SHAMBULIO LA RAIA DHIDI YA AFISA WA POLISI

skfull

JF-Expert Member
Dec 24, 2013
2,944
2,376
Wa jamvi habari za jioni hii; Kwanza nashukuru sikukuu ya idd imeisha salama salimini..
Naomba nianze na kastory kakweli halafu nitapenda ushari wa kisheria na mengineyo,,
Ilikuwa ni juzi j3 ya tarehe 20 nikiwa katika utafutaji wangu wa mkate wa watoto wangu,, Mimi ni Dereva,, siku hiyo ya j3 nikiwa natokea Gerezani kwenda Chanika,, kwa mtu anaeishi Dar es salaam, hususani mwenye kutumia barabara za Uhuru, nyerere na Mandela siku hiyo ya j3 ilikuwa hazipitiki kwa foleni ya maana hasa mida ya saa 12 jioni kwenda mpaka saa mbili usiku,,
Sasa wakati nikiwa maeneo ya Rozana pale buguruni,, nilikuwa kwenye foleni Mara ghafla gari zikaanza kutembea eneo nililokuepo lilikuwa eneo la U turn kwa madereva wanelewa ni sehemu ya namna gani sasa wakati nipo pale wakati nataka kuanza kuondoa gari ghafla ikatokea gari kushoto kwangu na ikaja na kutaka kulazimisha kupenye na kwenda upande wa pili yaani kutoka kushoto kwenda kulia lengo lake ni kuelekea Amana,,, basi bahati iliyo mbaya akawa amefanya maamuzi wakati namimi nishafanya maamuzi ya kusogea mbele kufuata foleni,, ikatokea kugongana japo ni kama kugusana maana hakuna gari iliokuwa na kasi hata moja japo yeye wa gari nyingine alitumia mafuta mengi ili anizidi hatua,,
Baada ya kugongana kule nikashangaa wakishuka watu wawili kwenye gari ile na mmoja akiwa na panga mkononi wakaja usawa wa mlango wa gari yangu na kuanza kunilazimisha kushuka kwenye gari,, kiukweli nilikataa cjakataa kwasababu ya ujeuri au uoga lah nilikataa ili kumpisha shetani ambae alikuwa amewavaa wale watu,,, baada ya mda kidogo mmoja wao akaenda mbele ya gari yangu akiwa na panga akaanza kufanya juhudi za kung'oa namba ya usajili wa gari ninayo iendesha mimi,, uvumilivu ukaniisha maana kwanza siwajui wale watu pili sijui lengo lao hasa,, nikaamua kushuka niliposhuka sikufika upande wa mbele wa gari yangu nilijikuta nachezea kichapo cha maana halafu wakawa wanataka kuniingiza kwenye gari yao, ikabidi ni vimbe hasa kuvimba kule kukaendelea kunipa kipigo na baada ya muda mfupi RAIA walikuja wengi sana na kuwashambulia wale watu kwa maneno ya kuwashangaa kunishambulia huku wameshika panga na sababu nikiwa ni ajali ya Magari kusuguana kidogo,, basi watu wakawaweka kati yule mmoja akaficha panga wakadai Mimi ndiye ninayewashambulia ndipo mmoja akajitambulisha nakudai yeye ni afisa wa polisi,, lakini hakutoa kitambulisho wananchi wakakataa na wakati huo Mimi nimemkwida maana Dereva wake alishampa ishara nikagundua wanataka kukimbia,, wanataka nimuachie nikamwambia sikuachii mpaka afisa wa polisi usalama barabarani afike pale halafu akishapima ajali tuelekee kituoni,,,
Wakati hayo yote yanaendelea, kondakta wangu alikimbilia polisi kuwaita,, na baadae akampata mmoja akafika nae pale, akatuamuru kuachiana na tumfuate kwenda kituo cha polisi Buguruni,, tulipofika pale yule bwana aliejitambulisha kama afisa wa polisi akaongea sana sikupewa nafasi ya kujieleza,, nikauliza mbona mnamsikiliza mtu mmoja tuu anaongea sana na kurudia rudia taarifa? Mkuu wa kituo cha polisi Buguruni akaniambia nieleze lakini kila ninapoeleza yule bwana anaingilia kati maelezo yangu,, nikaambiwa nitoke nikasubiri kaunta,, na wakajifungia ndani ya ofisi ya mkuu wa kituo,, na baada ya muda kupita wakatoka na kuelekea nje wakati huo Mimi naamriwa nivue viatu niingie sero.. Nikashangaa maana kwenye maelezo ya yule bwana aliejiita afisa aalikiri kuwa kweli Mimi nimeshambuliwa lakini alienishambulia ni Dereva wake, sasa nikajiuliza kama ushahidi upo kuwa nimeshambuliwa kwa mujibu wa mtoa taarifa sasa kwanini Mimi ndiye niingie sero? Niliwaambia polisi pale mapokezi kuwa nataka nifungue mashtaka ya kushambuliwa maana nilipotelewa na vitu vyangu pamoja na kujeruhiwa sana zaidi jicho langu lakini walichoniambia ni kwamba lazima nimwambie mkuu wa kituo na wakati huo mkuu wa kituo yupo beneti na mhalifu wangu, Hapo nikachoka kabisa nikalala na kushinda pale nikaja kutolewa usiku wa saa moja siku iliyofuata,, je naweza fuata hatua gani ili kuwaadabisha watu hawa nikiwa ni pamoja na kumuadabisha mkuu wa kituo cha polisi husika? Natakiwa kuripoti tarehe 23 yaani alhamic, naombeni ushauri wa kunifaa,, kejeli hazinifai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom