DOKEZO Mkandarasi SGR anataka kutupunguza 50% ya Wafanyakazi wakati hajatuingizia fedha za NSSF miezi 9

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kwenye mradi wa SGR huku tunapojenga Reli ya Mwendokasi, hadi kufikia Septemba 2023, imetimia miezi 9 pasipo Mkandarasi wa Mradi Yapi Merkezi kutuingizia malipo yetu katika akaunti za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Kwa ufupi ni kuwa tunakatwa fedha za NSSF kila mwezi kwenye mishahara lakini ukiangalia kwenye akaunti ya mfuko mara ya mwisho wapo waliowekewa malipo yao Januari 2023 na wengine Desemba 2022.

Tumejaribu kuhoji hatukuweza kupata majibu, sasa ukifikiria na hili punguzo la Wafanyakazi haşa kwa kipande cha Morogoro hadi Makutupora unadhani tutapata wapi tena hizo haki zetu?

Hawa jamaa wakikufukuza au ukimaliza mkataba na wasipokuongezea mkataba ukiwa bado unadai, tambua kuwa hiyo imekula kwako.

Kuna kipindi walifanya hivi tukapiga kelele mitandaoni wakaanza kutulipa, sasa wamerudia tena mchezo wao na wanakatibia kutuondoa kwenye ajira.

Wamekuwa wakifanya vikao na sisi Wafanyakazi wakidai wanataka kutoa likizo ya miezi mitatu kwa lazima na ambayo haina malipo, ulishaona wapi likizo ya miezi mitatu bila malipo tena ya lazima, maana yake ni kuwa wanataka tupate kazi kwingine kisha unakuwa umejifukuzisha.

Kuondolewa kwenye ajira si jambo geni, lakini kama wanataka kutuondoa basi iwe katika njia sahihi, wasitishe mikataba, watulipe fedha zetu zote, waingize na malipo yetu ya NSSF tuachane kwa amani.

Kingine tunaambiwa Awamu ya Kwanza na ya Pili ya mradi zimekamilika lakini Watanzania hatujiulizi kuwa kwa nini reli hazijaanza kutumia? Kuna vitu havipo sawa, tuamkeni.

Pia soma - Mkandarasi wa anayejenga Reli ya SGR adaiwa kuyumba kifedha, Serikali yatafuta mbadala kukamilisha ujenzi

Serikali yasema inashughulikia madai ya Wafanyakazi wa SGR wanaodai malipo ya NSSF
 
Pole sana mkuu, kila sehemu ni vilio, sisi walimu tumeambiwa tufundishe orientation course had saa 10 na nusu bila malipo
 
Hivi inakuaje Mwajiri hajaingiza pesa NSSF karibia na shirika husika halifuatilii??
Au wanakua hawajui
Na je kama wanajua hakuna hatua za kinidhamu za kuchukua kwa waajiri hao?
 
Hivi inakuaje Mwajiri hajaingiza pesa NSSF karibia na shirika husika halifuatilii??
Au wanakua hawajui
Na je kama wanajua hakuna hatua za kinidhamu za kuchukua kwa waajiri hao?
Huu uhuni nilifikiri ni kwa ngozi nyeusi tu kumbe haungalii rangi.

Kuna dogo alikua anafanya kazi kwenye taasisi fulani hawajawekewa michango yao tangu mwaka 2022 , hakuna likizo , hakuna posho yoyote ile (responsibility allowance & extra duty allowance) kazi yenyewe wanafanyishwa saa 1 hadi 12 jioni na hii wamefanyiwa miaka 3 mfululizo muda mwingine hadi weekend , vikao visivyo na ratiba maalum wala tija yoyote hadi vya usiku.

Na boss wa hiyo taasisi ni muajiriwa serikalini na anazijua taratibu ila hafuati hivyo kwenye taasisi yake binafsi aliyoanzisha kajaza ndugu tu incompetetent kazi yao kumpelekea umbea tu.

Mwisho wa siku watu 3 wakasubmit barua za kuresign siku moja kwa pamoja ndio boss anatoka pangoni kujidai wayaweke sawa nikamwambia dogo kaza hakuna kurudi nyuma.

Ajabu ni kuwa hata baada ya kuresign madeni yao ya miaka 2 nyuma hawajalipwa na hata NSSF michango yao haijalipwa, hapa nikagundua NSSF ndio kuna tatizo kuside na hawa maboss .

Boss mwenyewe huwa nikimuona kwenye platform za kitaifa ambapo huwa ni mshiriki mzuri tu sura na kuongea kwake huwezi mdhania ndio rough anazowafanyia vijana wadogo wakiwa kwenye rika la utafutaji.
 
Back
Top Bottom