Sheikh Mohamed; Sio 'wivu' wa kidini, ni fedha zetu, only

Mambo yote ya kidini yakafanyikie kwenye nyumba za ibada na yatagharimiwa na yataendeshwa na waumini wenyewe full stop! Mimi naamini iwapo kama serikali ikiruhusu madhehebu ya kidini yaanzishe mahakama zake na watakao patikana na hatia wapelekwe jela za Serikali, basi madhehebu ya kikristo yanaweza kuanzisha na kugharimia uendeshaji wake bila kuidai serikali hata shilingi moja.

Kwa kabila la wasukuma walikuwa na mahakama na jeshi lake la sungusungu, liliendesha mambo yake bila kupata ruzuku toka serikalini. Watu wali waamini sana sungusungu na wakawa hawapeleki mashauri yao polisi wala mahakamani. Polisi na mahakimu walivyo ona mlungula umepungua, wakalipiga vita jeshi hilo mpaka likakosa nguvu!

Je wasukuma nao wadai jeshi na mahakama zao ili amani irudi kwenye maeneo yao wanayoishi? Iwapo kama waislamu (dini ya kushushwa/kuteremshwa!) ikikubaliwa, basi na wasukuma TUTAHAMASISHANA JESHI LETU LA SUNGUSUNGU NA MAHAKAMA ZETU ZA KIMILA ZITAMKWE KWENYE KATIBA NA ZIGHARIMIWE NA SERIKALI! Na moto huo huo utakwenda mpaka kwenye makabila mengine, kisha tutaona kitakacho tokea!
 
Sio Mazoea yangu hata siku moja kuanzisha wala kuchangia topic zinazohusiana na dini. Hata hivyo kwa leo naomba tu nimwambie huyu shehe anayefanya kipindi live pale channel ten (kama sijakosea anaitwa Mohamed, kama nimekosea aniwie radhi) kuwa kati ya hoja zake kumi juu ya mahakama ya kadhi, ni moja tu iliyokuwa sahihi, na ya pili ambayo hakuitaja kabisa.

Shehe alijitahidi kueleza kisomi sana kuhusu suala kuwa serikali itamlipaje kadhi, ilhali hayupo kwa maslahi ya taifa zima. Hoja yake ni kuwa hata sasa mahakimu wa kawaida (wa serikali), wanaolipwa na kodi za watanzania wote, bado wanahukumu kesi za masuala ya kiislamu (ndoa, mirathi, wakfu, malezi ya watoto) ambayo yanayohisiana na kadhi. Kwa hiyo mwanazuoni huyu anasema kuwa kama wanalipwa mahakimu hawa ambao wanafanya kazi, pamoja na hizi zinazohusiana na dini, then hakuna ubaya wakiwepo wanaohusika na dini (kadhi) peke yake, na bado akalipwa na serikali (kama nilikuelewa vyema, ndivyo ulivyomaanisha mwalimu).

Hata hivyo pamoja na hoja zako shehe, mi napenda kukujulisha yafuatayo
1. Hoja kuwa wasio waislamu wanakataa kadhi kwa sababu ya 'wivu' wa kidini, kwangu mimi sio kweli, mi (naamini na wengi wasio waislamu) nakataa kadhi kwa sababu ya kodi yangu.
2. Hoja yako kuwa mahakimu wa serikali wa kawaida bado wanafanya kazi za kadhi ni sahihi lakini kumbuka hawa hawafanyi tu za kadhi, wanahukumu pia kesi za kimila (kikabila), kiukoo nk. Kama tukisema awepo hakimu (kadhi) anayelipwa na serikali leo, then tutawakataliaje wasambaa wakitaka hakimu wao atakayehukumu kesi zao za kimila? wapare je? wasukuma/ nk.

Hapa namaanisha kuwa yapo makundi tofauti ya watu humu nchini wenye sheria zao wanazozitambua, hivyo sio busara kila kundi (wakiwemo waislamu), kutaka awepo hakimu specific wa kuhukumu tu kesi zao, na bado alipwe na serikali. Mi nadhani utaratibu wa sasa kuwa kama hakimu wa kawaida hana weledi katika sheria za kundi fulani la dini au kabila, au jingine lolote, then kwa mujibu wa sheria hakimu huyo ana mamlaka ya kuomba ushauri kutoka ndani ya kundi hilo, mathalani masheikh, kwa mfano.

Serikali itabeba mzigo mkubwa sana kama ikiruhusu kila dini, na kila kundi likawa na taasisi yake inayolipwa nayo.

