Shadow circuit inaua kwa haraka kuliko mbinu yoyote ya kijasusi

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
879
4,125
Tanzania inaishi kwenye shadow circuit development dilemma; mfumo ambao huna uwezo wa kuweka akiba kwa ajili ya kuendesha serikali bali unatumia makusanyo ya mwezi au kipindi flani kulipa salary na mambo mengine.

Ukitaka kufanya jambo lolote la maendeleo lazima ukakope. Unaweza ukakopesheka lakini majasusi wa kiuchumi wakigundua umefilisika wanakupa mkopo kwa masharti ya mkataba wa kubadilishana na rasilimali wanayohitaji.

Utaona waziri wa fedha kila siku anatangaza mikopo baada ya kusainiwa mikataba aidha ya utafiti au yakuendesha sekta flani nyeti inayogusa wananchi. Utagundua kila mkopo tunatajiwa kiasi kwenye TV means wakopeshaji wanaweka kumbukumbu sawa endapo atajitokeza mwanasiasa huko mbele kuwapinga

Hii shadow circuit ubaya wake nikikukufanya uwe mtumwa wa kukopa na mtumwa wakufunga RAIA wako wanaopiga kelele. Mwekezaji akisema wananchi wananipigia kelele wewe kazi yako nikuwanyamazisha kwa dola. In long run wananchi watakuta hata sekta ya ulinzi mifumo yake yote ikiwemo ya TEHAMA inatengenezwa na kusimamiwa na wageni. Means mifumo ya TEHAMA ikiwa chini ya wageni mnabaki na nini.......means you are finished.

Ukikooa wanajua, ikilia wanajua , ukicheka wanajua. Haya yote yanapelekea nchi kukosa uwezo wakuamua mambo yake. Inafika wakati wawekezaji wakifanya mgomo baridi hata mapato ya kulipa bills na salaries utakosa. Kukosa kwako ni neema kwao kwa sababu wataomba uzidi kuwamegea nchi maeneo yaliyobaki.

Shortly tunapaswa kufanya analysis mapema kuhusu nguvu ya watanzania kwenye uchumi wetu against nguvu ya hawa tunaowapa thamani. Contrary kwa namna uzalendo unavyoshuka na tulivyotengeza CHAWA nchi inakwenda kutawaliwa.
 
Big point...

Hata haya mambo ya wawekezaji wa nje wakubwa sana sio sahihi....wakiwa Ellites siku za mbeleni wanaweza kusema tunatoa uwekezaji wetu mwisho uchumi unayumba assume unakuwa na kina bakhresa km 10 nchini

Ndio maana china,russia,iran wanajitahidi kutoa ruzuku kwa wazawa ili hili lisitokee au kulazimisha share holder wawepo juu wazawa
 
Back
Top Bottom