni mbinu za defensive driving. Mojawapo ya mbinu hizo ni kuhakikisha kuwa unaacha umbali wa kutosha kati yako na gari la mbele yako kiasi kuwa uweze kusimama bili kuligonga iwapo litapata breakdowan yoyote ya ghafla
 
Kwa kuongezea katika defensive driving, unatakiwa wakati wote una angalia mwenendo wa gari lililo mbele yako kwani hilo ndiyo litakalo kufanya wewe ujue uendesheje gari lako.
Kwa kusisitiza, kitendo cha kuingia kwa nyuma ni makosa.
 
wadau kuna siku nilikuwa kwenye gari ndogo barabara ya Shekilango, kuna dala dala lilikuwa mbele yetu (Ubungo - msasani) Ghafla lilisimama katikati ya barabara na brake light hazifanyi kazi, ujanja hatukuwa nao tukaligonga kwa nyuma na sisi ndio tulioonekana na kosa. Hii ilinifanya kila mara niseme Ditopile alikuwa sahihi kumpiga risasi dereva wa daladala.
Wadau madereva wa daladala wanakera sana na ukiwa na hasira ..........

NI nani wakulaumiwa ???
 
jamaa tulivyomgonga konda alikuja akaangalia gari yake haijaumia akamwambia dereva 'haijaumia twnde zetu'
 
unapoendesha gari assume madereva wengine wote ni VICHAA......guess what.........you will always be safe....labda ugongwe na "KICHAA"
 
wadau kuna siku nilikuwa kwenye gari ndogo barabara ya shekilango, kuna dala dala lilikuwa mbele yetu (ubungo - msasani) ghafla lilisimama katikati ya barabara na brake light hazifanyi kazi, ujanja hatukuwa nao tukaligonga kwa nyuma na sisi ndio tulioonekana na kosa. Hii ilinifanya kila mara niseme ditopile alikuwa sahihi kumpiga risasi dereva wa daladala.
Wadau madereva wa daladala wanakera sana na ukiwa na hasira ..........
siku zote kugonga nyuma ni makosa.
 
Kwa kuongezea katika defensive driving, unatakiwa wakati wote una angalia mwenendo wa gari lililo mbele yako kwani hilo ndiyo litakalo kufanya wewe ujue uendesheje gari lako.
Kwa kusisitiza, kitendo cha kuingia kwa nyuma ni makosa.
Kugonga nyuma ya gari la mwenzako.
 
Ni mambo ya sheria ila sasa inapokuwa mtu wa mbele yako kasimama ghafla au wale wanaoingia barabarani kwa ghafla halafu unamgonga inauumiza sana. Halafu kwa hakika ukigonga kwa nyuma wewe show ya gari inaumia pamoja na defects nyingine na ujue hapo ndo mashine za magari mengi ukiacha bito ndipo zilipo. Kwa daladala nyuma wameweka ngao nzito sana (nyingi) na ukigonga pale tu si rahisi dala iumie ila wewe wa gari ndogo lazima itaumia, walishajihami mapema wakijua wao hawana kituo. Always nikiendesha najitahidi kutokuwa nyuma ya daladala. Halafu kingine ukigongwa katika kituo cha daladala ikiwa inatoka kituoni kuingia barabarani ni kosa pia, ni kuwa makini sana unapoendesha na kukaribia kituo cha daladala slow dawn check usalama. Vinginenvyo ukigongwa hapo huna lako, ni hasara tu.
 
hawa madereva wa daladala/tax ni vurugu sana utakuta daladala halina brake light halsfu usiku limesimama katikati ya barabara. Ila kuna taarifa kuwa bunge litapitia upya hiyo sheria.
 
Kwa kuongezea katika defensive driving, unatakiwa wakati wote una angalia mwenendo wa gari lililo mbele yako kwani hilo ndiyo litakalo kufanya wewe ujue uendesheje gari lako.
Kwa kusisitiza, kitendo cha kuingia kwa nyuma ni makosa.
Fafanua hapo....!
 
Fafanua hapo....!

Mkuu una macho makali.....au unakula mchicha kupita kipimo? LOL.

Utaratibu wa uendashaji wa gari ni rahisi sana.
"Endesha gari ukiwa na uhakika wa kusimama salama inapobidi kufanya hivyo"
Suala la umbali gani kati ya gari na gari inategemea aina ya magari, mwendo kasi, uzima wa magari husika n.k. Kifupi busara yako ndio usalama wako.
Pia hata kama hakuna gari mbele yako, endesha kwa kuzingatia umbali wa barabara unaouna (sight distance), sababu inawezekana barabara ikawa hata imekatika au kuna mti umeanguka...kifupi uwe tayari kusimama salama muda wote!
 
Kwa kuongezea katika defensive driving, unatakiwa wakati wote una angalia mwenendo wa gari lililo mbele yako kwani hilo ndiyo litakalo kufanya wewe ujue uendesheje gari lako.
Kwa kusisitiza, kitendo cha kuingia kwa nyuma ni makosa.

... tehe tehe tehe,,,,kiswahili hiki bwana we acha tu,,,mie langu jicho tu;)
 
Back
Top Bottom