Bado hoja ulizotoa sheikh kuwa ni kwanini waislamu wasianzishe mahakama ya kadhi chini ya mamlaka yao wenyewe, eti itakosa authority kwa maana kuwa kunaweza kuwa na makundi tofauti, kwangu hiyo ni hoja dhaifu na inayowadhalilisha waislamu. Sidhani kama taasisi kubwa kama waislamu wanaweza kushindwa kuwa na hierarchy inayoheshmika kiasi cha kuwa na makundi yanayopingana. Sijawahi kusikia kumekuwa na Mufti wakuu wawili Tanzania, je mufti anateuliwa na raisi? Sasa iweje watu ambao wana uwezo wa kuchagua,na kumheshimu kiongozi wa taasisi yao nchini watashindwa kufanya kwa sehemu tu ya taasisi hiyo, yaani kadhi.

Sheikh Mohamed pamoja na waislamu wote wenye nia ya kushinikiza serikali ikubali mahakama ya kadhi kuwa chombo cha dini kinachoendeshwa na serikali, naomba niwashauri kuwa, kama kweli mnapenda amani ya nchi hii, basi heshimuni dini nyingine na muanzishe hiyo mahakama bila ya kuihusisha serikali, kwa hata dini zingine zimeanzisha taasisi nyingi sana bila kuihusisha serikali, Hakuna sababu ya kuitumbukiza hii nchi katika malumbano yasiyo na msingi, nawaomba ndugu zangu waislamu...

Nashauri pia askofu mkuu wa KKKT achaguliwe na rais kumpa uwezo wa kuadibisha waumini wake katika masuala ya uadilifu, kuwajali wenye shida katika jamii (kama yatima na wajane) maana hiyo ndiyo ibada inayokubalika kwa Mungu. Leo jamii ina watoto yatima na wa mitaani kwa vile maaskofu wamepoteza uwezo wa kuwabana washirika wao tena wengine wana uwezo mkubwa kuwajali yatima na wajane.

Tena napendekeza maaskofu walipwe mishahara na serkali kwani idara ya ustawi wa jamii imekuwa ikitekeleza majukumu yake vibaya huku maofisa wakilipwa mishahara na serkali.

Pia napendekeza sheria ya ndoa ya mwaka 1973 ifutwe kwani jamii yetu imegawanyika katika makundi mbali mbali ya imani na utamaduni. Wahaya wanazo taratibu zao tena za kale za kufunga ndoa. Waachiwe wafunge ndoa za kihaya, waislamu waachiwe ndoa zao wazifunge kupitia kadhi, wakristo nao wanao mwongozo wao kuhusu kufunga ndoa wautumie bila kulazimishwa na serkali kuweka mashahidi na kutangaza ndoa siku 21 ( maana vijana wengine wanawahi masomoni na ughaibuni hivyo wasibanwe na sheria hii). Kikristo ndoa lazima ihusishe wazazi (biblia husema mwanaume anatokea kwa wazazi wake kabla ya kuambatana na mkewe). Hivyo wakristo nao waendeshe ndoa kwa sheria zao. Tena wale wafungishaje na kamati zote za ndoa za makanisani zitambuliwe na kugharimiwa na serkali kuliko ambavyo Afisa tawala (w) analipwa fedha nyingi na kuishia kufunga ndoa bila hata wazazi kujua. ( Ananajisi imani huyu). n.k
 
Waislam tuwemacho, maswala nyeti kama ya kadhi sio ya Kufuata makumbo. Leo tunaona Ni rahisi kudai mahakama hii lakini ikianza kufanya Kazi chini ya usimamizi wa serikali na ikiwekwa chini ya sheria za serikali hatutakuwa na uwezo sana nayo maana kitakuwa chombo Cha serikali na kinaweza kutumika kutuchakachua na kutubana Waislam badala ya kutatua matatizo yetu. Tutafakari kwanza kwa undani. Mi naona ndani yetu Kuna watu waliopandwa kutuburuza Katika mambo mengi.
 
Sio Mazoea yangu hata siku moja kuanzisha wala kuchangia topic zinazohusiana na dini. Hata hivyo kwa leo naomba tu nimwambie huyu shehe anayefanya kipindi live pale channel ten (kama sijakosea anaitwa Mohamed, kama nimekosea aniwie radhi) kuwa kati ya hoja zake kumi juu ya mahakama ya kadhi, ni moja tu iliyokuwa sahihi, na ya pili ambayo hakuitaja kabisa.

