Sh 5,000 inaweza kabisa kunitoa kimaisha!

Wakuu kunajambo ambalo watu wengi hawajaliona,watu hapa naona wanazungumzia mambo ya kuchukua elfu tano na kupata na kuendelea mpaka unakua tajiri ambayo ni ndoto.Sasa basi nyie mnaotupigia mahesabu jinsi elfu tano ilivyoongezeka mpaka ikafikia mamilioni suala la hasara kwenye hiyo biashara halipo?wewe hiyo joice yako umeichukua ukaipeleka standi kuuza bwana afya akajanmgambo wa jiji akaichukua katika zoezi la kuzibiti kipindupindu.Manake naona kila mtu anazungumzia kupata tuuu biashara haiko hivyo wakuu ukiona faida kuna hasara pia.

Kitu kingine nilichoona watu wengi hapa kwenye vichwa vyao biashara wanayofikiria ni umachinga tuu,hamuwezi kuwa na mawazo mapana zaidi mkaachana na biashara ya umachinga mkafikiria biashara nyingine kama kilimo n.k.

Panueni mawazo wakuu msifikirie umachinga tuu ndio utawatoa.

Lakini hata kilimo kinategemea usindikaji pia. Hao wasindika matunda (kama NDYOKO) ni important stakeholder in the value chain
 
Sasa jamani si mwendo wa polepole hiyo elfu nne au tatu ya faida kwa siku mara mwezi ni kama 100,000. Akitunza na kupanua biashara yake baada ya miezi 3 basi anapata wastani wa 300,000 hii inakuwezesha kufanya kitu kingine kikubwa zaidi au kutanuka zaidi
assuming that all other costs remain constant (nadhani huyu mtu mwenye mtaji wa 5000 ni aidha mama wa nyumbani au mtu anakaa kwa ndugu au mfanyakazi ambaye kipato chake hakitoshi kuweza kubaki na mtaji mkubwa zaidi ya huu)
Naona wengi hawaamini lakini ujasiriamali ni kubuni biashara kulingana na malighafi ulizonazo au unazoweza kutumia bila gharama yeyote au kwa gharama ndogo sana. Mtu wa nyumbani au mama anaangalia jiko, vyombo nk wanavyotumia hapo kama malighafi hivyo anahitaji unga, mafuta nk ili aanze biashara. Ndiyo mfano wa ndg Mengi aliiangalia uwani kwake akaona anaweza kuanzia kiwanda, wakati kwa alipyepanga ingebidi akodi yard ili aweke hicho kiwanda.
Mtaji kwa uelewa wangu ni hela nje ya matumizi yako ya kila siku, hivyo akisema 5000 hamaanishi chakula, mavazi na malazi itoke hapo kabla sijazalisha na kuwa stable walau kwa mwezi 1 au 3.

Unachosema kina ukweli Mama Joe, lakin mchanganuo wako unapaswa kuonyesha na matumizi yako binafsi kutokana na kipato chako. Hakuna suala la kuzalisha na kuuza tu. Mpaka ufanye hivyo ndio tutaweza kuhitimisha kama biashara yako itafanikiwa nawe utatoka.
 
haya mimi nataka nitoke kwa tsh. 5,000/=. mchanganuo ni kama ifuatavyo.

Nitafanya biashara ya mchicha na spinach/chinees. nitaziuza kilimahewa stend eneo ambalo wengi wanashuka kwa kasi. Kwa biashara hii, nitakuwa naenda kuchukua bidhaa yangu kwa mkulima moja kwa moja.
1. Chinees 15 kwa sh. 200/- bei ya jumla. nitoa fungu 3 kila moja ikiwa na chinees 5. nitauza kwa tsh 200/- kwa fungu moja nitatengeneza 400 faida. faida itazidi mtaji.

kwa hiyo ukichukua 5,000/200= 25.
fungu 25 za jumla zitaleta fungu 25*3=75
75*200=15,000/=

kwa mapato hayo kwa siku, natengeneza 10,000 kama faida. kwa mwezi 300,000/= nadhani kula, kupanga chumba na sebule nitaweza. baada ya miaka miwili nanunu kiwanja na kujenga chumba kimoja kwanza, nahamia kwangu

Umeandika as if una uhakika wa kuuza kila siku?!
 
