Serikali yatoa siku 4 kwa wafanyabiashara wa Korosho kusema tani wanazohitaji. Baada ya hapo hawataruhusiwa tena kununua

Nafurahi Sana nazidi kupata matumaini kuona serikali yangu haiyumbishwi
Safi Sana walizoea..na huu NI ujumbe tosha kwa vikundi vingine vinavyoamini vina nguvu kuliko ofisi ya Rais
Wawe wauza madawa ya kulevya,wawe Wala ruzuku,wawe wafadhili wa mashoga,wawe waaandishi mankanjanja wote wakae wakijua awamu hii iko on fire walete tu vichwa vyao uone Magufuli anavyovikata kwa shoka
NINJAMBO JEMA SERIKALI KUTOKUYUMBISHWA ILA UBABE HAUNA NAFASI KWENYE FREE MARKET NA MAANA YA BIASHARA NI FAIDA KAMA HAKUNA FAIDA HAKUNA ATAKAYENUNUA ndo maana tunasa mambo haya yanahitaji sera zenye kulinda wakulima na si tu wa korosho mahindi yetu yameshuka bei hadi tsh 3000 kwa debe sawa na kilo ya sukari hakuna anayewatetea wakulima mbaazi ndo usiseme kila kg 1 ni tsh 200, tunapofanya siasa tuwe tu acheck and balance
 
Hivi ni mimi sijaelewa au? Si walisema wafanyabiashara wasiponunua kwa bei elekezi Serikali itanunua?
 
SERIKALI YATOA SIKU NNE KWA WANUNUZI WA KOROSHO

*Yawataka waandike barua wakionesha tani wanazohitaji na lini watazichukua

*Yasema zaidi ya hapo haitoruhusu kampuni yoyote kununua korosho tena

SERIKALI imetoa siku nne kwa wanunuzi wote 35 waliojiandikisha kununua korosho wawe wamepeleka barua katika Ofisi ya Waziri Mkuu wakionesha kiasi cha tani wanazohitaji na lini watazichukua.

“Hivyo wanunuzi waliojiandikisha wakiwemo na wale wote ambao wamekuwa wananunua kwenye minada lakini kwa kiasi kidogo, wahakikishe ndani ya siku hizo nne kuanzia leo Ijumaa hadi Jumatatu saa 10 alasiri wawe wameleta barua na ofisi yangu ipo wazi saa 24.”

Hayo yamesemwa leo (Ijumaa, Novemba 9, 2018) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akitoa tamko la Serikali kuhusu ununuzi wa zao la korosho, ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma.Baada ya kupita siku hizo Serikali italazimika kufuta usajili kwa wote waliojisajili kununua zao hilo kwa sababu walikubaliana kwenda kununua lakini hali inayoonekana sasa ni kama kumkomoa mkulima kitu ambacho imesema haitakubaliana nacho.

“Mwenye nia ahakikishe katika siku hizo nne iwe ndio mwisho wa kununua korosho na waandike barua kwani ofisi yangu ipo wazi saa 24 wana nafasi ya kuleta barua wakati wowote wakionesha nia yao na kiwango wanachokihitaji. Zaidi ya hapo Serikali haitoruhusu kampuni yoyote kununua korosho tena.”

Waziri Mkuu amesema kwenye msimu wa ununuzi wa korosho wa mwaka huu, walishuhudia kusuasua kwa minada, ambapo Serikali ilikutana na wanunuzi wa korosho katika kikao kilichoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli ambapo walikubaliana kununua kwa bei inayoanzia sh 3,000 na kuendelea.

“Mjadala ulikuwa wa wazi na wafanyabiashara wenyewe walipendekeza bei ambayo ilikuwa inaanzia sh. 3,000, hata hivyo baada ya kikao hicho ununuzi katika minada imeendelea kusuasua na hata tani zilizokuwa zikinunuliwa zilikuwa kidogo sana. Sisi tunaiona hali hii kama mgomo baridi ambao si sawa sawa sana kwani malengo yetu sisi na sekta binafsi ni kumfanya mkulima apate bei nzuri.

Hali hii haifurahishi kwa sababu Serikali imedhamiria kuboresha mazao yanayolimwa na wakulima kwa kuwasaidia kuanzia katika hatua za utayarishaji wa mashamba, upatikanaji wa pembejeo na masoko ili waweze kunufaika na kilimo na kupata tija katika mazao hayo.”Waziri Mkuu amesema baada ya kugundua bei imekuwa tatizo Serikali ilifanya jitihada za kupeleka wataalamu wake katika masoko makuu duniani na kupata bei halisi ambayo bado inatosha kumlipa mkulima sh 3,000.

