Serikali yarejesha kodi kinyemela kwenye allowance zote!

Rungu la KODI kwa wafanyakazi limerejeshwa tena kinyemela bila hata kutangazwa na waziri wa fedha kwenye hotuba ya bajeti! Allwance zote zitakatwa kodi kama zamani na TRA tayari wameanza kusambaza majedwali yenye kanuni mpya ya kufyeka mishahara ya watumishi wa serikali na mashirika yake bila hata huruma! Danganya toto ya kupandisha mishahara itaishia kwenye mlolongo wa makodi katika kila bidhaa na mfumuko wa bei ambao hadi hii leo BOT hawana takwimu halisi! Tunakwenda wp?
Viwango vya kodi kwa watu binafsi wakazi kuanzia tarehe 1/7/2012

hii ni kweli na msala si mchezo
ISO 9001:2008 CERTIFIEDVIWANGO VYA KODI KWA WATU BINAFSI WAKAZI KUANZIA TAREHE 1/7/2012 KWA MUJIBU WA MUSWADA WA SHERIA YA FEDHA YA MWAKA 2012
Mapato kwa mwezi Kiwango cha kodi
Mapato yasiyozidi shs 170,000/=Yamesamehewa
Mapato yanayozidi shs 170,000/= lakini hayazidi sh. 360,000/=14% ya kiasi kinachozidi sh 170,000/=
Mapato yanayozidi sh. 360,000lakini hayazidi sh. 540,000/=Sh. 26,600/= ongeza 20% ya kiasi kinachozidi sh 360,000/=
Mapato yanayozidi sh. 540,000/= lakini hayazidi sh. 720,000/=Sh. 62,600/= ongeza 25% ya kiasi kinachozidi sh 540,000/=
Mapato yanayozidi sh 720,000/=Sh 107,600/= ongeza 30% ya kiasi kinachozidi sh 720,000/=
1. Mapato ya mwajiriwa kwa mwezi ni pamoja na mshahara , ujira kwa kazi za ziada , bonasi, kamisheni, malipo kwa ajiri ya nyumba, usafiri na malipo mengine ya ajira baada ya kuondoa michango ya akiba ya uzeeni inayokubalika (mfano NSSF au PPF)) 2. Mapato kwa mwaka yasiyotozwa kodi ni Sh 2,040,000 /=3. Viwango vya kodi kwa Zanzibar : Waziri wa Fedha atashauriana na Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

ni kweli
 
Watanzania tunapelekwa wapi? Sheria kandamizi kwa wananchi haziishi, wakati wa kuchukua hatua ni sasa vijana tuamke ktk kulikombo jahazi linaloendelea kuzama
 
MTAANI

ACTION RESPONSE
Kusonywa.........kimyaaaaaaaaaa
Kuzodolewa.......kimyaaaaaaaaaaaaa
Kutukanwa........kimyaaaaaaaaaaaaaaa

OFISINI
ACTION RESPONSE
Low pay...........kimyaaaaaaaaa
Pension............Kimyaaaaaaaaaaaaa
Paye................kimyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Kamanda KOVA atatuambia hili suala liko mahakamani halipaswi kujadiliwa, hii nchi kila eneo mgogoro! Waalimu mgogoro, maDR gogoro, Timu ya taifa gogoro, NSSF dhoruba usafiri wa ndege balaa, usafiri wa treni network haisomeki, usafiri wa majini muamala hausomi, ofisi za magogoni raaamustarehe!!! Bata kwenda mbele!
 
Rungu la KODI kwa wafanyakazi limerejeshwa tena kinyemela bila hata kutangazwa na waziri wa fedha kwenye hotuba ya bajeti! Allwance zote zitakatwa kodi kama zamani na TRA tayari wameanza kusambaza majedwali yenye kanuni mpya ya kufyeka mishahara ya watumishi wa serikali na mashirika yake bila hata huruma! Danganya toto ya kupandisha mishahara itaishia kwenye mlolongo wa makodi katika kila bidhaa na mfumuko wa bei ambao hadi hii leo BOT hawana takwimu halisi! Tunakwenda wp?

Acha uongo mkuu...jedwali zinazotolewa ni kwa ajili ya new rates kutokana na mabadiliko ya sheria kutoka kima cha chini 135000 hadi 170000 hivyo kuna unafuu kidogo..hakuna allowance kwa watumishi wa serikali ambazo zinatozwa kodi bado zipo exempted..isipokuwa watumishi wa sekta binafsi wao hawako exempted kwenye hizo allowances..muda mwingine tafuta taarifa iliyo sahihi..
 
Mwakajila@ ww ni ni miongoni mwa magamba! Allowance zote zimerejeshwa kwenye utaratibu wa kodi! Na ile 1% ya unafuu kwenye PAYE imerudishwa! Rungu la KODI limerudi tena! Acha upotoshaji! Kasome waraka mpya wa hazina
 
Rungu la KODI kwa wafanyakazi limerejeshwa tena kinyemela bila hata kutangazwa na waziri wa fedha kwenye hotuba ya bajeti! Allwance zote zitakatwa kodi kama zamani na TRA tayari wameanza kusambaza majedwali yenye kanuni mpya ya kufyeka mishahara ya watumishi wa serikali na mashirika yake bila hata huruma! Danganya toto ya kupandisha mishahara itaishia kwenye mlolongo wa makodi katika kila bidhaa na mfumuko wa bei ambao hadi hii leo BOT hawana takwimu halisi! Tunakwenda wp?

hata hao wanaotupa misaada wanatoza kodi kwenye allowances mkuu. Kwa mfano nchi kama Canada Hadi wafanyakazi wanajidhibiti kufanya overtime kwa kuwa kodi inakuwa kubwa kuliko unayobaki nayo. Issue hapa ni inflation mkubwa wangu.
 
Hairuhusiwi kujadiliwa, viache vyombo vya kisheria vinashughulikia
Mbona unazuia kujadili maslahi ya wafanyakazi ama wewe ndugu yangu hujui vyombo vya sheria vya TZ ni vya kulinda maslahi ya tabaka fulani? Usizuie hoja nzito kama hizi ndugu tafadhali tafadhali maana machungu ya KODI twayajua sie bana
 
Rungu la KODI kwa wafanyakazi limerejeshwa tena kinyemela bila hata kutangazwa na waziri wa fedha kwenye hotuba ya bajeti! Allwance zote zitakatwa kodi kama zamani na TRA tayari wameanza kusambaza majedwali yenye kanuni mpya ya kufyeka mishahara ya watumishi wa serikali na mashirika yake bila hata huruma! Danganya toto ya kupandisha mishahara itaishia kwenye mlolongo wa makodi katika kila bidhaa na mfumuko wa bei ambao hadi hii leo BOT hawana takwimu halisi! Tunakwenda wp?

Kweli hujuhi au ? unataka tupandishe jazba?
 
Back
Top Bottom