Sheria ya Hotel Levy bado ipo?

kanganyoro

Senior Member
Jun 22, 2011
127
33
Wadau wajuzi wa sheria, naombeni mnisaidie juu la uwepo wa sheria ya hotel levy namba 23 ya mwaka 1972 ambayo inaelekeza mmiliki wa nyumba ya kulala wageni (guest house) kulipa 20% ya mapato yake ghafi ya malazi kwa halmashauri. Nimejitahidi kuitafuta kwenye orodha ya sheria ambazo zilifanyiwa mapitio mwaka 2002 hotel levy act sijaiona. Kama sijaiona ina maana kuna mawili, either ilifutwa au iliunganishwa na sheria nyingine. Cha kushangaza halmashauri za wilaya, manispaa na majiji zimekuwa zikikusanya ushuru wa malazi kwa kila nyumba ya kulala wageni kwa tozo ya asilimia 20 kwa kunukuu sheria namba 23 ya mwaka 1972. Naombeni wajuzi wa sheria mnisaidie juu ya uhalali wa kulipa hotel levy.
 
Mi nadhani ipo maana uwa naona pale iringa na kule Arusha wanakusanya. .
 
Mi nadhani ipo maana uwa naona pale iringa na kule Arusha wanakusanya. .
Jambo la kujiuliza hapa ni kwamba, je, mtu ukiingia Guest House unaandikiwa risiti? Unapotaka huduma ya chap chap, ile buku tano inaandikiwa risiti, tena yenye jina la mteja?
 
Back
Top Bottom