Sherehe za miaka 50 uhuru zina umuhimu gani?

sina ubishi na sherehe za miaka 50 ila mpangilio wake nionavyo mm siku ya 9 desemba ingetosha. BASI kama tukiona turasimishe zaidi wiki moja ya maonyesho kabla ya siku yenyewe ingetosha sana. lakini baba miezi sita kabla ni sherehe kila siku. kibaya zaidi agenda kuu ni TUMEFANYA HIKI TUMEFANYA KILE hivi kilichofanyika si huwa kinaonekana ??? kuna sababu ya kutumia gharama kukitangaza ???????????
 
hapa kuna marinjirinji hii Tanzania haina hata hiyo miaka hamsini, lakini suala hapa ni nini umuhimu wa kuwa na matumizi ya pesa zetu shagharabaghara na vp kama zingesaidia kutatua kero za wananchi zinazohitaji hii pesa? vp hata mngewapatia wale watoto wa wakulima waliokosa mikopo ya elimu ya juu mkidai bajeti imefika kikomo! lakini pia ninyi mnaokua mnaunga mkono matumizi kama haya japo mungu amewapatia akili, uelewa, ujinga na kila k2 hamzuiliwi kushabikia huo upuuzi lakini hamjafikilia kama mnatuonesha waanajamii jinsi vichwa vyenu vilivyo na vacuum2 je mnawazidi mawazo kweli watoto wenu?
 
Nimejiuliza sana pasipo kupata majibu wizara, Taasisi za uma, mashirika, mikoa na wilaya zote wanaadhimisha kwambwembwe na gharama kubwa najiuliza pasipo majibu je itatusaidia nini kutuonyesha posta ya mwaka 1970 kisha unatuonyesha posta ya mwaka 2011 tunafaidika na nini au kutuonyesha uzinduzi wa kiwanda miaka ya sabini inatusaidia nini?

Unashangaa!!!!!!! Ndugu yangu nilichoka nilipoona hata TRC eti wanasherehekea miaka 50 ya Uhuru, hata ATC walikuwepo, Watanzania tunaumwa nini ??????
 
hakuna umuhimu wa hizi sherehe-maana wamezipindisha-tutasheherekeaje sherehe za miaka 50 ya tanzania?tanzania ipi?kama si kutupotosha kabsa
viongozi bila aibu wanazitangaza kila siku ili kupotosha watu
 
Mimi nilitegemea huumwaka wa kusherekea Tunge fanya kitu chamaana ambacho hata wajukuu wetu wangekuja kuona kua kulikua na sherehe za miaka hamsini.kama vile sisi tunavyo ona kua kipindi kile cha uhuru watu walijenga minara na kulikua na mwenge na vitu vingi ambavyo hata sasa ukiviona unajuakweli wale wazee walisherekea na walifurahia . lakini chaajabu leo tunakua na moonyesho ya wizara yanafanyika mkoani Dar es salamu pale mnazimmoja ,Hiyo hela inayo tumika kukaa mnazimmoja tungechanganya nazakuchanga kama tunavyo fanya kwenye kampeni tungejenga hosipitali mpya kila wilaya ama shule ama tungenunua ndegekubwa ama treni yakwenda kasi ama barabara moja ya juu ama chochote kingine ilimradi tu baada yamiaka kathaa tukikiona tuseme ulemwaka tulisherekea miakahamsini na tukawa na hiki,
Lakini mpaka sasa sijui kama kunakitu kimefanyika kushuudia kua kweli Tanzania imefikisha miaka hamsini .

Mfano mdogo tu ni kwenye familia zetu huaga tukiwa na birthday tuna toa zawadi ambako inakua na kumbukumbu kwayule mwenye birthday ,hata baada ya miaka miwili atakumbuka.sasa kwa hii miaka hamsini ya uhuru serikali imetuongoza tufanye nini ili kiwe kama kumbukumbu hata baada ya miaka hamsini mingine ?

badala yake wameweka maonyesho Mnazimmoja Dar es salamu je yule mwananch wa kule Masasi aatafikaje mnazimmoja kwaajili ya kujionea hayomaonyesho ya wizara ?so serikali inamwongozaje kwenye kusherekea hiimiaka hamsini ?