Shehe alijitahidi kueleza kisomi sana kuhusu suala kuwa serikali itamlipaje kadhi, ilhali hayupo kwa maslahi ya taifa zima. Hoja yake ni kuwa hata sasa mahakimu wa kawaida (wa serikali), wanaolipwa na kodi za watanzania wote, bado wanahukumu kesi za masuala ya kiislamu (ndoa, mirathi, wakfu, malezi ya watoto) ambayo yanayohisiana na kadhi. Kwa hiyo mwanazuoni huyu anasema kuwa kama wanalipwa mahakimu hawa ambao wanafanya kazi, pamoja na hizi zinazohusiana na dini, then hakuna ubaya wakiwepo wanaohusika na dini (kadhi) peke yake, na bado akalipwa na serikali (kama nilikuelewa vyema, ndivyo ulivyomaanisha mwalimu).

Hata hivyo pamoja na hoja zako shehe, mi napenda kukujulisha yafuatayo
1. Hoja kuwa wasio waislamu wanakataa kadhi kwa sababu ya 'wivu' wa kidini, kwangu mimi sio kweli, mi (naamini na wengi wasio waislamu) nakataa kadhi kwa sababu ya kodi yangu.
2. Hoja yako kuwa mahakimu wa serikali wa kawaida bado wanafanya kazi za kadhi ni sahihi lakini kumbuka hawa hawafanyi tu za kadhi, wanahukumu pia kesi za kimila (kikabila), kiukoo nk. Kama tukisema awepo hakimu (kadhi) anayelipwa na serikali leo, then tutawakataliaje wasambaa wakitaka hakimu wao atakayehukumu kesi zao za kimila? wapare je? wasukuma/ nk.

Hapa namaanisha kuwa yapo makundi tofauti ya watu humu nchini wenye sheria zao wanazozitambua, hivyo sio busara kila kundi (wakiwemo waislamu), kutaka awepo hakimu specific wa kuhukumu tu kesi zao, na bado alipwe na serikali. Mi nadhani utaratibu wa sasa kuwa kama hakimu wa kawaida hana weledi katika sheria za kundi fulani la dini au kabila, au jingine lolote, then kwa mujibu wa sheria hakimu huyo ana mamlaka ya kuomba ushauri kutoka ndani ya kundi hilo, mathalani masheikh, kwa mfano.

Serikali itabeba mzigo mkubwa sana kama ikiruhusu kila dini, na kila kundi likawa na taasisi yake inayolipwa nayo.

Bado hoja ulizotoa sheikh kuwa ni kwanini waislamu wasianzishe mahakama ya kadhi chini ya mamlaka yao wenyewe, eti itakosa authority kwa maana kuwa kunaweza kuwa na makundi tofauti, kwangu hiyo ni hoja dhaifu na inayowadhalilisha waislamu. Sidhani kama taasisi kubwa kama waislamu wanaweza kushindwa kuwa na hierarchy inayoheshmika kiasi cha kuwa na makundi yanayopingana. Sijawahi kusikia kumekuwa na Mufti wakuu wawili Tanzania, je mufti anateuliwa na raisi? Sasa iweje watu ambao wana uwezo wa kuchagua,na kumheshimu kiongozi wa taasisi yao nchini watashindwa kufanya kwa sehemu tu ya taasisi hiyo, yaani kadhi.

Sheikh Mohamed pamoja na waislamu wote wenye nia ya kushinikiza serikali ikubali mahakama ya kadhi kuwa chombo cha dini kinachoendeshwa na serikali, naomba niwashauri kuwa, kama kweli mnapenda amani ya nchi hii, basi heshimuni dini nyingine na muanzishe hiyo mahakama bila ya kuihusisha serikali, kwa hata dini zingine zimeanzisha taasisi nyingi sana bila kuihusisha serikali, Hakuna sababu ya kuitumbukiza hii nchi katika malumbano yasiyo na msingi, nawaomba ndugu zangu waislamu...
tatizo nadhni ni wivu wa kidini, kwani kama sio wivu nini? kwani mnasema waislam ni ndugu zenu, rafiki zenu. inamaana ni rafiki wa maeno bila ya vitendo? unahofia fedha yako kutumiwa na rafikl yako> unaumia fedha yako kutumia ndugu yako? halafu unasema sio wivu wa kidini?
 
