Serikali yasema inashughulikia madai ya Wafanyakazi wa SGR wanaodai malipo ya NSSF

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, David Kihenzile amesema Serikali inafahamu Mkandarasi Mkuu wa Mradi wa Reli ya SGR (Yapi Merkezi) anasuasua kufanya malipo kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa Watumishi na kuwa vikao vinaendelea ili awe anakamilisha malipo mara tu anapolipwa fedha.

Akiongezea majibu ya hoja hiyo, leo Ijumaa Novemba 10, 2023, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Prof. Joyce Ndalichako amesema “Nakiri kweli kuna madai ambayo Mkandarasi anadaiwa na Mfuko unafuatilia, kuna makubaliano kati ya NSSF na Mkandarasi ili madeni yalipwe ndani ya mwaka mmoja pia kuna utaratibu maalumu wa kuwalipa ambao wanastahili kulipwa.”

Hivi karibuni Wadau wa JamiiForums.com waliripoti mara kadhaa kuhusu Mkandarasi kutoingiza malipo ya NSSF na baadaye Yapi ikakiri na kusema inashughulikia changamoto hiyo.

Pia soma:

Mkandarasi Reli ya SGR asema sababu za Wafanyakazi kutoingiziwa malipo ya NSSF ni kwa kuwa kuna makubaliano maalum

Mkandarasi SGR anataka kutupunguza 50% ya Wafanyakazi wakati hajatuingizia fedha za NSSF miezi 9
 
Back
Top Bottom