Lingine ni hili la slogani ya hii miaka hamsini ya uhuru naisikia watu wanaiongeatu lakini sijawahi kusikia mtu anaitolea ufafanuzi kua ina maana gani ''Tumethubutu tumeweza na tunazidi kusongambele'' huaga nashindwa kuelewa Tumethubutu nini ? yaani ni sawa na nyumba ni yako halafu unamwa nunua godoro kisha uwaambie majirani eti nimethubutu kununua godoro wakati nyumba niyako na kitanada nichako. Ama hii tumethubutu nikua tumethubutu kuibafetha za uma ,Mwenye maana halisi ya hili neno tumethubutu anifafanulie .

Ukija kwenye hii ya tumeweza nayo pia inanichanganya nikipi amabacho tulikua tunashindwa kabla ya uhuru sasa tumeweza ,kabla ya uhuru kulikua hakuna shule zakutosha na kulikua hakuna madawati yakutosha na mpaka sasa havitoshi je tumeweza nini ,ama nihili lakuweza ku iba na kuweka watu wanao chukua rasilimalizetu na hakuna anehoji? umeme ule ule wa uhuru ndo tunao mapakaleo na ile reli alio jenge mkoloni ndo tunayo mpaka leo tumeweza nini ?

ok Tunasongambele hukombele ni wapi , shilingi sasa inazidi kuporomoka kila kukicha ndombele huko? Vifo vya mama wajawazito vinaongezeka ,mashirika viwanda tulivyo kua navyo vime kufa , swali ni kipi tunachosonganancho mbele ?

Mimi sioni faida ya hayo moonyesho pale mmnazimmoja zoidi naona niupotevu wahela za walipa kodi huku wakiwa wanafaidi wachache
 
Wizara ya fedha walikata kama wiki mbili pale mnazi mmoja uku wakiwachezesha dance watoto wa Jitegemee Sec School wale kama sikosei meanwhile uchumi wa nchi unasua sua!
Am sure ukijumlisha ela zote watakazotumia zitafika mabilioni kadhaaa
Ivi na hawa donors hawaoni haya na bado wanaendelea kutoa misaada?

Donor wenyewe hiyo misaada yao ni kama robo tu ya kile wanachotuibia! sisi wa-tz na sirikali ya magamba ni wajinga ndio waliwao!
 
Hakuna umuhimu wowote kusherehekea nchi iliyouawa na wanasiasa bila ridhaa ya wananchi wote. Tuna matatizo kibao ya msingi tungeyamaliza kwanza ndo tukasherekea. Wao wanafurahia kwa vile wanalipana posho kubwa kubwa na kuvishana T-shirt na kofia utadhani tuko kwenye kampeni za uchaguzi! Na siku wakitangaza wasiseme watanzania wote wanasherekea, waseme watanzania wanasherekea kasoro Anko Sam!
 
Si ajabu serikali inaelekea kufilisika! Kila Wizara ina wiki yake ya kutangaza mafanikio yake kwenye vyombo vya habari ambapo mamilioni ya pesa hutumika!
 
Lengo lake ni moja tu; kuwaelimisha magwanda kuwa mambo mengi sana ya kimaendeleo yamefanyika hapa nchini tangu tupate uhuru; ili waache kuendelea kupotosha umma kwamba tangu uhuru wa nchi hii hakuna kilichofanyika!!!
 
Lengo lake ni moja tu; kuwaelimisha magwanda kuwa mambo mengi sana ya kimaendeleo yamefanyika hapa nchini tangu tupate uhuru; ili waache kuendelea kupotosha umma kwamba tangu uhuru wa nchi hii hakuna kilichofanyika!!!

Ni vigumu kuamini kuwa takeurabu kama ni mzazi anao watoto !
Ni vigumu kuamini kuwa takeurabu kama ni kijana anao wazazi !
Ni vigumu kuamini kuwa takeurabu kama ni mwanamke anaye mume !
Ni vigumu kuamini kuwa takeurabu kama ni mwanamme anaye mke !