Wakristo hawatawaliwi na sheria bali neema. Paulo alishasema. Ila hawataki wenye kutii sheria wafanye hivyo, huu ndio wivu wa kidini' Wameenda mbali mpaka kukumbatia CDM ili kuhakikisha hili halitokei!
 
nashauri pia askofu mkuu wa kkkt achaguliwe na rais kumpa uwezo wa kuadibisha waumini wake katika masuala ya uadilifu, kuwajali wenye shida katika jamii (kama yatima na wajane) maana hiyo ndiyo ibada inayokubalika kwa mungu. Leo jamii ina watoto yatima na wa mitaani kwa vile maaskofu wamepoteza uwezo wa kuwabana washirika wao tena wengine wana uwezo mkubwa kuwajali yatima na wajane.

Tena napendekeza maaskofu walipwe mishahara na serkali kwani idara ya ustawi wa jamii imekuwa ikitekeleza majukumu yake vibaya huku maofisa wakilipwa mishahara na serkali.

Pia napendekeza sheria ya ndoa ya mwaka 1973 ifutwe kwani jamii yetu imegawanyika katika makundi mbali mbali ya imani na utamaduni. Wahaya wanazo taratibu zao tena za kale za kufunga ndoa. Waachiwe wafunge ndoa za kihaya, waislamu waachiwe ndoa zao wazifunge kupitia kadhi, wakristo nao wanao mwongozo wao kuhusu kufunga ndoa wautumie bila kulazimishwa na serkali kuweka mashahidi na kutangaza ndoa siku 21 ( maana vijana wengine wanawahi masomoni na ughaibuni hivyo wasibanwe na sheria hii). Kikristo ndoa lazima ihusishe wazazi (biblia husema mwanaume anatokea kwa wazazi wake kabla ya kuambatana na mkewe). Hivyo wakristo nao waendeshe ndoa kwa sheria zao. Tena wale wafungishaje na kamati zote za ndoa za makanisani zitambuliwe na kugharimiwa na serkali kuliko ambavyo afisa tawala (w) analipwa fedha nyingi na kuishia kufunga ndoa bila hata wazazi kujua. ( ananajisi imani huyu). N.k
wewe ulikuwa bingwa wa kudesa ukiwa shule, unadesa mpaka mambo ya dini!
 
Wakristo hawatawaliwi na sheria bali neema. Paulo alishasema. Ila hawataki wenye kutii sheria wafanye hivyo, huu ndio wivu wa kidini' Wameenda mbali mpaka kukumbatia CDM ili kuhakikisha hili halitokei!

Ulitaka wakumbatie cuf kama nyie?
 
Hivi kule kenya ambako waislam ni wachache (20%) so ndo walitakiwa wakatae kwa sana tu? Mbona wameona logic na ikawepo? Kule south Africa Je? nako ni waislam pekee au ni % ngapi? Na kwengineko kwingi, hebu angalieni kwenye mtandao mtaona. Je waislam ni % ngapi hapa Tz? Si zaidi ya 50%. Je wingi huo wote ni wakupuuzwa?
halafu pia wewe yaelekea ni kilaza wa hesabu, hebu cheki mfano wa mchanganuo huu hapa chini
hakimu1-----kesi za kawaida 20+za mambo ya waislam 5 ======25
hakimu2------ 20+ 5=======25
hakimu 3------ 20+ 5=======25
hakimu 4----- 20+ 5=======25
Hakimu5----- 20+ 5=======25
-----------------------------------------------------------------------------------
Total 100 + 25=======125

kama uwezo wa hakimu ni kuhukumu kesi 25 mathalani kwa mwezi na katika kesi hizo zipo 5 ambazo kadhi alitakiwa kuzitenda, why don't we have professional kuliko kuwa na mtu wakubahatisha mara awaite mashehe nini! ubabaishaji mtupu. Hivi mnasema eti na wakristo nao waanzishe zakwao, kwani wao wanasheria? kuna nchi ngaki zenye wakristo karibia wote nitajieni ni nchi gani inaongozwa kw sheria zake? nchi zenye waislam je? kenye mbona kuna mahakama ya kathi kwani nini kawaanzishi hizo za kikrsto tuzione? hawa si jirani zetu kwanini tusijifunze kutoka kwao?
Hivi kama wakoloni waliona ni muhimu kwa waislam kuwa na mahakama ya kadhi imekuwaje waTz wenzetu hawaoni umuhimu huo. NA SEMA HIVUI HUU NI UNAFIKI, NA NI WIVU WAKIDINI. PERIOD!

