kanganyoro
Senior Member
- Jun 22, 2011
- 127
- 33
Wadau wajuzi wa sheria, naombeni mnisaidie juu la uwepo wa sheria ya hotel levy namba 23 ya mwaka 1972 ambayo inaelekeza mmiliki wa nyumba ya kulala wageni (guest house) kulipa 20% ya mapato yake ghafi ya malazi kwa halmashauri. Nimejitahidi kuitafuta kwenye orodha ya sheria ambazo zilifanyiwa mapitio mwaka 2002 hotel levy act sijaiona. Kama sijaiona ina maana kuna mawili, either ilifutwa au iliunganishwa na sheria nyingine. Cha kushangaza halmashauri za wilaya, manispaa na majiji zimekuwa zikikusanya ushuru wa malazi kwa kila nyumba ya kulala wageni kwa tozo ya asilimia 20 kwa kunukuu sheria namba 23 ya mwaka 1972. Naombeni wajuzi wa sheria mnisaidie juu ya uhalali wa kulipa hotel levy.