Na kwa misingi hiyo hiyo;

Ni vigumu kuamini kuwa takeurabu kama anayo macho anaweza kuona.
Ni vigumu kuamini kuwa takeurabu kama anayo masikio anaweza kusikia.
Ni vigumu kuamini kuwa takeurabu kama anayo pua anaweza kunusa.
Ni vigumu kuamini kuwa takeurabu anacho kichwa kina chembe cha akili.

Hata hivyo;

Ni rahisi kuamini kuwa ni kwa sababu ya watu kama takeurabu, hadi leo CCM iko madarakani.
Ni rahisi kuamini kuwa ni kwa sababu ya watu kama takeurabu, Kikwete yuko madarakani.
Ni rahisi kuamini kuwa ni kwa sababu ya watu kama takeurabu, ujinga umejikitaTanzania.
Ni rahisi kuamini kuwa ni kwa sababu ya watu kama takeurabu, nchi imekithiri umasikini.

Lakini pamoja na hayo yote;

Inatia moyo kuwa wanafiki kama takeurabu, hata nafsi zao zinaanza kuwasuta
Inatia moyo kuwa walafi kama takeurabu, wananchi wanaanza kuwashtukia
Inatia moyo kuwa waliolala kama takeurabu, jamii itawaamsha hata kwa mijeledi
Inatia moyo kuwa watu kama takeurabu, siku zao zimeanza kuhesabika tik..tak..

Kwa mbali naliona taifa inayopiga hatua kimaendeleo bila CCM.
Kwa mbali naiona Tanzania yenye neema bila watu kama takeurabu.
Kwa mbali nawaona wananchi wakipiga hatua ya mendeleo bila ufisadi.
Kwa mbali naiona nchi madhubuti isiyo na utawala legelege kama wa Kikwete.
 
Na msishangae kuwa asilimia 50% ya bajeti ni kwa ajili ya events kama hizi za kipuuzi zisizo na tija kwa taifa

kweli bongo ni nchi ya kusadikika, i think it is not a real one
 
Watanzania wachache wenye ubongo wenye akali yakuweza kujikomboa kifkra wengi pamoja na viongozi wao kama jike na ccm unaishi kwakuwa wamejikuta wanaishi.
Mpaka leo watu wanaoji dhana nzima ya sherehe ya mwika 50 ya uhuru wa Tangazania bara lakini hakuna majibu yanayotolewa.Wanabaki kutoa kejeri tu kwa watu wenye utashi wakujua mambo ili kuweza kuweka mstakabari mzuri wa nchi yao.
Ukiuliza watasema wewe muaini,unahatarisha usalama,muungano na siyo mzalendo!heh Jamii ilijue na kuelewa hili kuwa bila kuwa na utashi au kiu ya kujua basi jamii hiyo imekufa kifra na inaishi kwa matukio kitu ambacho sitabia ya mwanadam aliyestaharabika(civilised social creature)
 
hizo fedha wangenunua madawati kwa shule za msingi amabazo madawati kwo wanayaona kwenye pic za vitabu
 
Kiukweli mimi sioni mantiki ya kusherekea hiyo miaka hamsini japo unaweza kusherekea birthday lakini si yatanganyika kwasababu wanazidi kunitia machungu kwani wanatumia pesa nyingi kwenye maadhimisho yasiyo na msingi je nami nauliza Hio siku serikali itatueleza nini wanachojivunia?Kama ni gari basi tanganyika ni gari bovu ambalo linaenda polepole kama tolori kwani walichokifanya hakiendani na miaka hamsini.Ni mimi mwanaharakati
 
Wewe ndio unapotosha jamii hayo maendeleo unayoyasema ni yapi yanayolingana na miaka hamsini kama si ufisadi na kujilimbikizia mali kwa walio wachache.Naomba uniambie ni wananchi wangapi tanganyika au asilimia ngapi wanaotumia umeme ambao ndio chachu ya maendeleo kwenye nchi yoyote hapo ndipo utagundua ni uzandiki mtupu unaofanyika
 
Tanzania ni nchi masikini lakini si kiasi cha kutosherehekea sherehe zetu za kitaifa. Kila nchi duniani ina siku yake ya kuzaliwa na inasherehekewa ipasavyo. Labda ungeleta hoja nyingine lakini kwa hili sidhani kama una pointi.