Kazi kwenu wenye kuzijua hesabu!

Hivi idadi ya hao Kadhi itakuwa kiasi gani?

Hesabu zako ni ngumu kwangu!
 
Katika hicho kipindi , mchangiaji mmoja alitukumbushia kuwa kwa Imani ya Kiislam ndoa na miradhi ni sehemu ya IBADA. Hivyo kwakuwa katiba imetoa uhuru wa kuabudu ni vyema mahakama ya Kadhi iruhusiwe kwani kutokuwepo ni kuingilia uhuru wa kuabudu.

Hapo kuna pointi; lakini natahadharisha pale tunapohalalisha matumizi ya pesa ya walipakodi katika hili. Je pesa ya walipakodi ikitumika kutimiza IBADA (kugharamia mambo ya ibada) kwa dini moja si na dini nyingine zitataka pesa yetu tena itumike kugharamia sehemu ya IBADA zao?

Wengine watasema haiwezekani lakini kwa haya mashindano ya Kidini tunayoshuhudia, mwenye akili apime na kuona!

TAFAKARI!

Nani atasimama kukatatae endapo dini nyingine zikitaka serikali igharamie IBADA zao? TAFAKARI
 
Tatizo letu ni unafiki,tungeweza kuanzisha wenyewe lkn tatizo tumegawanyika mno,bakwata hawezi kubali mawazo ya shura ya maimamu and viceversa achilia mbali kuheshimiana,tusaidieni jamani suala la ibada yetu ni mhimu

Msaada utaupata kwenye Furqan el karim Hadith ima sunna! hizo ni rejea tosha za Muumini na si Serkali! ambayo haikuanzisha uislamu!!
Tatizo ni viongozi wa Kiislamu wameshindwa kufuata miongozo Hiyo iliyo bainishwa ya kiislamu wameshindwa kuhamasisha waislamu kwenye njia ya Mungu wao hadi wanaomba Makafiri wawapangie ibada waumini! wamebaki sasa kufitinisha ndugu wagombane sijui kwa manufaa ya nani!;
Kama ulivyo sema wengi wao ni Wanafiki na wachumia tumbo tu Uislamu haupo rohoni bali kwenye kanzu bakora! Na ndevu.

TUTAFIKA?
 
Mbona kelee nyingi saana!
Waisilamu hebu semeni. nani kawakatalia kuanzisha mahakama yenu??
Si muianzishe, kwani mnasubiri nini?
Kwa nini mnataka kila kitu mfanyiwe hata pale ambapo haistahili? Kazi kulalamaa all the time!
 
Nadhani suala la msingi ni kufumua, kuunda na kuimarisha mfumo wa sheria, mahakama na upatikanaji haki Tz.

Naamini kama Tz itakuwa na mfumo mzuri wa sheria & mahakama, basi mashehe watakosa nguvu kudai mahakama ya kadhi. Pengine moja ya sababu ni kuwa wanaona tofauti katika hali ya mahakama za sheria Tz, ya kwao ingetoa haki zaidi kwa mambo yao kuliko mahakama za sheria.

Naungana na baadhi wachangiaji wenzangu. Mahakama ya kadhi si jambo zuri (la afya) katika nchi yenye watu wenye dini, mila, desturi, makabila nk tofauti.

I think Tz is a multi-racial nation. So I'm always sceptical when people start to see the subjective agendas and embark on pursuing them.
 
