nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
na Hellen Ngoromera
MNAJIMU Mkuu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein, amewatabiria viongozi wa siasa na wafanyabiashara maarufu kutekwa nyara.
Sheikh Yahaya amewatabiria pia viongozi hao, wake zao au maswahiba zao kuibiwa na kufanywa kama bidhaa.
Alisema hayo jana katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari kuhusu utabiri wake wa mwezi huu.
Kuanzia Aprili 19 na kuendelea hadi Julai, viongozi wa siasa na wafanyabiashara maarufu wajichunge kutekwa nyara na kuibiwa, wao wenyewe na kufanywa kama bidhaa.
Aliwataka wachukue tahadhari hasa wanapotembea na kusafiri kwani kuna uwezekano wasirudi mara watakaposafiri.
Utekaji nyara huo ni wa viongozi tuliowataja na wasijiamini wanaposafiri au wakiwa kwenye mikutano wasiwe peke yao na wawe na mipangilio ya tahadhari nyakati zote. Kwa mujibu wa Sheikh Yahaya ambaye amekuwa akitabiri mambo mbalimbali, nyota hizo pia zinawalenga wake na maswahiba wa viongozi hao mashuhuri.