Nimeanza kusoma tu umenichefua,ww hulew alichokisema jamaa,ni uhuru wa tanganyika au tanzania?maana tanganyika haipo mbona mgumu kuelewa ucwe kichwa maji.
 
Lengo ni kuwalazimisha watanganyika waamini kwamba kuna kitu ccm wamekifanya tangia uhuru ilihali wanajua ni wizi mtupu! na sasa serikali ndiyo inazidi kufilisika,

Mimi ngoja niwape mfano:

Hivi kuna umuhimu gani kwa wizara ya Afya kusherehekea miaka hamsini kwa kutumia mamilioni ya shilingi za walipa kodi wakati pale Muhimbili sasa ni wiki ya pili CT SCAN haifanyi kazi!? inaingia akilini? nini cha muhimu kununua spear ya hiyo mashine ili iweze kuwahudumia wanannchi au kwenda pale mnazi mmoja na kufuja pesa for nothing!?.jamani humu kunawanahabari wengi sana hebu nendeni mkachunguze hii kitu pale muhimbili, nimempeleka mgonjwa wangu pale MOI naambiwa CT Scan haifanyi kazi sasa ni wiki ya pili na alikuwa amelazwa tu pale akiambiwa atafanyiwa ct scan, ilibidi nichukue ambulance nimpeleke TMJ apate hiyo huduma na kumrudisha MOI, na amekutwa na tatizo; ni pesa imetumika hapo.

sasa niambieni ni wagonjwa wangapi wanapoteza maisha pale muhimbili kwa kukosa huduma hiyo na serikali inaendelea kutumia mamilioni kufanya tafrija za miaka 50?, na wakati wanasema hawana pesa ya kununua spear ya hicho kifaa. kweli tupo sawa kweli hapo jamani,

CT SCAN agakhan na TMJ bei yake wakuu mnaijua!? sasa nielezeni watu wa Buguruni malapa watamudu hiyo kweli?

nchi yetu kwa kweli hatuna viongozi wanaofikiri kwa umakini na kwa kutumia akili.
 
Ni vigumu kuamini kuwa takeurabu kama ni mzazi anao watoto !
Ni vigumu kuamini kuwa takeurabu kama ni kijana anao wazazi !
Ni vigumu kuamini kuwa takeurabu kama ni mwanamke anaye mume !
Ni vigumu kuamini kuwa takeurabu kama ni mwanamme anaye mke !

Na kwa misingi hiyo hiyo;

Ni vigumu kuamini kuwa takeurabu kama anayo macho anaweza kuona.
Ni vigumu kuamini kuwa takeurabu kama anayo masikio anaweza kusikia.
Ni vigumu kuamini kuwa takeurabu kama anayo pua anaweza kunusa.
Ni vigumu kuamini kuwa takeurabu anacho kichwa kina chembe cha akili.

Hata hivyo;

Ni rahisi kuamini kuwa ni kwa sababu ya watu kama takeurabu, hadi leo CCM iko madarakani.
Ni rahisi kuamini kuwa ni kwa sababu ya watu kama takeurabu, Kikwete yuko madarakani.
Ni rahisi kuamini kuwa ni kwa sababu ya watu kama takeurabu, ujinga umejikitaTanzania.
Ni rahisi kuamini kuwa ni kwa sababu ya watu kama takeurabu, nchi imekithiri umasikini.

Lakini pamoja na hayo yote;

Inatia moyo kuwa wanafiki kama takeurabu, hata nafsi zao zinaanza kuwasuta
Inatia moyo kuwa walafi kama takeurabu, wananchi wanaanza kuwashtukia
Inatia moyo kuwa waliolala kama takeurabu, jamii itawaamsha hata kwa mijeledi
Inatia moyo kuwa watu kama takeurabu, siku zao zimeanza kuhesabika tik..tak..

