Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,178
- 7,320
Sio Mazoea yangu hata siku moja kuanzisha wala kuchangia topic zinazohusiana na dini. Hata hivyo kwa leo naomba tu nimwambie huyu shehe anayefanya kipindi live pale channel ten (kama sijakosea anaitwa Mohamed, kama nimekosea aniwie radhi) kuwa kati ya hoja zake kumi juu ya mahakama ya kadhi, ni moja tu iliyokuwa sahihi, na ya pili ambayo hakuitaja kabisa.
Shehe alijitahidi kueleza kisomi sana kuhusu suala kuwa serikali itamlipaje kadhi, ilhali hayupo kwa maslahi ya taifa zima. Hoja yake ni kuwa hata sasa mahakimu wa kawaida (wa serikali), wanaolipwa na kodi za watanzania wote, bado wanahukumu kesi za masuala ya kiislamu (ndoa, mirathi, wakfu, malezi ya watoto) ambayo yanayohisiana na kadhi. Kwa hiyo mwanazuoni huyu anasema kuwa kama wanalipwa mahakimu hawa ambao wanafanya kazi, pamoja na hizi zinazohusiana na dini, then hakuna ubaya wakiwepo wanaohusika na dini (kadhi) peke yake, na bado akalipwa na serikali (kama nilikuelewa vyema, ndivyo ulivyomaanisha mwalimu).
Hata hivyo pamoja na hoja zako shehe, mi napenda kukujulisha yafuatayo
1. Hoja kuwa wasio waislamu wanakataa kadhi kwa sababu ya 'wivu' wa kidini, kwangu mimi sio kweli, mi (naamini na wengi wasio waislamu) nakataa kadhi kwa sababu ya kodi yangu.
2. Hoja yako kuwa mahakimu wa serikali wa kawaida bado wanafanya kazi za kadhi ni sahihi lakini kumbuka hawa hawafanyi tu za kadhi, wanahukumu pia kesi za kimila (kikabila), kiukoo nk. Kama tukisema awepo hakimu (kadhi) anayelipwa na serikali leo, then tutawakataliaje wasambaa wakitaka hakimu wao atakayehukumu kesi zao za kimila? wapare je? wasukuma/ nk.
Hapa namaanisha kuwa yapo makundi tofauti ya watu humu nchini wenye sheria zao wanazozitambua, hivyo sio busara kila kundi (wakiwemo waislamu), kutaka awepo hakimu specific wa kuhukumu tu kesi zao, na bado alipwe na serikali. Mi nadhani utaratibu wa sasa kuwa kama hakimu wa kawaida hana weledi katika sheria za kundi fulani la dini au kabila, au jingine lolote, then kwa mujibu wa sheria hakimu huyo ana mamlaka ya kuomba ushauri kutoka ndani ya kundi hilo, mathalani masheikh, kwa mfano.
Serikali itabeba mzigo mkubwa sana kama ikiruhusu kila dini, na kila kundi likawa na taasisi yake inayolipwa nayo.
Bado hoja ulizotoa sheikh kuwa ni kwanini waislamu wasianzishe mahakama ya kadhi chini ya mamlaka yao wenyewe, eti itakosa authority kwa maana kuwa kunaweza kuwa na makundi tofauti, kwangu hiyo ni hoja dhaifu na inayowadhalilisha waislamu. Sidhani kama taasisi kubwa kama waislamu wanaweza kushindwa kuwa na hierarchy inayoheshmika kiasi cha kuwa na makundi yanayopingana. Sijawahi kusikia kumekuwa na Mufti wakuu wawili Tanzania, je mufti anateuliwa na raisi? Sasa iweje watu ambao wana uwezo wa kuchagua,na kumheshimu kiongozi wa taasisi yao nchini watashindwa kufanya kwa sehemu tu ya taasisi hiyo, yaani kadhi.
Sheikh Mohamed pamoja na waislamu wote wenye nia ya kushinikiza serikali ikubali mahakama ya kadhi kuwa chombo cha dini kinachoendeshwa na serikali, naomba niwashauri kuwa, kama kweli mnapenda amani ya nchi hii, basi heshimuni dini nyingine na muanzishe hiyo mahakama bila ya kuihusisha serikali, kwa hata dini zingine zimeanzisha taasisi nyingi sana bila kuihusisha serikali, Hakuna sababu ya kuitumbukiza hii nchi katika malumbano yasiyo na msingi, nawaomba ndugu zangu waislamu...