Kweli unaweza ukafanikiwa but utachelewa sana. Lakini NDYOKO mbona umepigia mahesabu ya hizo raw materials tu na si vitendea kazi? Kwa mfano Blender? Kisu? Fridge/Ice Blocks?, Dumu?, Glass?, Usafiri (to/from Sokoni), Sufuria, Boiled water (mkaa, jiko, maji n.k). Hiyo 5000 labla itatosha kama utakuwa umeshajipanga, kwani hiyo biashara si rahisi namna hiyo
Nadhani anaanza kwa kusindika kwa mkono ubaridi anadandia kwa wazoefu , kuhemsha anadandia jiko la mama ntilie alitye karibu n.k. otherwise haitoshi 5000 kuanza nayo
 
Je kwa asiyekua KKB(Kulakulala Kwa Baba)?

Kaka badlisha avatar; maana naona sku hizi umeanza kufanana nayo..hahahaa!
Nadhani ni vizuri ukarudia kusoma heading ya Ndyoko; amesema hiyo elf5 inaweza kumtoa yeye ambaye ni kula kulala katika mazingira yake kivyake, kama wewe siyo kula kulala unatakiwa ujiongeze kivyako ili hyo elf5 ikutoe, ukipenda unaweza kwenda kuirambia ugimbi ili upunguze mawazo!:yawn:!
 
Wakuu kunajambo ambalo watu wengi hawajaliona,watu hapa naona wanazungumzia mambo ya kuchukua elfu tano na kupata na kuendelea mpaka unakua tajiri ambayo ni ndoto.Sasa basi nyie mnaotupigia mahesabu jinsi elfu tano ilivyoongezeka mpaka ikafikia mamilioni suala la hasara kwenye hiyo biashara halipo?wewe hiyo joice yako umeichukua ukaipeleka standi kuuza bwana afya akajanmgambo wa jiji akaichukua katika zoezi la kuzibiti kipindupindu.Manake naona kila mtu anazungumzia kupata tuuu biashara haiko hivyo wakuu ukiona faida kuna hasara pia.

Kitu kingine nilichoona watu wengi hapa kwenye vichwa vyao biashara wanayofikiria ni umachinga tuu,hamuwezi kuwa na mawazo mapana zaidi mkaachana na biashara ya umachinga mkafikiria biashara nyingine kama kilimo n.k.

Panueni mawazo wakuu msifikirie umachinga tuu ndio utawatoa.

Ungekuja na wazo panufu mkuu ungekuwa umesaidia wengi kuliko kuponda tu bila kutoa ushauri ulio wazi na mpana. Tunajaribu kumsaidi ndugu yetu Ndyoko hapa yeye anadai ana mtaji wa buk5 tu na anataka imtoe na aendelee kubaki mjini na hatimae kutoka, sasa wewe kama unamshauri arudi shamba kulima itakuwa vizuri kumwekea mchanganuo wa kilimo kwa hiyo buku5, kumbuka kuwa hana ardhi wala jembe!!! Karibu.
 
AMOEBA umerudi,nashukuru sana AMOEBA umeanza kupata mwanga kua elfu tano haiwezi kununua hata jembe kwa kweli mie hua nashukuru sana napomwelimisha mtu halafu akaanza kunielewa,ndio maana AMOEBA nikakuambia labda elfu tano ya kimarekani ili aweze kununua angalao kajishamba na jembe na kabalance kabaki ka emegency lakini mwanzoni ulipinga sana lakini naona kadri tunavyozidi kukuelimisha unaanza kutuelewa.
 
Kaka badlisha avatar; maana naona sku hizi umeanza kufanana nayo..hahahaa!
Nadhani ni vizuri ukarudia kusoma heading ya Ndyoko; amesema hiyo elf5 inaweza kumtoa yeye ambaye ni kula kulala katika mazingira yake kivyake, kama wewe siyo kula kulala unatakiwa ujiongeze kivyako ili hyo elf5 ikutoe, ukipenda unaweza kwenda kuirambia ugimbi ili upunguze mawazo!:yawn:!

Ha ha haa haaaaa AMOEBA unavituko kweli.
 
AMOEBA umerudi,nashukuru sana AMOEBA umeanza kupata mwanga kua elfu tano haiwezi kununua hata jembe kwa kweli mie hua nashukuru sana napomwelimisha mtu halafu akaanza kunielewa,ndio maana AMOEBA nikakuambia labda elfu tano ya kimarekani ili aweze kununua angalao kajishamba na jembe na kabalance kabaki ka emegency lakini mwanzoni ulipinga sana lakini naona kadri tunavyozidi kukuelimisha unaanza kutuelewa.