Hatua hiyo imekuja baada ya zao la korosho kuendelea kununuliwa kwa bei ya chini na idadi ya wanunuzi kuwa ya chini licha ya uzalishaji wa mwaka huu kuwa mdogo ukilinganisha na msimu wa mwaka jana.Amesema msimu wa mwaka jana uzalishaji ulikuwa zaidi ya tani 300,000 na mwaka huu zinatarajiwa tani zaidi ya 200,000 hivyo wafanyabiashara wanao uwezo kununua korosho zilizopo.

Hata hivyo Serikali imewataka wananchi hususani wakulima wa korosho nchini kuendelea kuwa wavumilivu na watulivu wakati ikiendelea kushughulikia suala hilo.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980
41193 – Dodoma
IJUMAA, NOVEMBA 9, 2018.

View attachment 927388View attachment 927389
Hivi yale mahind yaliyoshuka bei washayanunua
 
Mm nimeisoma akili ya waziri mkuu yale maneno aliyosema Leo hayajatoka moyonii Bali atafanya nini kama mkulu kaamua...

Unajua raisi wetu sometime yupo vzuri sometime ndongaa yakee inajaa upepoo...

Eti unaonge na wafanyabiashara unajijua ww ni mkuu wa nchi unauliza mtanunua korosho unajibiwa ndio alafu mnasema mmekubaliana wakati huohuo mmetaja bei ambayo mnaona korosho hazitok store

Nahisi majaliwa amesema tuu...kwa shingo upandeee utakuja kusikia anajiuzuru Siku c chachee kama hujingaa huu utaendelea...

Ccm hawana jipyaaaa washachokaaa hii serikali inatakiwa wajee watu wapyaaaaa kabisaaa ambao waanzisha vitu na kuendeleza vilivyopoo tutabak na mambo haya haya....

We ukiangalia tangu nyerere yupo madarakan kaacha chata zake ktk nchii...mwinyii kaachaa...mkapa kaachaa chataaa sake kikwete kaachaa chataaa zake... Magufur ataacha chataaa...wakistaafu wawezee kukingiwaa kifuaa...

Sukumaa njeee ccm...utaona tukavyo endelea maana kuna mizizi katika hii nchii watu hawaelewi tuuu...weka serikali mpyaaa
 
Kama alivyosema rais wetu... serekali itanunua hizo korosho kwa bei yenye tija kwa wakulima na itapeleka yenyewe kwenye masoko .... China na kwingineko
Sasa shida na mikwara ya nini? Kumbe mlishatoa ultimatum na plan B, nini kinakwamisha kwenda kununua kwa kilo ikibidi hata 5000 na kupeleka China na huko kwingineko?
 
wakulima wa korosho njooni katika maisha ya mashetani sasa. jiungeni kama walivyojiunga watumishi wa umma
 
Maajabu haya!

Yaani ufutie watu usajili kisa wameshindwa kununua bidhaa/korosho? Kama bei imeporomoka, wao wafanyaje?

Hata kwenye sukari kulikuwa na vitisho vya aina hii ila mwisho wa siku yakawashinda.

Hili zao ndio limeshakufa hapa chini na sidhani kama wakulima watalima tena hili zao.

Vitisho na ubabe ndio vimegeuka kuwa mtaji wa hii serikali badala ya maarifa!!
Wafanya biashara kama wanaumoja wasusie tuu huwez kulazimishwa vile
 
Naye pm ameanza ulevi kama wa Pombe, so ameona awatishie ili wanunue kibabe? Yetu macho na masikio.
Ukiambatana na mlevi kila siku kuna siku nawe utataka kuonja, baadaye nawe utaishia kuwa mlevi.

Ndiyo ule msemo usemao, 'ndege wafananao huruka kwa pamoja'
 
Hawa viongozi Wana maruhani kwa vichwa vyao ai, si walisema wafanyabiashara wakishindwa Kunumua kwa bei elekezi basi serikali itanunua korosho yote? Sasa si serikali inunue, Kweli hii nchi ya vioja.
 
Serikali isifanye kosa la kununua hizo korosho kwa wakulima. Italiingiza Taifa kwenye hasara.

Pia, wakulima wa mazao mengine watahoji kwa nini korosho tu?
Walilikoroga acha walinywe usiwazindue ili na sisi wakulina wa mahindi tuwakabe koo.
 
Haya madini mwaka huu, yatashinda hata makinikia!
Naamini wakulima wangefahamu (Elimu) tangu wanazalisha na mazingira ya soko wangeuza tu. Tatizo kuna siri nyingi kwa mkulima kuhusu anacholima. Mfano kama angefahamu bei ya soko mwaka jana angelinganisha mwaka huu, utata usingekuwepo. wakulima niwaeelewa sana ila wanahitaji mwongozo.
 
Back
Top Bottom