Sh 5,000 inaweza kabisa kunitoa kimaisha!

Kuna mtu amependekeza kuanza biashara kwa sh 5000, kama kawaida waungawana humu jf wamedai apeleke huo uzi wake joke forum. Lakini mie nna mtazamo tofauti hapa. Kwamba bado hiyo elfu tano inaweza kukutoa kabisa kama kweli uko serious. kwa namna gani inaweza kukutoa, hebu fuatilia hapa chini:

Nimeamua kufanya biashara ya kuuza juisi ya matunda.

Mananasi 2 sh 2000
Parachichi 2, sh 1500
Sukari robo 1000
Jumla 4,500

Baada ya kuitengeneza zitatoka walau lita tano, ambazo kwa kiwango cha chini, ntapata jumla ya glass zisizopungua 15. Kwa bei ya gsh 500 kwa glass moja, ikiisha ntapata jumla ya sh 7500.

Kumbuka hapo nimemaliza chuo, bado mie ni mtu wa kula kulala-yaani nakaa geto. Nimeshatengeneza faida ya shi 3000, kwa siku. Hii ina maana kama ni ajira basi nalipwa 90,000 kwa mwezi. Hivi ntalala njaa kweli nikiamua kuwa serious na hii bishara?

Hivi kwa hesabu ndogo kama hii, kuna haja kweli ya mtu kulia njaa jamani. Mi nadhani kinachotusumbua wengi ni kale katabia kwamba hiyo kazi ni ya kufanywa na mtu ambaye hana shule, lakini hela haina shule, na sioni kama hapo kuna kudhalilika kwa aina yeyote. Jamani, let us start from the scratch kama hatuna mbadala wa aina yeyote ktk ajira zetu.

Tanzania hii kila kitu kinawezekana, sio ufisadi pekee tu!

Hiyo Sh5000 ni Tsh au Ksh?
 
Kwanza naomba nimshukuru muanzisha maada.
Nilichokiona mimi katika hii thread,
Wachangiaji wengi si wafanyabiashara/wajasiriamali halisi kwani wanashindwa kuelewa hali halis ya kinachotokea huku site. Na kama ni wafanyabiashara basi wengi hawakuanza na hizi biashara ndogo, hivyo uwelewa wao wa hizi biashara ndogo ndogo bado ni mdogo. Kati ya biashara nilizoanza nazo mimi ni hii ya juice na barafu, tena nikiwa darasa la tano. Hivyo ninaielewa vizuri, tena kipindi hicho hatukuwa na fridge wala umeme nyumbani, lakini niliimudu na ilinipeleka mbali sana.

Wachangiaji wengine ni good motivators "go get it", "you can make it"...(na ni watu muhimu sana). Hii ni factor nzuri sana kwenye ujasiriamali lakini bado haibadilishi nyekundu kuwa njano. (kama mtu hana mtaji)

Wachangiaji wengine ni wale wafanyabiashara/wajasiriamali halisi. Au wafanyabiashara waliopitia biashara ndogondogo na wanajua what it takes kufanikiwa (kutoka) katika biashara ndogo, waliojitolea kuongea hali halisi hata kama watapingwa, au wataonekana kama wanawakatisha watu wengine tamaa (ni vizuri kuwaambia watu huku site kuna nini).

Mimi nimalize kwa kusema zipo biashara ambazo unaweza ukazifanya hata kama huna cash (sizungumzii mtaji) na ukafanikiwa pia. Kwa mfano mtu mwenye Social Capital nzuri anaweza akawa anachukua bidhaa kwa supplier na kuziuza pia. Kuamini ni kitu kimoja na kuwa motivated ni kitu kimoja, lakin kutenda ni kitu kingine. Kwa ambaye anaamini anaweza akafanya hizo biashara kwa mtaji huo tunamkaribisha site. Na kwa wale ambao wanaamini kuwa mtaji huo unatosha lakini hawana kiasi hicho najitolea kumpatia Ndyoko dollar 200 ili awapatie vijana 64 kwa minajili ya kurudishiwa baada ya mwaka mmoja bila riba yoyote. Nafanya hivi kwa moyo wa dhati kabisa nikiamini Bw. Ndyoko utakubali kuwadhamini vijana hao kwa namna tutakavyokubaliana. I real need those boys in need, those boys who want to better themselves but tatizo ni elfu 5

if it cost 3$ to establish a job you need $ 60 million to for 20 million jobs
. Sioni ni kwa nini vijana wa Kitanzania wazidi kulalamikia suala la ukosefu wa ajira. Shukrani kwa mkuu LAT kwa namna ulivyokuwa real, MALILA, NEWAZZ na WHO CARES kwa namna mlivyotoa motivation.
 