Kaka haujajbu hoja!! Mdau ametoa mchanganuo wake vizuri kabisa, na mifano HALISI tumekuwekea hapa, bado unabisha tu!....nimeanza kupata mashaka na wewe!:A S embarassed:
 
AMOEBA umerudi,nashukuru sana AMOEBA umeanza kupata mwanga kua elfu tano haiwezi kununua hata jembe kwa kweli mie hua nashukuru sana napomwelimisha mtu halafu akaanza kunielewa,ndio maana AMOEBA nikakuambia labda elfu tano ya kimarekani ili aweze kununua angalao kajishamba na jembe na kabalance kabaki ka emegency lakini mwanzoni ulipinga sana lakini naona kadri tunavyozidi kukuelimisha unaanza kutuelewa.

Katika Dunia ya wajasirimali michango kama hii haitakiwi kabisa,

Mkuu mjasiriamli huwa ana strategies nyingi sana za biashara na moja ya strategies ni kuona aanzishe vipi business kwa mtaji mdogo?

Hapa mjasirimali inabidi akae chini na aumize kichwa atafanyeje.

MKUU NDO MAANA KATIKA STRATEGIES ZA KIJASIRIAMLI KUNA HAYA,

1. Kuanzisha biashara ukiwa nyumbani/ offisi inakuwa ni chumba unacho ishi wewe,- hii ni mbinu ya kupunguza ghalama na usiniulize hicho chumba kitakuwa hakilipiwi, hapa ni kwamba kabla ya kuingia kwenye ujasiriamli hicho chumba ulikuwa unakilipia vip?

2. Kutumia vifaa vyako ulivyo nunua kwa kazi tofauti. mkuu wewe unaweza ukawa unagheto lako na unataka kuligeuza gheto lako la chumba kimoja kuwa gest na na tiyali ulikuwa na kitanda ulicho kuwa unalalia so hapa tiyali unakuwa umetumia strategies nzuri sana,

3. Kuwa kila kitu- wewe ndo meneja, mhasibu, mkurugenzi, msambazaji, afisa ugavi, afisa masoko, na kazalika so hapa ili kuipeka ghalama wewe una kuwa kila kitu mpaka hapo utakapo simama vizuri ndo uweze kuajiri wafanyakazi,

4. Kuangalia wapi uatapata vifaa vya bure vya kufanyia kazi, hapa mkuu mtoa maada anaweza kuwa atatumia vifaa vya rafiki yake, ndugu au jirani yake kwa kuanzia, so hii mkuu ni mbinu ya kijasiriamali.

SO WA KUU MSISEME HAIWEZEKANI NA KAMA WEWE NI MWAJIRIWA UNASUBILIA MWISHO WA MWEZI HAITAKAA 5000 IFANYE BIASHARA DAIMA, NA KAMA WEWE NI MFANYA BIASHARA HAITAWEZEKANA, ILA KAMA WEWE NI MJASIRIMALI INAWEZEKANA SANA
 
Nadhani anaanza kwa kusindika kwa mkono ubaridi anadandia kwa wazoefu , kuhemsha anadandia jiko la mama ntilie alitye karibu n.k. otherwise haitoshi 5000 kuanza nayo

Mkuu hizo zote ni moja ya mbunu za kijasiriamli, huwezi anzisha biashara bila kuwa na mbinu mbalimbali, la sivyo makampuni makubwa ya dunia kwa sasa yasingekuwepo kabisa
 
Unajua watu wanashindwa kuelewa lazima hapa tufahamishane,kuna watu wanasema kuwa wanawafahamu watu wametoka kutokana na hiyo elfu tano halafu wanaanza kutukokotolea mahesabu feki hapa,mwingine anasema atafanya atafuga kuku awazalishe chakula hanunui,hawatakufa kwa magonjwa,hawataibiwa,vicheche hawatawagusa na blabla nyingi za kufikirika,mie napenda kusema hivi unapomwona mtu alikua anauza karanga,machungwa au barafu leo kajeuka kua bharesa lazima kuna mahali kapiga panga ndio akatokea hapo.Wewe ambaye ulimwona yule mtu alikua anauza barafu na kidumu leo yuko na prado eti unaanza kuzani kuwa ni ile biashara aliyokua anafanya akafika hapo,watu wengine mchana anauza machungwa usiku kibaka jambazi you never know?kwa sababu wewe hauko nae wakati wote kumbe amepata fedha za hujma akafanya kitu kikubwa we unaanza kuwazia ile elfu tano ndio imemtoa,unafikiri yeye atakuambia zari amelipata wapi?

