Hao madaktari wasifikiri wao ndio wanatoa uhai. Kwanza wengi wao ni interns, sasa watajuwa kuwa Serikali ina mkono mrefu.
Hiyo mikutano yao kwa sasa ni haramu, imeshapigwa marufuku na Serikali, Ilikuwa wakutane na Waziri Mkuu leo, kilichowafaya wasiende ni nini?
Hao wengine wanajiharibia maisha yao kwa kudanganywa na kuchotwa na akili na kundi dogo la watu.
Hao madaktari wasifikiri wao ndio wanatoa uhai. Kwanza wengi wao ni interns, sasa watajuwa kuwa Serikali ina mkono mrefu.
Serekali iwatimue tu,
Msikusanyike mahali popote bakini majumbani kwenu wekeni extreme ya SMS kisha muwe mnawasiliana. Hakuna sababu ya kubishana na watu wasio na upeo wa kutatua mambo, Nangojea siku hao FFU wakigoma sijui nani ataenda kuzuia mgomo?
Kweli mama? Una ubongo wewe?wakishaenda kulima. Je sisi wagonjwa twende wapi?au tusubiri kuvuna? Kweli nimetambua una roho mbaya sana. Roho mbaya sana hasa hasa kwa mwanamke anayestahili kuitwa Mama!Na kesho kama hawakwenda vituoni ndio wamejifukuzisha kazi. Namuunga mkono Pinda mia kwa mia.
Tena wasipewe leseni kabisa za kufanya hizyo hapa Tanzania, wakatafute pakufanyia au wakalime, hiyo kazi hawaiwezi kabisa.
Serikali imeendelea kuongeza juhudi zake za kuwabana madaktari na sasa imenyang'anya ukumbi wa starlight
na wameamua kuulinda na FFU kama walivyowahamisha pale Don Bosco na kumbi zingine za Korean Culture na
Diamond ili kuendeleza juhudi zake za kukandamiza wananchi wake ndani ya nchi yao.
pinda hana akili kabisa huyu....
Posho za wabunge zimetoka kwenye budget ipi?
Pumbaf!!
Wakati doctors wana-seek audience na serikali, serikali ilikiwa likizo. Sasa hivi wanachukua masaa matatu kueleza utumbo wao hapa.
kutaneni majumbani kwenu kama kuna mmjoja wenu ananyumba yenye eneo, msikate tamaa mpaka kieleweke
Hakuna kazi isiyo na sulubu zake, ndio maana inaitwa kazi. Wao ndio kazi yao na wewe unaweza kuwa unaona ya kutisha wao wanaona ni kawaida tu.
Lakini hili la kufanya dharau kwa Serikali, hatuliungi mkono hata kidogo, wangekwenda kusikiliza kama hawajaridhika wangesema hilo hapana, ndio mambo yanavyokwenda, sio kususa, wanasusa nini? hawajajifunza kutoka kwa wasusaji wakuu walipoamuwa kususuka?
Issue ya madaktari iangaliwe katika mitizamo miwili, tunahitaji madaktari kuokoa maisha ya wagonjwa wetu na pili wanatakiwa kusikilizwa kuhusu madai yao. Pinda yuko sahihi kuwaambia warudi sehemu zao za kazi na matatizo yao yatafanyiwa kazi kupitia viongozi wao, sasa madaktari wanatakiwa kusikiliza kiongozi wao anasema nini! Kama kiongozi anakubaliana na serikali na wamewekeana muda wa kutatua hili tatizo, kama halitafanyiwa kazi hapo wanaweza kuendeleza mgomo. Sidhani kama ni busara wazidi kushinikiza serikali ili hali wagonjwa wanakosa tiba hata kufariki. Kama Pinda ametoa vitisho kweli basi hatakuwa na busara hata kidogo katika kutatua matatizo, na kuweka FFU siyo sahihi kama watakuwa wanajadiliana kuhusu yaliyotokea leo au kumsikiliza kiongozi siyo tatizo. Uchumi wa nchi uko vibaya na serikali haina hela, yote haya si waziri mkuu au raisi kusema walipwe sijui 3.5m hii inatakiwa wizara muhimu kama utumishi, fedha, afya, hazina sikae chini na kuona kama revenues, government spending zitakuwa sustainable... wanaosema raisi anatumia milioni 300 kwa safari madaktari wangepewa, leo wakipewa mwezi kesho zitatoka wapi? ya wabunge si issue ya leo walishakaa chini na wakajua hela itatoka wapi. UCHUMI MBAYA NA SERIKALI HAINA HELA, mambo yakiendelea hivi tutaingia kwenye hatua ambayo hata hao wanaolipwa kidogo hawatapa. Mungu ibariki Tanzania.
Kama serikali inadhani kwa kuzuia madaktari wasiruhusiwe kukutana kwenye kumbi ndio dawa, hii ndio serikali ya abunuwasi kwani haina hata fikara kuwa hawa madaktari wasomi na kila mmoja wao mpaka sasa ana simu ya mkononi kwahiyo wanaweza kuwasiliana na kupeana habari kwa njia ya simu bila ya kukutana na wakafanikisha mikakati yao!! They do not even follow the world events to know how the Arab spring succeeded!! Madaktari pashaneni habari kwa kutumia simu na internet basi.