Sheikh Khalifa Khamis alalamika Waislam kuminywa na Serikali Kuu, TRA na Vyombo vya Dola

Hii nchi uwa imejaa wanafiki nyie sindiyo mlikuwa mnamshambulia JK kuwa ni mdini leo kipo wapi.
Kama kuna post niliwahi kuiweka hapa jukwaani ya kumtuhumu Rais wangu mpendwa na mstaafu wa awamu ya nne juu ya Udini, kwa heshima zote, naomba uiweke hapa hadharani. Watu wote waione, na kisha nitaomba Moderators wote washirikiane kunipiga ban ya miaka kumi kuchangia uzi wowote hapa jukwaani.
Sitanii...!!!
 
Hakuna kitu hapo.Hawa wana asili ya ulalamishi.Dawa yao ni kuwapuuza tu.

Hamna, inawezekana kabisa kwa sababu ya tabia ikawa wanafanya hivi kwa nia ya kuwa- harass marais wakristo, inawezekanaje wasikosoe hata siku moja akiwongoza rais mwislamu, hata kama kuna kosa la wazi, ila akishakuwa mkristo wanataka akose amani, wamwondoe kwenye reli kilalamishi hadi ishindikane kutawala!
 
-Kwani Vigezo Vinavyotangazwa kwenye nafasi za kazi Dini ipo? Mbona Utawala wa Nyerere alishawahi kuzushiwa hivyo hivyo ikabidi aangalie ni kweli,kuja kuchunguza akakuta wakristo wapo wawili tu yeye Nyerere na mtu mwingine,Ndugu Zangu Waislamu tufanye kazi kwa bidii,tujifunze sana,Ebu tuangalie stastistics kwenye Vyuo vyetu kuna waislamu wangapi na wakristo wangapi? Ukianza kuanzia Nursery-Primary-Secondary-chuo utaona kabisa idadi ya wakristo wanaosoma ni wengi kuliko waislamu,Huo ndio ukweli kwahiyo hata kwenye soko la ajira wakristo obvious watakuwa wengi...Kama umekata shule vizuri hauwezi ukanyimwa kazi eti kisa ni mkristo au muislamu,watu wanaangalia unajua nini.
 
Hawa waslamu bana.

Wao kila siku wanaona wanaonewa tu.

Kazi yao kulialia tu.

They need to grow up.

To grow up wakati masheikh wamewekwa ndani mwaka wa tatu Kwa kubambikizwa kesi Kwa kuwaamsha watu kuukataa muungano fake wa kivamizi
 
Huyu mzee inabidi wamshughulikie liwe fundisho na kwa wengine, Rais ana mambo mengi ya kufanya sio kuangalia usawa wa dini.
 
sheikh anahoji kwa nini TRA wanawasumbua,na akasema kama vipi,TRA ifungue ofisi misikitini wawe wanakusanya sadaka,

Teh! Teh! Teh! hizo sadaka zenyewe wanazo?. Ushauli wangu TRA na SERIKARI KUU kazeni buti misimaha ya kodi kwa mashirika ya dini ilitumiwa vibaya kama ilivyo kuwa kwenye misamaha ya kodi kwenye maduka ya jeshi.
 
Sheikh Khalifa naomba takwimu sahihi ya idadi na majina ya wakuu wa idara za Halmashauri 2015.Ziko idara 7 kila Halmashauri (daktari, mhandisi, kilimo/mifugo, elimu, mhazini, mipango na utawala ) kisha nipe Ma DC na Ma DED.
Kuhesabu wakristo na waislamu kwenye taasisi za serikari wanaweza, ila ukiwaambia wajihesabu wao wenyewe nchi nzima eti hawawezi wanataka usaidizi kutoka serikarini kwa kuweka kipengele cha dini kwenye sensa, hawa Extremist niwakushugulikia hivi TISS mko wapi?
 
Ukidhohofisha mmoja anaibuka mwingine. Sheikhe Ponda katulia, sasa kaibuka huy,, anajaribu kutafuna mfupa uliomshinda Sheikh Ponda
Mmh! Ponda kuacha si rahisi nafikiri kabadilisha sytle (nahisi anafanya underground movement na si za wazi tena).
 
Tanzania Tanzania Nakupenda,

Rais wa nchi anapofanya teuzi, yaani anatakiwa ;
1.Abalance dini,

2.Abalance kanda,

3.Abalance Jinsia,

4.Abalance mikoa,

5.Abalance makabila,

6.Abalance pande 2 za Muungano,

7.Alipe fadhila,

8.Inatakiwa ubalance makundi maalumu kama WALEMAVU,
--------------------------------------------------------------------------------------------------------
UKIFANYA BALANCE YOTE HAPO JUU,UTATEUA KILA MTANZANIA Maana mwingine asipokuwemo kwenye Teuzi basi kila utaporomoshewa LAWAMA za kufa mtu.

Muda huo huo anatakiwa atafute WACHAPAKAZI, Maana ukimteua mtu halafu baadaye ukamfukuza watakuona kama umemfukuza kwasababu ya dini yake -Utashikiwa bango wewe mbaguzi.

