Serikali yatoa muda mpaka saa 12 jioni kwa mawaziri wasiopeleka tamko la mali watakuwa wamejiondoa



Rais John Pombe Magufuli ametoa muda mpaka leo jioni kwa Mawazri wa 4 na Naibu waziri 1 ambao hawajarejesha fomu kwa Sekretarieti ya maadili kwa ajili ya kuanisha mali na madeni wanayodaiwa ambapo wamepewa muda mpaka saa 12 wawe wamesharejesha fomu hizo.

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataja majina mawaziri hao kuwa ni
Agustine Mahiga
Charles Kitwanga,
January Makamba,
Joyce Ndali Chako na
Naibu waziri Mh.Luhaga Mpina.
=======
Jana nilikabidhiwa majina ya mawaziri na manaibu mawaziri ambao hawakuweza kurudisha fomu zote mbili au fomu moja
.


Hao wengine bila shaka hawakujua taratibu isipokuwa Januar Makamba ambaye alikuwa ktk baraza la mawaziri lililopita na anajua kuwa huo ni utaratibu wa kawaida. Hivi ndg wasomaji wa JF tangu utaratibu huu umeanza kutumika nchini mlishawahi kusikia kiongozi aliyewajibishwa kwa kujirimbikizia mali?
 
Kama kuna waziri ama naibu kamsimamisha mtendaji wa chini yake kwa sababu ya utendaji usioridhisha basi na wao wanapaswa kufanyiwa hivyo hivyo.Waziri ndio taswira ya Wizara kama waziri huwezi kuzingatia matakwa ya sheria zote za nchi ina maana utendaji wako wa kazi hauridhishi na unapaswa kutumbuliwa. Sheria inawataka kujaza na kurudisha form tume ndani ya siku 30 tangu uteuzi ulipofanyika..Tunaongelea siku zaidi ya 50... Mtendaji wa chini asipotii amri yenu ndani ya muda stahiki hamtakuwa na moral authority ya kuwa wajibisha
 
Hivi inakuwa ni suala la kuorodhesha mali tu basi au ukiorodhesha huwa zinafuatiliwa pia kujua uhalali na ukweli wake.

Najiuliza sana swali hili, lakini pia tume ya maadili ingeanza kutoa tathmini ya uzalendo wa viongozi waliomaliza muda wao ili kujua kama mienendo yao ilikuwa safi ktk utumishi
 
Re
Rais John Pombe Magufuli ametoa muda mpaka leo jioni kwa Mawazri wa 4 na Naibu waziri 1 ambao hawajarejesha fomu kwa Sekrtariati ya maadili kwa ajili ya kuanisha mali na madeni wanayodaiwa ambapo wamepewa muda mpaka saa 12 wawe wamesharejesha fomu hizo.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataja majina mawaziri hao kuwa ni Agustine Mahiga,Charles Kitwanga,January Makamba,Joyce Ndali Chako na Naibu waziri Mh.Luhaga Mpina.
Real G=Kibo10...confirmed by IP address
 
Sidhani kama itampa shida sana, kwasababu atadanganya na hakuna wa kuthibitisha vinginevyo au atazificha kwa muda kwa jina la dada yake.
Ila kwa jinsi alivyo Magufuli nadhani hatua itayofuata baada ya uandikishaji itakuwa ni uchunguzi wa taarifa hizo za kumiliki mali kama ni za kweli.
Bado unaishi jana na unaomba mambo yasibadilike ili upate cha kusema!
 
Ziwekwe hadharani hizo fomu.Kuna mali zao nyingi wananchi wanazijuwa na zitakuwa hazipo kwenye fomu.Nina wasiwasi kama Mh...........atarudisha hizo fomu by saa 12 jioni leo.
 
Hawakutakiwa kupewa muda, kama walishindwa kuwakilisha kwa wakati muafaka, wangetumbuliwa tu ili tuwe na imani utumbuaji hata kwa alio waweka yeye unawezekana.
 
Sijui kwanini nimejikuta namuwazia Pinda. Naweza kubet kuwa hapo alipo anatamani angekuwa Waziri Mkuu ktk kipindi hiki kuliko awamu ya 4. Maana angeshainishwa na Magufuli
 
magufuli1.jpg

Rais John Pombe Magufuli ametoa muda mpaka leo jioni kwa Mawazri wa 4 na Naibu waziri 1 ambao hawajarejesha fomu kwa Sekretarieti ya maadili kwa ajili ya kuainisha mali na madeni wanayodaiwa ambapo wamepewa muda mpaka saa 12 wawe wamesharejesha fomu hizo.

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataja majina mawaziri hao kuwa ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Dk Agustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Wa Rais Mazingira na Muungano Mh.January Makamba, Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina.
 
Wengine sina mashaka nao. Ila huyu Januari Makamba inawezekana kuna usanii amefanya na ndo maana hataki kujaza hizo fomu
Ulipata moja ya zile smartphones alizogawia wajumbe wote WA mkutano mkuu wa UVCCM?
 
kumekucha hongera jpm hii ni awamu mpya na mambo mapya wasioweza kwenda na kasi yako wakae pembeni.

naamini wasiokupigia kura wanajuta mioyoni mwao hongera jpm.
me sijampigia na sijutii aslan.. ni nguvu ya togwa
 
Back
Top Bottom