Mfano wa jamaa mmoja anaitwa Reginald Mengi anakuambia utajiri wake umeanzia kwenye sijui kuuza kalamu leo ni bilionea zari kalipata wapi la kuinuka,kaipiga NBC sawasawa twende kwenye NICO kaianzisha kakusanya elfu tanotano zenu kawabwaga,we unabaki kutoa mfano hata mengi alianzia chini,naombeni wakuu mnaoona elfu tano itawatoa muwe na mawazo mapana zaidi.

Hii nilikuwa sijaisoma, UNA MAWAZO POTOFU! Mifano niliyokupa mimi si ya kusadikika, ni real life scenario kaka, ELEWA! Sifahamu Mengi alikotoka, lakn suala la kusema alipiga NBC linaonesha kuwa uko low sana kaka. Hata hzo deals huwezi kupata kizembezembe tu, lazima wadau wakuone we mchakarikaji!
AMKA!
 
Wakuu kunajambo ambalo watu wengi hawajaliona,watu hapa naona wanazungumzia mambo ya kuchukua elfu tano na kupata na kuendelea mpaka unakua tajiri ambayo ni ndoto.Sasa basi nyie mnaotupigia mahesabu jinsi elfu tano ilivyoongezeka mpaka ikafikia mamilioni suala la hasara kwenye hiyo biashara halipo?wewe hiyo joice yako umeichukua ukaipeleka standi kuuza bwana afya akajanmgambo wa jiji akaichukua katika zoezi la kuzibiti kipindupindu.Manake naona kila mtu anazungumzia kupata tuuu biashara haiko hivyo wakuu ukiona faida kuna hasara pia.

Kitu kingine nilichoona watu wengi hapa kwenye vichwa vyao biashara wanayofikiria ni umachinga tuu,hamuwezi kuwa na mawazo mapana zaidi mkaachana na biashara ya umachinga mkafikiria biashara nyingine kama kilimo n.k.

Panueni mawazo wakuu msifikirie umachinga tuu ndio utawatoa.

Mkuu Sijakupata kabisa, kila biashara inawezekana kukua na ikawa kubwa sana.

1. Mama lishe anaweza kupanua biashara yake na akamiliki migahawa mikubwa ya chakula east and central Africa, tatizo wanakosa mbinu za kijasirimali wanakosa Vision na ndo maana biashara zao zinashindwa ku graduate kutoka small to medium na kutoka medium to big one.

2. Machinga mutembeza viatu anaweza kugraduate na kuwa na maduka makubwa sana ya kuuza viatu, anakosa mbinu za kijasiriamali ndo maana anashindwa ku grdaute kutoka hapo alipo kwenda hatua nyingine.

3. Jamaa muuza juice anaweza kugradute na akamiliki kiwanda cha kusindika juice na akawa anauza hadi ulaya, mkuu huyu mtyu anakosa mbinu za biashara za kumwezesha ku sogea kutoka step moja kwenda nyingine,

4. Mkulima, anatakiwa amove kutoka hapo alipo, amiliki shamba kubwa na vitendea kazi vyote hii ni pamoja na kuwa na kiwanda chake mwenyewe cha ku process na kupak,

MKUU WAKULIMA UNAO SEMA MBONA WENGI WAO WAKO HAPO WALIPO MIAKA NENDA RUDU? JE WANATOFAUTI GANI NA WAMACHINGA?

WOTE WANAKOSA MBINU ZA KUWEZESHA BIASHARA ZAO KU GRADUATE KUTOKA BIASHARA NDOGO KWENDA YA KATI NA HATIMAYE KUBWA

So mkuu biashara ya aina yoyote inaweza kumfanya mtu akawa bilionea mkubwa sana tatizo watu wetu wana laki mbinu za kuwa fanya kusogea ndo maana miaka nenda rudi utakuta ni umachinga tu au ni mama lishe miaka nenda rudu,
 
Unachokiongea KOMMANDO kina ukweli ndio maana nimekugingea like (BUT hapo kwenye RED unapingana na title, kwani jamaa anataka kutoka), lakini umebase kwenye lecture zaidi ya hali halisi inayotokea site (soma saiti). Wakati nafanya mafunzo ya ujasiriamali hayo maneno niliyasikia sana, but ukimtizama mkufunzi anayekufundisha utagundua haamini anachokisema au hajui hali halisi ya site.

