Serikali yatoa siku 4 kwa wafanyabiashara wa Korosho kusema tani wanazohitaji. Baada ya hapo hawataruhusiwa tena kununua

Serikali ya magu haijashtuka tu hiki kibano kinapigwa kutoka nje kumnyoosha huyu anaejifanya mungu mtu ngoja wanaume wamkaange.
 
tatizo lako huwa unaangalia upande mmoja na kuwaza negativity kwa taifa lako,umeshindwa kukumbuka kuwa wafanyabiashara walikubali wenyewe kuwa watanunua kwa bei isiyopungua 3000 hadi leo wamenunua korosho kidogo huku wakulima wakiwa hawajui hatima yao.
Unataka serikali iendelee kuwachekea watu ambao hawaeleweki kama watanunua korosho au hamna?ndio maana serikali imewataka waeleze watanunua tani ngapi ili serikali ijue inawasaidiaje wakukima.
Kama walijua hawawezi kununua kwa nini walikubali kwamba watanunua kwa bei isiyopungua 3000?
Acha kulalamika. mkuu alisema jeshi lipo watabangua hata kwa meno huu ndio muda sasa waende.kelele za nini? Ebo
 
Acha kulalamika. mkuu alisema jeshi lipo watabangua hata kwa meno huu ndio muda sasa waende.kelele za nini? Ebo
silalamiki Mkuu, ila lawama zangu naziweka kwa wafanyabiasha kwanini walikubali kwamba watanunua,au waliogopa kukataa mbele ya Rais?
 
yes, leta sababu za kushuka kwa bei ya mahindi.
Sidhani kama kuna mtu mwenye akili timamu na anayefuatilia vizuri siasa za nchi yetu na Afrika mashariki kwa ujumla asiyejua sababu za kushuka kwa bei za mazao!

Kila mwenye akili timamu anajua vema!!!
 
Kwamba korosho ni "tanzanite" sio!?
Hahaaaaa,vitisho havijawahi kuwa suluhisho la tatizp lolote sehemu yoyote ile duniani na hata mbinguni.
Hapa nafikiri kuna watu wanaamini hakuna korosho sehemu nyingine huko duniani.
 
silalamiki Mkuu, ila lawama zangu naziweka kwa wafanyabiasha kwanini walikubali kwamba watanunua,au waliogopa kukataa mbele ya Rais?
ni ngumu kukataa moja kwa moja mbele ya mkuu wa nchi,,,so walikubali shingo upande ili watoke salama.
 
Sidhani kama kuna mtu mwenye akili timamu na anayefuatilia vizuri siasa za nchi yetu na Afrika mashariki kwa ujumla asiyejua sababu za kushuka kwa bei za mazao!

Kila mwenye akili timamu anajua vema!!!
ushajiuliza kwanini mwalimu humuuliza mwanafunzi swaki ambalo yeye mwalimu analijua?
 
ni ngumu kukataa moja kwa moja mbele ya mkuu wa nchi,,,so walikubali shingo upande ili watoke salama.
ahaa eti watoke salama kwa hiyo waliogopa kukataa kwa kuhofia mkongoto kutoka kikosi rasmi cha ikulu?
 
kwa hisani ya Sikwangalasyene ..........

1. hali za wakulima zinatia simanzi. Masoko ya mazao ya wakulima yamevurugwa

2. wafanyakazi hawakopesheki kwa kuwa hawajaongezewa mishahara kwa miaka mitatu mfululizo hivyo kutokidhi vigezo vya makato

3. biashara zimevurugwa

4. kodi inakusanywa kwa vitisho

5. biashara kama enzi za ukoloni

6. hakuna uwazi kwenye manunuzi (Ndege zimenunuliwa pasipo kufuata taratibu)

7. kuna double standard kwenye kuwajibisha watumishi (Upendeleo)

8. vyombo vya habari havipo huru tena

9. wananchi wamenyimwa haki ya mijadala ya wazi

10. serikali haipo radhi kukosolewa

11. kila mwenye mamlaka ana kauli ya mwisho (Wakuu wa Wilaya na Mikoa wamekuwa kero)

12. upotoshaji kwenye hali ya uchumi wa nchi ni mkubwa

13. 1.5 trillion hazina maelezo (Kuna wizi na ufisadi mkubwa kuwahi kutokea)

14. polisi wanafanya kazi za CCM na si kwa maslahi ya wananchi

15. usalama wa viongozi ni kipaumbele na si usalama wa nchi

16. Traffic police wanakusanya kodi badala ya kuimarisha usalama barabarani
Duh kweli tupu kabisa aiseeeee
 
Back
Top Bottom