Serikali yatangaza majina ya waliochaguliwa kujiunga na mafunzo rekebishi (bridging course) kwa chuo

nyakahanga

JF-Expert Member
Mar 7, 2013
240
56
ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO MAALUMU REKEBISHI
(BRIDGING COURSE) YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI KATIKA CHUO CHA UALIMU MONDULI
MWAKA WA MASOMO 2014/2015.
Wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo haya wanatakiwa kuripoti Chuo
cha Ualimu Monduli kuanzia tarehe
14/07/2014 hadi 15/07/2014.
MAELEKEZO MUHIMU
Wanafunzi wanatakiwa kufika chuoni wakiwa na mahitaji yafuatayo:-
1. Vyeti halisi vya Baraza la Mitihani la Tanzania vya Kidato cha NNE na SITA;
2. Sare ya Chuo (Shati/Blauzi nyeupe mikono
mirefu:Suruali/sketi: koti na tai rangi ya “dark blue”); na
3. Fedha za tahadhari chuoni na matumizi binafsi.
Usajili wa waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo utafungwa terehe 18/07/2014 saa 12.00 jioni.

Kuona majina pitia hapa www.moe.go.tz/indexphp?option=com_c...rekebishi-bridging-course&catid=1:latest-news
 
mkuu vipi kuhusu ya waliochaguliwa vyuo vingine?maana walisema kuna monduli,morogoro,butimba na vingine jumla vilikuwa kama sita au vitano hivi,sasa nashangaa wametoa ya monduli pekee
 
mkuu vipi kuhusu ya waliochaguliwa vyuo vingine?maana walisema kuna monduli,morogoro,butimba na vingine jumla vilikuwa kama sita au vitano hivi,sasa nashangaa wametoa ya monduli pekee

Mkuu wametoa wale wa mafunzo ya rekebishi yaani waliokuwa na sifa pungufu mfano mtu hana principal bali ana subsidiary 2 au 3, wale wenye principals bado hawajatoa
 
Back
Top Bottom