Kwa mbali naliona taifa inayopiga hatua kimaendeleo bila CCM.
Kwa mbali naiona Tanzania yenye neema bila watu kama takeurabu.
Kwa mbali nawaona wananchi wakipiga hatua ya mendeleo bila ufisadi.
Kwa mbali naiona nchi madhubuti isiyo na utawala legelege kama wa Kikwete.
haya ni mashairi tu ambayo tumeshazoea kuyasikia kwa mrisho mpotu; ndugu yangu mambo mengi sana yamefanywa tangia uhuru mpaka hii leo ila kwa kuwa CDM hamna macho ya kuyaona ndiyo maana serikali inatumia nguvu nyingi kuwajuza; baadhi ya maendeleo hayo ni kama ifuatavyo:

1. ELIMU
  • Kutoka chuo kikuu kimoja cha serikali mpaka 13 leo hii
  • kutoka shule 600 (2005) HADI 4000 za sekondari leo hii
  • elimu ya msingi kufikishwa mpaka ngazi ya kitongoji
  • kutoka wahandisi 2 wakati tunapata uhuru mpaka kufikia zaidi ya 5000 leo hii
  • ongezeko la fedha za mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu aina zote yaani serikali na binafsi
2. Afya:
  • uboreshwaji wa hospitali za rufaa za muhimbili, KCMC, Bugando ili kutoa huduma za upasuaji wa moyo, mishipa ya fahamu, tiba ya saratani, tiba bingwa za meno na kinywa ambazo zilikuwa hazipatikani hapa nchini
  • upanuzi wa hospitali za mikoa, wilaya na vituo vya afya
  • ujenzi wa zahanati kila kijiji na kituo cha afya kwa kila kata
  • ongezeko kubwa la madaktari kutoka 12 (1961) hadi kufikia zaidi ya 1500 hii leo
3. Miundombinu:
  • ujenzi mkubwa wa barabara kutoka chini ya km 1000 wakati tunapata uhuru hadi kufikia km 12,000 kwa kiwango cha rami ifikapo 2014, kwa sasa km 6000 tayari zimekamilika na kandarasi wapo site maeneo mbalimbali hapa nchini ili kukamilisha mngwe iliyobaki
4. Kilimo:
  • utoaji wa ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha ambapo wakulima zaidi ya milioni moja hunufaika kila mwaka
  • kuajiri maafisa kilimo wengi zaidi kuliko kipindi chochote kile na kuwasambaza vijijini ili kuwasaidia wakulima
  • nchi kuendelea kujitoshereza kichakula
5. Mawasiliano:
  • sekta hii imekuwa kwa kasi kubwa na kuchangia pato kubwa la taifa
6. Makusanyo ya kodi ya mapato:
  • makusanyo yameongezeka kwa kiasi kikubwa ambapo sasa inakadiriwa kufikia bilioni 600 kwa mwezi kutoka bilioni 250 (2005)
7. Ulinzi na usalama:
  • amani imeendelea kutawala hapa nchini hata hili nalo hulioni kama ni fanikio kubwa?
8. uhuru wa vyombo vya habari na utawala bora:
  • uhuru wa vyombo vya habari umetawala hapa nchini ambapo CDM mnabwabwaja hovyo, mpaka kufikia kumtukana rais, lakini rais yupo kimya tu kwa kuheshimu uhuru wenu wa kuongea
  • utawala wa kidemokrasia pia umeshamili ambapo kila kukicha CDM mnafanya maandamano bila bugudha yoyote ile
Michezo:
  • Ujenzi wa uwanja mpya wa kisasa Dar unaoitwa uwanja wa taifa
  • Timu ya taifa kuchukua ubingwa wa CECAFA 2010
  • Timu ya taifa kufuzu mashindano ya CHAN
  • Twiga stars kufuzu kombe la mataifa ya africa 2010
  • Twiga stars kufuzu mashindano ya All african games
  • Twiga stars kushika nafasi ya tatu kombe la COSAFA
  • Taifa Queen kufanya vyema mashindano ya All african games
YAPO MENGI ILA HAYO KWANZA YANAKUTOSHA
 
Back
Top Bottom