Je kwa asiyekua KKB(Kulakulala Kwa Baba)?

Maisha yana options nyingi sana, na ndiiyo maana nilikwambia jaribu kufikiria nje ya sanduku. Unaona sasa walau umeongea something sensible. Na huko ndo kuwaza kwenyewe nje ya boksi mkuu. Hapo ni wewe na mimi sasa tujadili itakuwaje kwa mtu ambaye sio kula kulala, kumbe sometime akili zako huwa na akili!
 
Mimi nina mfano halisi wa mtu ninayemfahamu ambaye alianza biashara kwa kiwango chini ya hicho miaka minne iliyopita. Yeye alianza kufanya biashara ya kuuza vipande vya sukari guru, Yaani ananunua kilo moja ya sukari guru then anaikata kata vipande vidogo vidogo na kuiuza. Alianza na mtaji wa Tsh 4,000 na siku ya kwanza kuanza biashara alipata jumla ya mauzo ya tsh 11,200 hivyo faida ya shilingi 7,200. Leo hii ana mtaji mkubwa katika biashara zake, kwa hiyo siyo kweli kwamba huwezi kuanzisha biashara kwa kiwango kidogo sana cha mtaji. Binadamu wanatofautiana pengine wewe unadhani milioni mia tano ndio inatosha kufanyia biashara lakini kwa mwingine kiwango hicho ni kidogo sana na hakuna biashara yoyote anayoweza kuifanya kulingana na hadhi yake.

Unajua watu wanashindwa kuelewa lazima hapa tufahamishane,kuna watu wanasema kuwa wanawafahamu watu wametoka kutokana na hiyo elfu tano halafu wanaanza kutukokotolea mahesabu feki hapa,mwingine anasema atafanya atafuga kuku awazalishe chakula hanunui,hawatakufa kwa magonjwa,hawataibiwa,vicheche hawatawagusa na blabla nyingi za kufikirika,mie napenda kusema hivi unapomwona mtu alikua anauza karanga,machungwa au barafu leo kajeuka kua bharesa lazima kuna mahali kapiga panga ndio akatokea hapo.Wewe ambaye ulimwona yule mtu alikua anauza barafu na kidumu leo yuko na prado eti unaanza kuzani kuwa ni ile biashara aliyokua anafanya akafika hapo,watu wengine mchana anauza machungwa usiku kibaka jambazi you never know?kwa sababu wewe hauko nae wakati wote kumbe amepata fedha za hujma akafanya kitu kikubwa we unaanza kuwazia ile elfu tano ndio imemtoa,unafikiri yeye atakuambia zari amelipata wapi?

Mfano wa jamaa mmoja anaitwa Reginald Mengi anakuambia utajiri wake umeanzia kwenye sijui kuuza kalamu leo ni bilionea zari kalipata wapi la kuinuka,kaipiga NBC sawasawa twende kwenye NICO kaianzisha kakusanya elfu tanotano zenu kawabwaga,we unabaki kutoa mfano hata mengi alianzia chini,naombeni wakuu mnaoona elfu tano itawatoa muwe na mawazo mapana zaidi.
 
Hii thread imenihamasisha sana leo na nijutia kwa nini wakati mwingine hua napoteza muda kwenye majukwaa ya Chitchat na MMU, mimi ni mfano mzuri na historia ya jamaa mmoja..
Alianza ujasirialmali akiwa darasa la tano, anasema alikua anabeba Big G, Pipi na Ubuyu akawa anauza Darasabi na kipindi hicho alikua darasa la nne, anasema anamaliza darasa la saba alikuwa tayari ameanza Unga wa Mahindi, Maharage na mboga mboga kwa mama Ntilie kuzunguka eneo la shule maana kulikua na watu wengi ambao walikua wapo around na lile eneo la shule, akaendelea kupata tenda sehemu zaidi ya 8 kwa siku akajikuta anasambaza Unga hata kilo mia 300, na maharage kilo 30-50 kwa siku, sitaandika yote lakini mpaka sasa Jamaa anakaa Kuwait, na makao yake mara nyingi ni Cape town, Kuwait na nchi za UAE.. hapa Dar es salaam ana kampuni za kufyatua matofali, Magari ya kubeba mizigo kwenda nchi za jiranii...
Hebu piga hesabu jamaa alikoanzia.. kwa hiyo kila kitu ni Kuthubutu...
TO DARE IS TO DO.
 