- Ukisema Uteue wanavyotaka na maendeleo yale wanatotaka watu yasionekane basi utaporomoshewa LUNDO LA LAWAMA kwamba umeshindwa kazi.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Kuna mambo mengine hata akiwa nani hawezi kufanya.Kuna MABILIONI YA IMANI ZA DINI Duniani lakini hii dini sijapata kuona , Dunia nzima .

Nice comment, ni kweli ukiteua kwa misingi ya kutazama dini, kanda, mkoa, kabila na madudu mengine chance ya kupata watendaji mizigo ni kubwa sana.
 
Ukombozi wa Fikra ni Muhimu sana kwa hao wanaopenda kulalamika, mimi sijaona katika nchi hii Sheria inayowabagua waislam hata kidogo, ni mambo ya uchochezi wa kijinga ambayo pia yamekuwa yakiwagharimu waislam sehemu nyingi duniani. Kikubwa ni kufanya maendeleo tu na tusiangalie lawama kama hizi kwani zitaingiza nchi katika machafuko. Tangu nchi hii imepata Uhuru waislam wao ni kulalamika tuuu hivi ni kweli mnaonewa au ni tabia tuu ya kulalamika lalamika?
Hao watu walianza kabla ya hata uhuru, kazi ni kujipambanisha na wakristo, ndio maana walitaka uhuru uchelewe mpaka pale watakapo kuwa sawa sawa na wakristo.

Udini na kelele zake unaletwa na kukuzwa na baadhi ya waislamu, Over!.
 
Utulivu na amani wa kikondoo usingewapa uhuru Zimbabwe Namibia Angola Namibia nk
Biase ya dini isiyo yake sasa ni dhahiri.
sheikh huyo amechanganyikiwa hayo magari ya bakwata yako wapi kama si mtu kaingiza kwa manufaa yake.viongozi wa dini wa aina hii wanastahili kupigwa vita kwani shetani amemtawala
 
Hakuna kitu hapo.Hawa wana asili ya ulalamishi.Dawa yao ni kuwapuuza tu.

Enzi ya kikwete nyinyi wala kiti moto mlikua midomo juu kulalama kuwa ni mdini anawapendelea waislam hadi makanisani mkaanza kupiga kampen za udini apewe Dr Slaa nchi mmesahau?

Ule siyo ulalamishi?au ni mapambio tuh yale
 
Namuheshimu Sana huyu sheikh,kuna mambo aliyoongea Ni kweli yanahitaji majibu lile la ma sheikh kama hawana ushahidi bora waachiwe tu
I feel sorry for their families
 
Sijui mnatupeleka wapi?Itafika wakati timu za michezo zikichaguliwa tutauliza mbona timu haina waisalamu ni wakristo watupu!!! Baada ya hapo tutaacha hata kusalimiana. Tatizo la waisilamu hata wasomi baada ya kukemea vitu kama hivyo, wanaunga mkono madai ya kijinga. Ndiyo maana nasema tukichagua wachezaji wa timu ya taifa tu hakikishe waisilamu na wakristo wanalingana sio ubora wa mchezaji. Hizi dini tuliletewa, tusifarakane Utanzania kwanza.
Na kwanini timu iwe na wachezaji wa kanda moja... ilhali kanda nyingine wapo wachezaji katika idara zote...!?
 
Hawa hawana shida....ni utukutu wa kitoto tuu...ukiwachapa viboko vitatu wanatulia.
Usijidanganye!
Mkoloni anajua Waislamu ni akina nani!
Mkoloni anamjua Sheikh Mkwawa
Mkoloni anamjua sheikh Kinjekitile
Mkoloni anamjua sheikh Abushiri
Mkoloni anamjua Sheikh Mwinyikheri
Mkoloni anawajua waliounda TANU na kumuweka kijana wao Nyerere alisongeshe!
Never play with Muslims if they decide to deal with any issue of injustice, you can't stop and no one can!
 
Hivi makamo wa rais mkristo, waziri mkuu nae mkristo, kuna mawaziri na wakuu wa mikoa/wilaya wangap wakristo, kuna wakurugenz na makatibu tawala wote ni wakristo? Awamu iliyopita rais alkuwa muislam mwenzenu mkasema anapendelea wakristo, enzi za mkapa pia mlisema mnabaguliwa, now mnasema mnabaguliwa.

Wakat mwingine waislam wanaonewa ila kwanini waonewe wao kila siku?
Je viongozi wanachaguliwa/kuteuliwa kwa kuangalia kigezo cha Dini tu ama elimu, uzoefu na uwezo wa mhusika?

Mara ngap watu wanakamatwa kwa tuhuma za ugaidi? Je wanaokamatwa kwa tuhuma za ugaidi ni dini gan?

Mimi kama mkristo ninaamini kuwa uislam ni dini safi ila kuna watu wanaitumia vibaya kufanikisha malengo yao.
 
Thread kama hizi ni kwa ajili ya kuanganisha nyumbu wa ufipa na wakatoliki wa CCM kuwa kitu kimoja wengine hazituhusu kabisaa.
 
huyu bora angekuwa kama yule mwezake hapa jf yy anadili na mambo ya majini ti
 
Back
Top Bottom