Salaam aleikhum
ndugu zangu waislamu inabidi tuwe makini sana kama jamaa alivyoshauri hapo juu. Kudai mambo bila kuangalia mbele hatutajenga na itatuharibia amani tuliokuwa nayo.
Sisi tunaamini ya kuwa maswala ya kadhi,mirathi ni moja ya ibada, na hapohapo tunataka serikali ighalimie ibada yetu. Je kamahela hiyo anaitoa mkristo ambae biashara yake ni kuuza nguruwe na sisi tunaamini kuwa kitimoto ni haramu,unafikiri ibada yetu itafanyika? Au kama hela hizo zitatoka kwa muisrael ambae sisi tunadhani anawaua ndugu zetu wa palestina na kuwanyonya je hapo ibada itakuwaje?
Nasema sisi waislamu bila unafiki tunamatatizo. Angalia nchi kama somalia ambayo ina waislamu watupu kuna matatizo kila kukicha. Angalia pakistani,afghanistani, yemeni,misri nk. Sasa tutawahakikishiaje wakristo kuwa tutakuwa na amani kama tutakuwa na mahakama yetu.
Waislamu wenyewe tu hatupendani: Ebu angalia ktk misikiti watu wanauana waumini wa dini moja na kudai kuwa tutakwenda ahera. Mfano ni kule pakistani. Utakuta ndugu zetu washia wanawaua wasuni na wasuni wanawaua wa shia sasa hapo utasemaje??
Mwaka jana ndugu zetu wengi wapikistani walikufa kutokana na mafuriko, je sisi waislamutulitoa mchango gani kwa hao waathirika? Waliotoa mchango mkubwa walikuwa hao ``makafiri`` wakati kunamatajiri wengi sana waislamu. Lakini kama wangeomba hela za misikiti, hao waarabu wangetoka bila hata kusita. Sasa hapo ndipo unapotofautiana na makafiri
kjitenga au kutafuta maslahi yetu sisi peke yetu waislamu haijengi chochote na tutauana wenyewe kwa wenyewe. Tutanza kuwabagua wakristo na baadae tutazidi kubaguana wenyewe kwa wenyewe. Sisi wenyewe hapa tz hatupendani na wenzetu wa ansal sunna, shia nk. Sasa tutaanzaje kuwabagua hayo madhehebu mengine!!
Unafiki mwingine unakuwa kwa sisi waislamu, kwa ninitukipata matatizo ktk nchi zetu tunakimbilia nchi za kikristo(ulaya,marekani) wakati tunajua kuwa hao jamaa ni ``kafiri`` kwa nini tusiende afganistani au somalia au sudani au hata saudi arabia kwenye chanzo cha uislamu? Mie naona sisi ni wanafiki (samahani)
masalaam
 
kwani si waanzishe hizo mahakama zao na wao wenyewe waislam waigharamie kuanzia majengo hadi mishahara ya hao mahakimu wao?
 
Asante mkuu tatizo la wenzetu ni kuwa wako very myopic na short sighted badala ya kufanya kazi za kiuchumi na kusoma ili kuondoa ujinga wao wanakazania marumbano yasiyokuwa na tija kwa nchi yetu!
wewe unaonekana umesoma saaaaaaaaana.
ila mbona bado una kiwango kikubwa sana cha ujinga.
shule na vidato sio ushahidi wa werevu wa mtu.
mbona waTZ kama wewe mko wengi kichizi..
 
Asante mkuu tatizo la wenzetu ni kuwa wako very myopic na short sighted badala ya kufanya kazi za kiuchumi na kusoma ili kuondoa ujinga wao wanakazania marumbano yasiyokuwa na tija kwa nchi yetu!

Mkuu Genekai..sipendezewi na matus yako kabisa, kuwaona waislam wapumbavu sio sahihi kabisa. Tujitahid kupunguza kutumia lugha kali mkuu, tutatengeneza chuki za kidini sizisosameheka.
 
Nilishawahi kuongea na Mzanzibari mmoja mwanamke ambaye kwao kuna hiyo mahakama. Yule mama alinielezea manung'uniko yake juu ya mahakama ya kadhi jinsi inavyodhurumu na kutoipenda kwake, maanake hata huko watu wanazunguka mbuyu na kumpa kidogo kadhi kitu ambacho kinasababisha haki kutokutendeka. Kwa hiyo kuanzisha hiyo mahakama ni kuongeza tu matatizo mengine.
 
Sheria za Tanzania zinafuata Katiba na si dini!!. Kama una taka sheria za dini nenda Saudi au Vatican kuishi huko.
 
Ianzishwe fedha sio tatizo sisi sote ni ndgu wa nchi moja...siyo vibaya tukiwalipa kadhi kutoka serikalini..maana itakuwa inahudumia jamii kubwa ya kiislamu

Muda na pesa zinazotumika sasa kwa kuhukumu kesi za waislamu (kwa man made laws) ndizo subsititute

Fanyeni utafiti tuwepe haki banadamu hasa za kidini ok.
 
Napata shida kuelewa kwanini ibada ya waislam ipewe mwongozo na kupata fedha kutoka kwa kafirs! Sasa kama waislam hawawezi kujiamulia mambo yao wenyewe mpaka wapate msaada wa kafirs, huoni kwamba hata hao waislam ni kafirs tu kwa namna moja au nyingine? Ina maana dini kubwa kama Islam inashindwa kuanzisha na kuendesha institute (ibada) ndogo kama hii ya kadhi?! Sasa wanachoweza ni nini?!
 
Back
Top Bottom