Sasa kwa kuwa wengine tulikuwa ni watu wa Site kwa muda mrefu tulikuwa na advantage kidogo ya kuwasumbua walimu wetu, ingawa nilijifunza mengi lakin vitu vingi nilivyotegemea kuvipata sikuvipata. Ni suala hili ndilo lililonifanya nitafute Mentor, ambaye yupo juu zaidi yangu ili nijifunze mambo halisi ya Site through what they call Tacit knowledge. Elimu hii haina cheti, lakin mchango wake kwa mtu yeyote ni mkubwa sana, nadhani ndio maaa watanzania wenye Asili ya Asia wanafanikiwa sana.

Mambo mengi ambayo sikuyapata darasani, niliyapata Site kwa Mentor wangu na baada yakuona nimekubuhu aliniacha niendelee na biashara zangu. Mambo niliyojifunza huko site ni tofauti sana na ya darasani, na ndio ninayokutana kila siku kwenye ujasiriamali wangu, hivyo naweza kukabiliana nayo. (Mpaka nilipata wazo la kuanzisha darasa litakalokuwa facilitated na real entrepreneurs, na litakuwa promoted na hii slogan WHAT IS NOT TAUGHT IN BUSINESS SCHOOL).

Nakumbuka wakati huo ninasomea ujasiriamali, tulikuwa tunafundishwa kwamba, fedha si chochote kwa mjasiriamali halisi, kama ulivyosema wewe na kweli nakubaliana na hilo kwa kiasi fulani, na hapa nitoe mfano labda utawa motivate watu fulani,
"Kuna binti aliamua kuingia kwenye car washing business, kwa kuanza na kuosha gari la baba na mama yake baada ya kuwashawishi wasiende tena car wash za nje. Resources zote zilipatikana nyumbani tena bure, hivyo akawa anatengeneza 8000 per day, baada ya mwezi mmoja akaamua kuwazungukia majirani zao wenye magari, akapata hapo wateja wengine wawili... biashara iliendelea kuingiza mapato na wateja wapya ikabidi binti aajiri watu wengine, na baada ya muda akanzisha CAR WASH kwani alishakuwa na fedha za kutosha, knowhow na soko"

Lakin mimi nasema hiyo ni kwa mazingira fulani tu, huku site mimi nilifundishwa mambo manne in getting more work done nayo ni motivation, know-how, capital and outlet. Na hapa query inayojitokeza ni kwenye hiyo capital (Tsh. 5000). Issue kwamba itatosha au haitoshi na mtu atatoka kwa muda gani, nadhani tuyaachie mazingira kwani yanatofautiana.

Ila kwangu mimi nasema mazingira hayo yataathirika sana na UMRI wa muhusika, majukumu yake, matumizi yake, soko lake na sehemu alipo. Until then ndio utaweza kutoa conclusion kuhusu huo mtaji.

Mkuu nimeipenda sana hii, na niseme ndo moja ya character za Entrepreners wote, huyo Dada hakuwa na hata sh 100 ila nyumbani kulikuwa na vitendea kazi akaamua kutumia hivyo vya nyumbani kuanzisha car wash,
Hiyo ni mbinu ya kijasiriamli kabisa na wajasiriamli wakubwa wa dunia wlitumia mbinu hii kutoka.

Kuhusu point yangu ya kwanza, ni kweli ila ni mejarubu tu kuonyesha ni jinsi gani inawezekana ila kama yeye ni profit oriented hiyo ni up to him
 
Mkuu, naona kuna kutoelewana "viswahili" hapa, labda tubadili Lugha kidogo; Hyo elfu tano kwa vijana wanatoka mlimani ni ndogo sana kwao kuanzia, lakn siyo jambo lisilowezekana! Amini nakwambia, kuna graduates wengi wanakaa mtaani hata mika miwili kulakulala hawana kazi wanasubiri keep change ya mama....na kuna FIV leavers wengi wanatumia mtaji wa el3 kwa siku kukodi troley la kubebe a mzigo na mwisho wa siku wanagawana mpaka elf20 take home!!! Haina haja ya kutajana majina humu, nina jamaa yangu wa karibu ambaye ana biashara za faida zaidi ya 400M/pm aliishia stdIV; amini nakwambia alianza kwa kufyatua tofali za kuchoma KWA MIKONO YAKE!! Huyu jamaa ratiba yake ni kuamka saa11 na kulala saaa6 usiku kila siku ispokuwa jumapili tu, huyu jamaa mpaka leo anaendesha CRESTA, vijana wa Bongofleva mnaweza?

