Serikali yashindwa kesi na Wachina walioshtakiwa kwa uvuvi haramu

by ifweero;
Ukweli ni huu acheni upotoshaji...mods tafadhali pandisheni hii post ku balance habari hii

Serikali yashinda kesi ya samaki wa Magufuli
hatimaye serikali imeshinda kesi dhidi ya wavuvi haramu(wale wachina waliokamatwa na meli ikiwa imejaa shehena ya samaki)


Leo mchana serikali imeshinda kesi hiyo...na hukumu ilikuwa hivi:


Watuhumiwa wawili ndio wamekutwa na hatia,wengine wameachiwa huru.


Hawa wawili waliokutwa na hatia mmoja inatakiwa alipe billlion 21 za kitanzania au kwenda jera miaka 20.


Mwingine naye alipe billion 1 au kwenda jera miaka kumi pia ile meli iliyokamatwa, hakimu ameridhia ombi la mawakili wa serikali kuwa itaifishwe na iwe mali ya serikali ya Tanzania. (kwa sasa ile meli ipo hapa nchini, na sehemu iliyopo imeshaanza kuzama....hivyo basi nijukumu la serikali kuhakikisha meli hiyo ama inatengenezwa ama inauzwa mapema iwezekanavyo.

You and mooduke like this.




ifweero huna akili hili bandiko lako ni la TUNTEMEKE la 2012 unalileta tena hapa leo?

Acha Ujinga ww!
 
Last edited by a moderator:
I have never trusted this man called opium. Anapenda sifa na kwa kuwa nasisi tunatoa sifa cheaply these are the fruits we reap. Haya tusubiri chorus nyingine
 
Tatizo la mahakama ya rufaa majaji wote wala rushwa.

Hivi wewe mwanasheria mkuu wa serikali ndiyo hivyo km tumuonavyo...! Juzi anatuingiza machakani anadai kuwa hakuna mtu mamlaka ya kuvunja bunge la katiba na ni jaji huyo huyo...! Wanasheria wachanga wakamsaidia kuwa mwenye mamlaka ya kuunda chombo katika cha kiutendaji ktk tanzania ndiyo mwenye uwezo wa kukivunja. Kadai rais hana uwezo wa kuvunja au kusimamisha bunge la katiba. Mr. Weriiema kichwa boga kabisa.
 
Nafikiri hii kitu ilikuwemo kwenye ile Mikataba zaidi ya 20 aliyosaini kwa kasi Rais wa China wakati wa ziara yake hapo Bongo!
 
Katika watu wachache ambao walisema Magufuli kakurupuka na kutafuta sifa za magazetini kwenye hili sakata ilikuwa ni mimi.

Ingawa sikujuwa uhalali au uharamu wa hii kesi lakini niliona kuwa publicity stunt iliyofanywa na Magufuli ilikuwa kubwa kuliko kiasi.

Nnaamini kuwa mahakama imetenda haki. Sasa tungoje kesi ya madai ya hao walioshikwa na wenye meli, na kila itapocheleweshwa ndio zigo linazidi kuwa kubwa, thamani, gharama za kesi, hasara, faida vyote vinahesabika.

Halafu hao wenye meli wanaweza kuwadai, si Tanzania tu bali na Afrika Kusini na Botswana kwani walishirikiana kuwakamata.
 
Hawa majaji wajinga kwanini hawana uzalendo.c wangefoji tu kesi nakuwapa ushndi tz kuliko kuingiza nch kwenye zgo la deni,ww unafikiri hyo meli garama n bilion ngapi plus samaki plus mda yani ni majanga
 
Sijui kama wengi watakuelewa hapa.
Mkuu MAHORO, kwa unadhani wale watalii waliofika jana kwa jina la Rili Madiridi wanapaswa kutulipa kwa kuja kufaidi kama watalii wengine au tunapaswa kuwalipa kama tulivyofanya!?

... Hahahaaa, Yaani Wamekuja Kutalii Na Bado Tunawalipa? Sijawah Ona Inch Ya Wapumbavu Kama Hii
 
Balozi wa China nchini alishasema kuwa atailinda tz kwa kila hali
 
Tatizo la mahakama ya rufaa majaji wote wala rushwa.

Mkuu MAJAJI hapa hawahusiki. Kilichoandikwa ni kuwa ofisi ya DPP imeamua kutoendelea na kesi hii na kuiondoa chino ya kifungu 91(1) CPA.

Nakushauri andika hivi;

TATIZO LA SERIKALI YA CCM, WOTE NI WALA RUSHWA.
 
Katika watu wachache ambao walisema Magufuli kakurupuka na kutafuta sifa za magazetini kwenye hili sakata ilikuwa ni mimi.

Ingawa sikujuwa uhalali au uharamu wa hii kesi lakini niliona kuwa publicity stunt iliyofanywa na Magufuli ilikuwa kubwa kuliko kiasi.

Nnaamini kuwa mahakama imetenda haki. Sasa tungoje kesi ya madai ya hao walioshikwa na wenye meli, na kila itapocheleweshwa ndio zigo linazidi kuwa kubwa, thamani, gharama za kesi, hasara, faida vyote vinahesabika.

Halafu hao wenye meli wanaweza kuwadai, si Tanzania tu bali na Afrika Kusini na Botswana kwani walishirikiana kuwakamata.

Kwa maana nyingine ni kuwa wewe ungefurahia na unafurahia jinsi Maliasili zetu ziendelee kuporwa?
 
Kama hii habari inaukweli basi kuna sehemu serikali imeteleza na nilazima ije na majibu mazuri lasivyo lazima watu wawajibishwe kwa jambo hili..!
 
Daaah huyu DPP ana biashara gani na RAIA wa kigeni? Sijawahi kumuona akifuta mashtaka kwa waswahili mfano babu seya, liyumba.na wengineo. Ila nimeona akiwafutia mashtaka wahindi wa IMTU na hawa wachina wa meli. Kunani hapa .?
 
Back
Top Bottom