Serikali zote duniani hazitaki watu wajue ukweli

Watawala ndiyo chanzo cha ugumu wa maisha kwasababu hawasemi ukweli
Magu alisema unataka serikali ikulishe. Lkn ukweli ni kuwa ukiwa na serikali inayoamini ktk uchumi wa kodi badala ya uzalishaji lzm tupitie maumivu haya. Binafsi Nina mifano hai. Nazi inayouzwa dar sh 1500 mwenye shamba anaiuza kwa sh 250 hadi 300 Lindi.

Fenesi linalouzwa dar 4000 mkulima anauuza sh 500 hadi 1000 shambani morogoro. Usidhanitofauti ya pesa iliopo ni ya walanguzi au madalali. Laa tofauti ya pesa inakwenda serikalini kupitia tozo na kodi na ushuru katika diesel.

Kwa ni diesel ibayouzwa sh 2900/- gharama hadi inafika kwa muuzaji ni sh 1300/- kwa Lita.

Kwa ufupi serikali ikiamua kutoa sh 700 kwa kila Lita ya mafuta utaleta unafuu mkubwa kutuondolea wananchi ugumu wa maisha. Lkn kubwa serikali itakusanya kodi zaidi indirect tax. Kwani samaki watapungua bei, wavuvi wataongezeka, vyakula vitapungua bei lkn wakulima wataiza na kununua pia vitu vingine. Hivyo hivyo kwa sekta zote. Tatizo la kwanza ni diesel. Ambapo kodi take inapaswa kukuswanya baada ya uzalishaji kufanyika na sio kabla yq
 
Duniani kote serikali zote hazitaki watu wajue ukweli!

Kwasababu "Ukweli huwaweka watu huru"

Duniani kote viongozi huapa kuficha siri, Hushika misaafu na biblia kutangaza kuwa wataficha siri badala ya kuapa kusema ukweli na haki!

Yote hayo ili serikali itawale kwa amani inabidi watu wasiwe huru kujua ukweli!
Hivyo nakusanua Leo ishi humu:
  • Ukiona jambo linakanushwa na serikali yoyote kuwa ni uzushi basi tambua "huo ndiyo ukweli wenyewe"
  • Ukiona jambo linatangazwa na kuhamasishwa wananchi wajitokeze tambua hilo jambo "linamaslahi makubwa kwa wahamasishaji kuliko wananchi wanaohimizwa kujitokeza"
  • Ukiona serikali inahimiza ibada ni kwa ajili ya kuiombea aman serikali husika
  • Ukiona mtoa taarifa anasakwa kwa tuhuma za kusema uongo basi alichosema ni kweli
  • Ukiona jambo limetolewa ufafanuzi basi huo ufafanuzi huo huwa ndiyo uongo halisi!
  • Ukiona jambo linatolewa bure basi hilo jambo linamaslahi kwa watawala
Huruma pekee ya kweli kwa serikali zote duniani kwa wananchi wake huwa ni kuwazika wanapofariki!

Jitahidi sana kuujua ukweli inje ya mifumo ya serikali, maana huo ndiyo ukweli halisi utakaokuweka huru!
de facto
 
Msemaji wa serikali huku kijijini kwetu angejibu hoja zako kwa mtiririko ufuatao.

Siri za nchi hazipo kwa sababu ya maslahi ya kikundi cha watu bali jamii nzima. Kuna mambo kuyaweka hadharani yanahatarisha maisha ya watu huko walipo field.

Wenzetu wana spies ambao kazi yao kubwa ni ku infiltrated mipango ya nchi zingine hiyo kazi ni risk business. Hata mipango yao ya ulinzi wa ndani mengine inabidi ifanywe kinyume na sheria hasa baada ya kupigwa na tukio ambalo wangeweza lizuizia isipokuwa sheria iliwabana kuweza kubaini tatizo mapema.

Hayo mambo yanataka siri na mengine kedekede, vinginevyo huko kwao kuna wanasheria private na wamebobea kwenye constitutional law wanaweza shitaki serikali na kutakiwa kuwaachia suspect huru kama walikamatwa kwa upelelezi kinyume na sheria au kuwalipa watu fidia. So siri ni kigezo kikubwa serikalini kwa sababu nyingi sana.

Serikali kukanusha
Moja ya jukumu la serikali ni kuelimisha jamii zao. Jambo ambalo linaweza potosha jamii ni lazima litolewe ufafanuzi na serikali ili wananchi wasiwe na mtazamo potofu (wanakichukulia hili swala very serious), it’s one of the national security top agenda nchi za wenzetu.

Mfano katika nchi zenye devolution ya majimbo lazima kuwe na chombo kimoja ambacho kipo chini ya serikali ili waweze fikia sehemu yeyote. Kwa nchi zilizoendelea serikali lazima iwe na upper hand kwenye ku control narrative, I can’t emphasis enough this a no joke kwenye usalama wa taifa huko kwao.

Kuhamasisha jambo
Ni kweli lakini mara nyingi ni kwa maslahi ya taifa serikali zao zinatumia nguvu nyingi sana ku shape behaviour za jamii kwa maslahi ya kubadili social thinking (again ni important tool kwenye maendeleo, be it some promotion ni debatable morally), lakini nyingi ni za ulazima na faida kwenye kubadili fikra za watu hasa wenye uelewa mdogo juu ya jambo fulani.

Ibada
Ni kwa sababu dini nyingi zinafundisha watu kufanya mambo mema, and offers hope to individual where the government can’t so positive religious reinforcement ni tool muhimu kwenye amani ya nchi.

Ukiona mtu anasakwa kusema uongo
Kuna mawili kama ni afisa wa usalama basi anashukiwa kutoa siri ya mambo ambayo nimeyaelezea awali au ame-leak sensitive information nje ya mfumo. Kama ni mtu wa nje kapewa siri na kabwabwaja huyo kiumbe watamsumbua kutaka kujua source yake na wakimbaini aliempatia hizo info, muhusika atatia akili kama hawajachukua uhai wake. Ulaya huwa awana utani na kutoa siri za nchi.

Pili kwa raia au vyombo vya habari kuna sheria kali za kutangaza habari usipofuata au ukajitungia story tu adhabu zake ni kali mno, Tanzania zipo Magufuli alijaribu vilio tumeviona ila huko kwao vunja ukione cha moto kama wewe ni mainstream media.

Ukiona jambo linatolewa bure
Hii ni sehemu ya promotion ya sera au kubadili social thinking kuendana na agenda ya kitaifa.

Hayo maelezo ni kwa ufupi tu, sijui kwetu Tanzania; lakini huko kwa wenzetu hiyo top echelon ya civil services inayoongozwa na katibu mkuu kiongozi sikia tu kuna mijitu ina akili na mbinu za kuongoza nchi sio mchezo, halafu imepikwa huko awaokoti watu mtaani na kuwapa post za juu ndani ya wizara hadi kufikia kuwa kigogo wizarani sio shughuli ndogo.

Hao wanasiasa wenyewe baada ya kushinda chaguzi chamoto wanakiona wakitaka kubadili dira ya nchi pamoja na kwamba wao ndio wenye mandate na sio hao civil services.

Tanzania ni nchi ambayo inaendeshwa ovyo mno sijapata kuona.
Haya ni majibu yanayofanana na kweli ila ni uongo. Maneno ya aina hii huwa ni silaha ya tatu kwa mwisho kwa watu ambao wanataka kujua ukweli. Bada ya maneno haya huja vitisho, baada ya hapa huja kifo.
 
Na pia serikali ni kikundi cha watu wachache kilichojitwalia madaraka kwa wananchi wa nchiehusika kisha kuweka mfumo wa kuwatoza pesa wananchi (kodi) kisha kuitumia pesa hiyo ili waishi maisha mazuri, wao pamoja na familia zao na hata ukoo wao, mishahara,mikubwa, kisha kiasi kinachobaki kwenye hiyo pesa mliotozwa ndo hutumika katika huduma za kijamii, mfano ELIMU, HUDUMA ZA AFYA ,MAJI UMEME nk kisha mnatozwa tena hela ili upate hizo HUDUMA muhimu kwa kifupi wananchi ndo tunaihudumia serikali na si serikali kuhudumia wananchi
 
Duniani kote serikali zote hazitaki watu wajue ukweli!