Mimi naona tunajifungia sana ndani jamani mpaka tunakuwa na mawazo mgando, internet tumeifanya kuwa chanzo cha kila kitu bila kufahamu kuwa kuna tabaka flani la watu tunaoweza kuwachukulia kuwa mifano ya kuigwa hawaingii huku!! LET US BE REALISTIC!

Nimeona nimeipenda nilijaribu na nikaweza
 
Hii kitu inawezekana kabisa siyo lazima uanze na mtaji mkubwa. mimi mwenyewe nilianzisha biashara nikiwa na mtaji wa 18,000,000/= baada ya mwaka mmoja na nusu nikapata hasara ya 4,000,000/= nikabakiwa na 14,000,000/= hii ilinipa changamoto sana nikaamua kuchukua 13,000,000/ nikanunua kiwanja na kujenga kibanda cha vyumba viwili na kuanzisha biashara kwa mtaji wa shilingi 500,000/ tu na kwa sasa naingiza 700,000/= kila mwezi kwa mtaji wa 500,000/= nilioanza nao.Mimi naamini kabisa hata hiyo 5000/= inaweza kukutoa kama uko committed kwa mfano wauza mchicha wananunua kwa shilingi 50/= kila fungu na kuja kutuuzia kwa shilingi 100/= anapata faida ya 100%.
 
Kuna watu hawaamini ktk hili,lakini kuna watu wameanza biashara wakiwa mikono mitupu kabisa na leo wana mitaji mizuri.Wakati mwingine nguvu/afya/kujua ni mtaji tosha kama uko ktk mazingira ya kula kulala.

Wakati nasubiri matokeo ilibidi niombe viazi home kama debe moja kisha nibebe kwa kichwa km 35 ili nikauze,debe hilo likiuzwa sh 150/. Mtindo uliokuwa ukitumika enzi hizo ni kwamba unalipwa nusu kisha nusu unaifuata siku nyingine. Kwa hiyo nilipiga safari kama kumi hivi na nikajipatia 1,500/. Enzi hizo 1500 ilikuwa ni ada ya secondary ktk shule binafsi.

Baada ya kupata hiyo hela,ilibidi home wasijue,nikabadili biashara, nikawa nakusanya mayai kijijini na kupeleka kimji cha jirani. Mjasiriamali lazima uwe mbunifu sana kwa kuangalia mazingira uliyo nayo.
 
Hili nalo neno
Kuna mtu amependekeza kuanza biashara kwa sh 5000, kama kawaida waungawana humu jf wamedai apeleke huo uzi wake joke forum. Lakini mie nna mtazamo tofauti hapa. Kwamba bado hiyo elfu tano inaweza kukutoa kabisa kama kweli uko serious. kwa namna gani inaweza kukutoa, hebu fuatilia hapa chini:

Nimeamua kufanya biashara ya kuuza juisi ya matunda.

Mananasi 2 sh 2000
Parachichi 2, sh 1500
Sukari robo 1000
Jumla 4,500

Baada ya kuitengeneza zitatoka walau lita tano, ambazo kwa kiwango cha chini, ntapata jumla ya glass zisizopungua 15. Kwa bei ya gsh 500 kwa glass moja, ikiisha ntapata jumla ya sh 7500.

Kumbuka hapo nimemaliza chuo, bado mie ni mtu wa kula kulala-yaani nakaa geto. Nimeshatengeneza faida ya shi 3000, kwa siku. Hii ina maana kama ni ajira basi nalipwa 90,000 kwa mwezi. Hivi ntalala njaa kweli nikiamua kuwa serious na hii bishara?

Hivi kwa hesabu ndogo kama hii, kuna haja kweli ya mtu kulia njaa jamani. Mi nadhani kinachotusumbua wengi ni kale katabia kwamba hiyo kazi ni ya kufanywa na mtu ambaye hana shule, lakini hela haina shule, na sioni kama hapo kuna kudhalilika kwa aina yeyote. Jamani, let us start from the scratch kama hatuna mbadala wa aina yeyote ktk ajira zetu.

Tanzania hii kila kitu kinawezekana, sio ufisadi pekee tu!
 
Kama biashara zingekuwa rahisi kwa mtindo huo sidhani kama kungekuwa na "MASIKINI"

ni maskin kwa sababu hata mind zetu ni maskin kwa kufikiri, acheni kukatisha wenzenu tamaa kuna watu wanakaa home wana kila kitu kama hizo vitendea kazi lakini anambwela tu kutwa kubadilisha movies na series, kula kulala bure angemwambia dingi me naanzisha kuuza juis nadhani pia angesapotiwa home

biashara ni nia na commitment
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom