Very sad indeed!This is really sad !
Yule anayetaka kugombea Kyela au?
Very sad indeed!
Matukio yalivyojiri katika picha...
Mhe Pius Msekwa akihutubia wageni na wanachama wa CCM Tawi la Uingereza.
Wageni waalikwa na wanachama wa CCM wakimkiliza kwa makini mgeni rasmi, Mhe Pius Msekwa.
Mgeni rasmi Mhe Pius Msekwa akitoa mkono wa pongezi na karibu kwenye Chama Cha Mapinduzi kwa baadhi ya Viongozi/ Wanachama wapya.
Mhe Pius Msekwa akikabithi vitendea kazi kwa viongozi wapya wa Mashina mapya ya CCM ya London East na South.
Mhe Msekwa akiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama wapya wa CCM Tawi la Uingereza.
Mlitegemea kitu tofauti? Kwa vipi? Inawezekana vipi kupata matokeo tofauti wakati input ni ileile?
kweli kusudi lake nini sijui? kama katumwa na ccm na akome.Nini kusudi la posti yako?
Wewe uliyebandika hii posti endelea na kazi yako ya IT siasa waachie wanasiasa utaumia ndugu yangu. Na ushauri kwa wale mlioko huko ughaibuni muendelee kazi zenu za kusafisha vibibi msitegemee kuwa mkiwa proactive katika politics mtapata access ya kuwa mafisadi bongo hilo halitawasadia bongo siasa zake ni za visasi na kuna royal family Tanzania mie na wewe tutaishia katikati,na vilevile watu hawataki kukosolewa ukiwakosoa tu kisasi kinaanza.
Adios!!!
yaani hizi picha zimenichefua kabisa,kichefuchu nahisi kutapika kabisa.yaani kuwa kwao nje kote bado hajakombolewa kifkra? tuwape pole watu hawa
-Labda hawa
Ni ngumu kuamini kwamba watu na akili zao wanaweza wakaa nje ya nchi na kushabikia sisiemu, wanacheka na kufurahia maisha, ni aibu! Au wanatafuta ubunge wa kuteuliwa baada ya uchaguzi?? Yaani kinachowavutia kuipenda sisiemu kiasi hicho nini hasa?
Matukio yalivyojiri katika picha...
Mhe Pius Msekwa akihutubia wageni na wanachama wa CCM Tawi la Uingereza.
Wageni waalikwa na wanachama wa CCM wakimkiliza kwa makini mgeni rasmi, Mhe Pius Msekwa.
Mgeni rasmi Mhe Pius Msekwa akitoa mkono wa pongezi na karibu kwenye Chama Cha Mapinduzi kwa baadhi ya Viongozi/ Wanachama wapya.
Mhe Pius Msekwa akikabithi vitendea kazi kwa viongozi wapya wa Mashina mapya ya CCM ya London East na South.
Mhe Msekwa akiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama wapya wa CCM Tawi la Uingereza.
Hebu tusaidiane mawazo kwenye hili Mkuu sababu mimi linaniumiza kichwa.
Hawa Watanzania walio nje; hawana shida ya maji, umeme, usafiri, n.k lakini kwa kuzingatia uhuru na busara zao wameamua kujiunga pamoja na kusheherekea kuzaliwa kwa CCM.
Watanzania wengi walioko Dar-es-salaam wana shida ya maji, umeme, usafiri n.k na wao pia kwa uhuru wao wameipigia 2005 wameipigia kura CCM katika viti vyote vya Ubunge.
Ni Watanzania wa upande gani wanastahili pole kati ya hawa?
Tusaidiane mawazo mkuu bila jazba.
Kwanza, ni lazima tutambue kwamba kila mtu ana haki ya kuwa mwanachama wa chama chochote anachokitaka. Sina uhakika kwamba kila mtu ana haki ya KUTOKUWA mwanachama wa chama anachokitaka. Maana mpaka leo Tanzania haturuhusu mtu yeyote asiye muumini wa chama kugombea public office.
Ukiangalia hawa kaka na dada zetu walio "majuuu" wakiwa wanaimba pambio za CCM kuna mengi unaweza jiuliza na kufikiria kwa kina. Je ni kweli kwamba wanataka wawe part ya "system" kusudi waweze kuibadilisha wakiwa ndani? historia haitu-support kwa hili. Maana "we have seen many who entered politics with a goal of changing politics, but politics ended up changing them" NA HAWA NDO WENGI SANA.. Au hawa wanataka wawe karibu na wakulu kusudi waweze kuwa na access ya walio madarakani? Kwa uzoefu wangu hapa Tanzania uwezekano mkubwa ni kwamba wengi wa hao walio kwenye picha na Msekwa wanataka wawe karibu na wazee wa chama kusudi ....well...wapate opportunities.
Sasa hao ndugu zetu wa majuu nadhani ni vyema wakajua kwa nini watu wako dissapointed na wao (specifically kwenye hii thread). Ni kwa sababu "to whom much is given, much is expected". Wengi tungewategemea hawa kwa vile wameenda nje, wameona democrasia ya kweli inavyofanya kazi, watu wanavyoadhibiwa wakifuja madaraka/mali ya umma nk. Lakini hawa hawa leo wanarudi kubariki yale tunayopigana nayo usiku kucha. Sasa hebu twambieni nyinyi mlio huko nje mna msaada gani kwa wananchi wenzenu? (hata msaada wa mawazo naona haupo!).
Na jee mtashangaa kweli mnapoona wananchi wanapinga uraia wa nchi mbili? Maana tayari mnaonekana (katika macho ya wengi) kwamba you are just selfish. You are out of touch with common people. Why? kwa sababu tumewaona watuhumiwa kibao hapa ambao wametuibia billions and billions..wakija huko (kwa kodi zetu) wanavyopokelewa kama waheshimiwa ambao wamefanya mambo makubwa kwa wananchi).
In all, I dont fault anyone kuingia kwenye chama anachokitaka. Hata ingekuwa Chadema, CUF nk I would have said the same. Lakini kwa vile CCM ndo chama chenye DOLA..ndo maana macho ya wengi yako kwake. Tunategemea kuona watanzania walio huko nje (well not all of them are doing well, maana wengine wana njaa kali tuu kama huku dunia ya nne...anyway). Lakini wawe na ile minimum decency ya kuelewa kwa nini watanzania sasa increasingly tunaona kila mtu aliye karibu na CCM ni opportunist na fisadi. correctly or wrongly.
Masanja