Kwasababu "Ukweli huwaweka watu huru"

Duniani kote viongozi huapa kuficha siri, Hushika misaafu na biblia kutangaza kuwa wataficha siri badala ya kuapa kusema ukweli na haki!

Yote hayo ili serikali itawale kwa amani inabidi watu wasiwe huru kujua ukweli!
Hivyo nakusanua Leo ishi humu:
  • Ukiona jambo linakanushwa na serikali yoyote kuwa ni uzushi basi tambua "huo ndiyo ukweli wenyewe"
  • Ukiona jambo linatangazwa na kuhamasishwa wananchi wajitokeze tambua hilo jambo "linamaslahi makubwa kwa wahamasishaji kuliko wananchi wanaohimizwa kujitokeza"
  • Ukiona serikali inahimiza ibada ni kwa ajili ya kuiombea aman serikali husika
  • Ukiona mtoa taarifa anasakwa kwa tuhuma za kusema uongo basi alichosema ni kweli
  • Ukiona jambo limetolewa ufafanuzi basi huo ufafanuzi huo huwa ndiyo uongo halisi!
  • Ukiona jambo linatolewa bure basi hilo jambo linamaslahi kwa watawala
Huruma pekee ya kweli kwa serikali zote duniani kwa wananchi wake huwa ni kuwazika wanapofariki!

Jitahidi sana kuujua ukweli inje ya mifumo ya serikali, maana huo ndiyo ukweli halisi utakaokuweka huru!

Hakika,umenena ukweli mtupu.
 
Haya ni majibu yanayofanana na kweli ila ni uongo. Maneno ya aina hii huwa ni silaha ya tatu kwa mwisho kwa watu ambao wanataka kujua ukweli. Bada ya maneno haya huja vitisho, baada ya hapa huja kifo.
Kwetu inaweza kuwa porojo, ila kwa wazungu hizo mbinu ni purely sababu ya ushahidi wa kisayansi.

Mtu mwenye taarifa sahihi inamsaidia kufanya maamuzi au kuchukua tahadhari sahihi kutokana na uelewa aliopata.

Sasa nani anakupa taarifa ambazo zinachangia kwenye maamuzi yako au uelewa wako ni swala lingine au hiyo taarifa umeletewa kwa ideologies zipi ni debatable ndio maana kuna theories luluki za media theories na ownership kwenye ku influence jamii, jumlisha na challenge za zama hizi za social media taarifa watu wanaokota kokote huko mitandaoni.

Ndio maana serikali zao hilo jambo wanalichukulia very serious kama sio sehemu ya taarifa zao (government propaganda) au kwenye upotoshaji wa jamii kuhusu mambo muhimu watatumia nguvu nyingi kuhakikisha watu wengi wanapata taarifa sahihi.

Hiyo nguvu ya media ni sehemu kubwa ya kuendesha nchi zao trust me (they take it very serious) nchi kama U.K. serikali ime devolve mambo mengi kwenda kwenye serikali za Wales, Scotland na North Ireland.

Nchi kama Scotland imebakiza mambo matano tu kwenye muungano na moja wapo ni muundo wa BBC hii taasisi control yake jinsi inavyoendeshwa ni swala la U.K. government na lazima iruke kote; usicheze na taarifa zinaweza jenga nchi au kubomoa nchi.
 
Ni mfumo unaoruhusu binadamu wachache kuongoza binadamu wengi.
Mbaya zaidi nchi maskini zinazuia taarifa mhimu, kiasi kwamba waandishi wengi wamekimbilia habari za kiumbea mbea za maisha binafsi kwa kuogopa kutoa taarifa nyeti za msingi (investigation journalism Inaaogopwa)
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Mbaya zaidi nchi maskini zinazuia taarifa mhimu, kiasi kwamba waandishi wengi wamekimbilia habari za kiumbea mbea za maisha binafsi kwa kuogopa kutoa taarifa nyeti za msingi (investigation journalism Inaaogopwa)
Upo sawa Sanaa.
 
Back
Top Bottom