Kilimo kinalipa sana

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Njmeshazisoma nyuzi kadhaa humu jamvini zinazohamasisha kilimo. Pamoja na kwamba ni nyuzi za kuvutia, kuna watu wameonekana kuwa na mashaka na hata kuwaita MOTIVATIONAL SPEAKERS watoa mada husika. Na wengine, katika kuonesha kutokukubaliana nao, huziita ni kilimo cha kwenye makaratasi.

Lakini ni kweli kilimo hakilipi?

Hivi majuzi nilimtembelea mkulima mmoja nchini Kenya. Yeye anajishughulisha na kilimo cha matunda mbalimbali, yakiwemo matunda yanayodaiwa kuuzwa ghali, DRAGONS. Na inawezekana kwa sababu hata mimi mwenyewe niliyanunua kadhaa humo shambani kwake kwa bei ya shambani , yaani, ya jumla. Niliuziwa tunda moja kwa Ksh 500/=. Nilichukua manne kwa Ksh 2,000/=.

Ingawa eneo lake si kubwa sana, lakini anaonekana kuwa na mafanikio katika shughuli zake hizo. Miundombinu iliyopo kwenye bustani yake, na hata wafanyakazi aliowaajiri, ni uthibitisho kuwa kazi yake inamlipa.

Mfanyakazi aliyepewa jukumu la kunitembeza bustanini, aliniambia kuwa robo eka ya shamba lililopandwa dragon fruits inaweza kuwaingizia hela ya Kenya sh milioni moja kwa mwaka. Ukiibadilisha kwa hela ya Kitanzania, ni zaidi ya million kumi na Sita. Na hiyo ni robo eka tu. Je akiwa na eka 20?

Huyo bwana ameisajili biashara yake ya ukulima wa matunda. Nilipofika bustanini hapo, niliwakuta wageni kadhaa akiwemo mtu wa mahesabu aliyeenda kumsaidia kuandaa ripoti ya masuala ya kodi. Wakati wa kuondoka, alitupeleka kwa gari lake hadi kituo cha mabasi.

Nilipata nafasi ya kubadilishana mawazo na huyo mhasibu ambapo nilipomwuliza kama ana mpango wa kujihusisha na kilimo, alisema anatafuta ardhi. Akipata kuanzia ekari 3, anakuwa mkulima wa "full time". Siyo eka 30, ni eka 3.

Aisee! Watanzania tuna fursa ambayo wengi hawajaijua!!!

Jibu lake, pamoja na nilichokishuhudia kwa huyo mkulima niliyemtembelea, imenifanya nitilie mashaka hoja kuwa kilimo hakilipi.

Ninashawishika kuamini kuwa kilimo kinalipa kikifanywa kwa mujibu wa kanuni zake.

Kama Wakenya wenye uhaba wa ardhi wamefanikiwa sana kwenye kilimo, sisi Watanzania tulio na ardhi tele yatupasa tuwe na mafanikio makubwa zaidi kuwazidi.

Najua kuna baadhi ya Watanzania ambao wameshaonesha kwa vitendo kuwa kilimo kinalipa, lakini bado wengi hawaliamini hilo.

Nihitimishe kwa kusema kuwa SIYO KWAMBA KILIMO HAKILIPI TANZANIA, BALI HAKILIPI KWA MTU YEYOTE ASIYEZINGATIA KANUNI STAHIKI.

Kilimo KINALIPA sana.
 
Nimekimbilia kufungua uzi nikajua unaleta maelezo uliyoyafanya wewe mwenyewe kwa vitendo ukapata mafanikio. Fanya hicho kilimo kwa kufuata kanuni ndio ulete ushuhuda
 
Aliyekwambia kilimo hakilipi nani?

Kinachosababisha watu wasipende kilimo hasa watu kutoka Bara Africa ni kwamba,kilimo hapo Zamani kilifanywa kama adhabu au kazi ambazo niza watu walioshindwa maisha!,Ndiyo maana vijana wengi walikikimbia kilimo,mtu akaona ni heri kama amemaliza chuo auze Ubuyu kuliko kurudi kulima kisasa!.

Zamani ulikuwa kijana akionekana ni mkulima anaonekana Mshamba na aliyekata tamaa!.

Watu hivi sasa wameelimika na wanafanya kilimo kwa njia za kisasa,siyo ile heka 10 unataka ulime kwa jembe la Mkono!.

Kwa namna ambavyo Vijana wengi wanamaliza vyuo na hakuna Ajira za moja kwa moja,nilitegemea serikali ishawishi wawekezaji wafungue viwanda vya kuunga Power Tila na Trekta ili ziuzwe kwa Bei nafuu,vijana wakopeshwe waingie kwenye Kilimo!.

Kilimo kina hela endapo utatumia vifaa vya kisasa kulima!
 
Kweli kilimo kinalipa kama utafuata taratibu za kilimo. Mimi nimelima ekari 5 za mahindi msimu huu na nimefuata taratibu zote ikiwa kupanda mbegu bora, kupiga dawa, kupalilia mara mbili, kuweka mbolea ya urea na jinsi ninavyoona mahindi yamestawi sana na natarajia kupata magunia 30 kwa ekari moja na hivyo kwa ekari 5 natarajia kupata magunia 150. Natarajia kuyaweka ghalani mpaka bei ifike tshs.100,000 kwa gunia. Hivyo nitakapouza nitapata Tshs.15,000,000. Gharama niliyotumia haizidi Tshs.2,500,000. Kilimo ukilima kufuata taratibu zote na mvua iwepo basi utatoboa.
 
Back
Top Bottom