Ndugu mtoa mada uko sahihi kabisa. Tatizo letu sisi watanzania hatupendi kuanzia chini. Wazo lako ni zuri sana.
Mie mwenyewe nilianza kabiashara kwa mtaji mdogo sana wakati nasoma A-level, sikuwa na mtu wa kunilipia ada ila kuna msamaria alinisaidia niishi kwake. Mie nilianza hii biashara kwa shida. Mie nilianza biashara ya kuuza maji ya kunywa majumbani
Kwa sababu tulikuwa tunaishi nyumba za polisi maji ya bomba yalikuwa ya bure. Mimi nilitafuta hela ya kununulia kuni ili niwe nayachemsha maji na baadae nayauza. nilianza kwa kununua kuni za sh 1500 ambazo zilitosha kuchemsha maji yaliyotoa lita 100 (at least) na dumu moja la lita 20 nilikua nauza sh 800. Na kwa sababu maji salama ya kunywa lilikuwa ni tatizo pale mtaani nilipata wateja sana na wengi walipojua nikawa nauza maji kwa order. Kwa sababu nilikuwa nyumbani kwa mtu aliyekuwa na masufuria makubwa matatu nilimwomba niyatumie kuchemshia maji. Kila siku nilikuwa nauza sh 4000 najikuta faida ni sh 2000 au 2500 coz gharama ilikuwa ya kununua kuni tu na hata km ningekuwa nanunua maji bei ya ndoo ilikua ni sh 20 tu bado faida ilikuwepo. kwa hiyo sikulalamika kuhusu ukosefu wa nauli, japo nilikuwa napata shida kuchemsha hayo maji
Jamani tuacheni kulalamika tufanye kazi kwa kujituma. Tuachane na story za utajiri wa haraka ndugu zangu
 
WAKUU MIMI SIONI TATIZO KABISA KWA MTOA MAADA HAPO JUU, HIYO BUKU TANO INATOSHA NA INAWEZA BAKI,

- WAKUU KUNA KITU KINAITWA BUSINESS STRATEGIES, NA HIVYO VYOTE MNAVYO MUULIZA NAULI, MASHINE NA KAZALIKA VIKO KWENYE BUSINESS STRATEGIES ZAKE.

Wakuu mimi huwa na soma sana historia za makampuni makubwa sana Duniani, na mengi ya hayo makampuni yalianza na mitaji midogo sana na leo hii ni moja ya bland kubwa za dunia,

WAKUU LABUDA TUULIZANE HILI SWALI.

1. Je ni kiasi gani cha fedha kipo maalumu kwa ajiri ya baishara?

2. Kuna kiasi maalumu wa kuanzishia aina yoyote ile ya baishara?

Ninavyo jua mimi hata ukipewa sh 1000 ukaweza kutengeneza sh 200 kutoka kwenye hiyo elfu 1000 ni strategies nzuri sana.

Na mkuu amejaribu kuorodhesha vitu vyake pale chini, na watu wamemcrash sana kwamba haiwezakani labuda ya kenya au Dolla, Ninacho weza kusema kwa real entrepreners hiyo elfu 5000 inatosha kabisa na kwa mtu ambaye ni mfanya biashara tu hiyo elfu 5 haitoshi kabisa.

Entrepreners anaweza tengeneza pesa ya kutosha kutoka hiyo buku 5 ila kwa business man haiwezekani kabisa na ni ndoto na watu wengi wanao pinga hii kitu watakuwa na wafanya biashara na si wajasirimali.

KWA NINI KWA MJASIRIAMALI INATOSHA?

1. Entrepreners si profit oriented so utaona kwamba inawezekana, mtoa maada hajajikita kwenye faida bali kutengeneza product

2. Entrepreners anakuja na uniq aidea yake, mtoa maada kaja na wazo la buku tano kutosha na ni kweli inaweza mtosha

3. Entrepreners huyatoa maisha yake yote katika biashara yake, so mtoa maada anaweza tembea kwa mguu kwenda sokoni kununua product bila hata kupanda gari kwa sababu maisha yake yote yako katika biashara hana muda wa kwenda kusalimia shangazi na mjomba

4. Ni inovative and revulutionary, hapa si kwenye product tu hata jinsi ya kucheza na cost

5. Ni risk taker tena calculated one, bila kuwa risk taker hiyo buku 5 si chochote

6. Mjasirimal ni kiongozi wa masoko

7. Entrepreners puts his own money first,
yeye anaanza na kile alicho nacho hasubiri mikopo na mashindano ya kuandika business planing, so mtoa maada anaweza kuwa mjasirimali kwa sababu ameanza na kile alicho nacho

Entrepreneurship is not an easy feat compare to merely doing business. We can also realize that an entrepreneur is a business person who has evolved into a more complete person – one that is not simply a business person but a real human being. Being a businessman is good. Being profit oriented, market player, business competitor, traditional, busy and active income earner is not bad since all business owners have been on those stages. Even the successful entrepreneurs, before they succeed, have been into that. It is just that they have taken the right move to evolve into a better and even the best businessmen that they can be. That is why they become not only businessmen, but rightfully they become entrepreneurs. So, how about you? Are you a businessman or an entrepreneur? Are you merely doing business or are you taking it into a higher level, which is called entrepreneurship?
 
yaa, its true, mie na agree! tena kipato kinaweza kuongezeka kwa haraka sana ikiwa hiyo 7500 utakayopata uta invest tena kununua matunda mengine kwa siku inayofuata, na faida unayopata uzidi kuwekeza tena na tena na tena. matokeo yake utakuta unajilipa 10 to 20 thouthands kwa siku, utawazidi wafanyakazi wengi sana wa serikali!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kweli unaweza ukafanikiwa but utachelewa sana. Lakini NDYOKO mbona umepigia mahesabu ya hizo raw materials tu na si vitendea kazi? Kwa mfano Blender? Kisu? Fridge/Ice Blocks?, Dumu?, Glass?, Usafiri (to/from Sokoni), Sufuria, Boiled water (mkaa, jiko, maji n.k). Hiyo 5000 labla itatosha kama utakuwa umeshajipanga, kwani hiyo biashara si rahisi namna hiyo
Biashara utaifanyia Stand ambako Mgambo wa Site available every time so andaa Buku 5 ya kuwahonga!!!
Hiyo biashara bora uuze ubuyu!!
 
Unaweza kabisa, mimi nilianza kuuza juisi ya miwa bila hata senti tano, kila kitu nilikopa. Hata nauli ya kwenda kuchukulia mashine niliyoikopa niliikopa. Sasa mambo swafi kabisa, nyumba kibao. watoto wanasoma akademi, ma hg wakiomba 200 nawapa buku 10.
 
teh teh teh

ulikopa sh. ngapi?

je mkopo siyo mtaji?

kazi kweli kweli
 
peleka ****** huko. Unatulete nadharia za nchi ya kusadikika? Kwamba other things constant, we unazalisha na kuuza tu

NB: hapo juu kumbe upu.uzi tusi?
 
unga wa ngano kilo 1.5 sh 2300
mafuta ya kula chupa sh 1000
chumvi sh 200
mkaa sh 1000
unapata chapati 30
nauli kwenda na kurudi posta 1200
utauza kila chapati sh 250 - 300 (7500 - 9000)
ni biashara ya muda mfupi ikifika saa nne umeisharudi, unaweza pia usiende mbali ukatembeza nyumba kwa nyumba au kupeleka dukani au hotelini kwa oda jioni ukapewa hela yako
Jamani kila kitu kinawezekana!
 
Unachosema kina ukweli Mama Joe, lakin mchanganuo wako unapaswa kuonyesha na matumizi yako binafsi kutokana na kipato chako. Hakuna suala la kuzalisha na kuuza tu. Mpaka ufanye hivyo ndio tutaweza kuhitimisha kama biashara yako itafanikiwa nawe utatoka.
 
peleka ****** huko. Unatulete nadharia za nchi ya kusadikika? Kwamba other things constant, we unazalisha na kuuza tu

...
Tatizo michanganuo mingi ya watu inaonyesha mapato tu halafu haionyeshi matumizi. Mchanganuo mzuri lazima uonyeshe mapato na matumizi, ili tuweze kutambua kama biashara itafanikiwa na huyo mfanyabiashara atafanikiwa pia. Hayo ndi mapungufu ninayoyaona
 
Kweli unaweza ukafanikiwa but utachelewa sana. Lakini NDYOKO mbona umepigia mahesabu ya hizo raw materials tu na si vitendea kazi? Kwa mfano Blender? Kisu? Fridge/Ice Blocks?, Dumu?, Glass?, Usafiri (to/from Sokoni), Sufuria, Boiled water (mkaa, jiko, maji n.k). Hiyo 5000 labla itatosha kama utakuwa umeshajipanga, kwani hiyo biashara si rahisi namna hiyo

haya mimi nataka nitoke kwa tsh. 5,000/=. mchanganuo ni kama ifuatavyo.

Nitafanya biashara ya mchicha na spinach/chinees. nitaziuza kilimahewa stend eneo ambalo wengi wanashuka kwa kasi. Kwa biashara hii, nitakuwa naenda kuchukua bidhaa yangu kwa mkulima moja kwa moja.
1. Chinees 15 kwa sh. 200/- bei ya jumla. nitoa fungu 3 kila moja ikiwa na chinees 5. nitauza kwa tsh 200/- kwa fungu moja nitatengeneza 400 faida. faida itazidi mtaji.

kwa hiyo ukichukua 5,000/200= 25.
fungu 25 za jumla zitaleta fungu 25*3=75
75*200=15,000/=

kwa mapato hayo kwa siku, natengeneza 10,000 kama faida. kwa mwezi 300,000/= nadhani kula, kupanga chumba na sebule nitaweza. baada ya miaka miwili nanunu kiwanja na kujenga chumba kimoja kwanza, nahamia kwangu
 
WAKUU MIMI SIONI TATIZO KABISA KWA MTOA MAADA HAPO JUU, HIYO BUKU TANO INATOSHA NA INAWEZA BAKI,

- WAKUU KUNA KITU KINAITWA BUSINESS STRATEGIES, NA HIVYO VYOTE MNAVYO MUULIZA NAULI, MASHINE NA KAZALIKA VIKO KWENYE BUSINESS STRATEGIES ZAKE.

Wakuu mimi huwa na soma sana historia za makampuni makubwa sana Duniani, na mengi ya hayo makampuni yalianza na mitaji midogo sana na leo hii ni moja ya bland kubwa za dunia,

WAKUU LABUDA TUULIZANE HILI SWALI.

1. Je ni kiasi gani cha fedha kipo maalumu kwa ajiri ya baishara?

2. Kuna kiasi maalumu wa kuanzishia aina yoyote ile ya baishara?

Ninavyo jua mimi hata ukipewa sh 1000 ukaweza kutengeneza sh 200 kutoka kwenye hiyo elfu 1000 ni strategies nzuri sana.

Na mkuu amejaribu kuorodhesha vitu vyake pale chini, na watu wamemcrash sana kwamba haiwezakani labuda ya kenya au Dolla, Ninacho weza kusema kwa real entrepreners hiyo elfu 5000 inatosha kabisa na kwa mtu ambaye ni mfanya biashara tu hiyo elfu 5 haitoshi kabisa.

Entrepreners anaweza tengeneza pesa ya kutosha kutoka hiyo buku 5 ila kwa business man haiwezekani kabisa na ni ndoto na watu wengi wanao pinga hii kitu watakuwa na wafanya biashara na si wajasirimali.

KWA NINI KWA MJASIRIAMALI INATOSHA?

1. Entrepreners si profit oriented so utaona kwamba inawezekana, mtoa maada hajajikita kwenye faida bali kutengeneza product

2. Entrepreners anakuja na uniq aidea yake, mtoa maada kaja na wazo la buku tano kutosha na ni kweli inaweza mtosha

3. Entrepreners huyatoa maisha yake yote katika biashara yake, so mtoa maada anaweza tembea kwa mguu kwenda sokoni kununua product bila hata kupanda gari kwa sababu maisha yake yote yako katika biashara hana muda wa kwenda kusalimia shangazi na mjomba

4. Ni inovative and revulutionary, hapa si kwenye product tu hata jinsi ya kucheza na cost

5. Ni risk taker tena calculated one, bila kuwa risk taker hiyo buku 5 si chochote

6. Mjasirimal ni kiongozi wa masoko

7. Entrepreners puts his own money first,
yeye anaanza na kile alicho nacho hasubiri mikopo na mashindano ya kuandika business planing, so mtoa maada anaweza kuwa mjasirimali kwa sababu ameanza na kile alicho nacho

Entrepreneurship is not an easy feat compare to merely doing business. We can also realize that an entrepreneur is a business person who has evolved into a more complete person – one that is not simply a business person but a real human being. Being a businessman is good. Being profit oriented, market player, business competitor, traditional, busy and active income earner is not bad since all business owners have been on those stages. Even the successful entrepreneurs, before they succeed, have been into that. It is just that they have taken the right move to evolve into a better and even the best businessmen that they can be. That is why they become not only businessmen, but rightfully they become entrepreneurs. So, how about you? Are you a businessman or an entrepreneur? Are you merely doing business or are you taking it into a higher level, which is called entrepreneurship?

Unachokiongea KOMMANDO kina ukweli ndio maana nimekugingea like (BUT hapo kwenye RED unapingana na title, kwani jamaa anataka kutoka), lakini umebase kwenye lecture zaidi ya hali halisi inayotokea site (soma saiti). Wakati nafanya mafunzo ya ujasiriamali hayo maneno niliyasikia sana, but ukimtizama mkufunzi anayekufundisha utagundua haamini anachokisema au hajui hali halisi ya site.

Sasa kwa kuwa wengine tulikuwa ni watu wa Site kwa muda mrefu tulikuwa na advantage kidogo ya kuwasumbua walimu wetu, ingawa nilijifunza mengi lakin vitu vingi nilivyotegemea kuvipata sikuvipata. Ni suala hili ndilo lililonifanya nitafute Mentor, ambaye yupo juu zaidi yangu ili nijifunze mambo halisi ya Site through what they call Tacit knowledge. Elimu hii haina cheti, lakin mchango wake kwa mtu yeyote ni mkubwa sana, nadhani ndio maaa watanzania wenye Asili ya Asia wanafanikiwa sana.

Mambo mengi ambayo sikuyapata darasani, niliyapata Site kwa Mentor wangu na baada yakuona nimekubuhu aliniacha niendelee na biashara zangu. Mambo niliyojifunza huko site ni tofauti sana na ya darasani, na ndio ninayokutana kila siku kwenye ujasiriamali wangu, hivyo naweza kukabiliana nayo. (Mpaka nilipata wazo la kuanzisha darasa litakalokuwa facilitated na real entrepreneurs, na litakuwa promoted na hii slogan WHAT IS NOT TAUGHT IN BUSINESS SCHOOL).

Nakumbuka wakati huo ninasomea ujasiriamali, tulikuwa tunafundishwa kwamba, fedha si chochote kwa mjasiriamali halisi, kama ulivyosema wewe na kweli nakubaliana na hilo kwa kiasi fulani, na hapa nitoe mfano labda utawa motivate watu fulani,
"Kuna binti aliamua kuingia kwenye car washing business, kwa kuanza na kuosha gari la baba na mama yake baada ya kuwashawishi wasiende tena car wash za nje. Resources zote zilipatikana nyumbani tena bure, hivyo akawa anatengeneza 8000 per day, baada ya mwezi mmoja akaamua kuwazungukia majirani zao wenye magari, akapata hapo wateja wengine wawili... biashara iliendelea kuingiza mapato na wateja wapya ikabidi binti aajiri watu wengine, na baada ya muda akanzisha CAR WASH kwani alishakuwa na fedha za kutosha, knowhow na soko"

Lakin mimi nasema hiyo ni kwa mazingira fulani tu, huku site mimi nilifundishwa mambo manne in getting more work done nayo ni motivation, know-how, capital and outlet. Na hapa query inayojitokeza ni kwenye hiyo capital (Tsh. 5000). Issue kwamba itatosha au haitoshi na mtu atatoka kwa muda gani, nadhani tuyaachie mazingira kwani yanatofautiana.

Ila kwangu mimi nasema mazingira hayo yataathirika sana na UMRI wa muhusika, majukumu yake, matumizi yake, soko lake na sehemu alipo. Until then ndio utaweza kutoa conclusion kuhusu huo mtaji.
 
Wakuu kunajambo ambalo watu wengi hawajaliona,watu hapa naona wanazungumzia mambo ya kuchukua elfu tano na kupata na kuendelea mpaka unakua tajiri ambayo ni ndoto.Sasa basi nyie mnaotupigia mahesabu jinsi elfu tano ilivyoongezeka mpaka ikafikia mamilioni suala la hasara kwenye hiyo biashara halipo?wewe hiyo joice yako umeichukua ukaipeleka standi kuuza bwana afya akajanmgambo wa jiji akaichukua katika zoezi la kuzibiti kipindupindu.Manake naona kila mtu anazungumzia kupata tuuu biashara haiko hivyo wakuu ukiona faida kuna hasara pia.

Kitu kingine nilichoona watu wengi hapa kwenye vichwa vyao biashara wanayofikiria ni umachinga tuu,hamuwezi kuwa na mawazo mapana zaidi mkaachana na biashara ya umachinga mkafikiria biashara nyingine kama kilimo n.k.

Panueni mawazo wakuu msifikirie umachinga tuu ndio utawatoa.
 
Back
Top Bottom