Serikali yamtaka Luhaga Mpina Kuomba na kupata Ufafanuzi kwa Serikali kabla ya kuzungumza mambo yasiyo na ukweli hadharani

Kwa hiyo huo mbango ndio ushahidi ? Ndio ushahidi unaoweza kumtia mtu hatiani mahakamani?
Nani mlishampeleka mahakamani kwa wizi?

Yani wezi wapeleke mahakamani wezi?

Hii ni ripoti ya CAG aliyopokea Samia hizo pesa zilizopotea nani alifikishwa mahakamani?.

Yani watu wanakuja na matokeo ya tafiti unaita bango?
images (20).jpeg
 
Ndugu zangu Watanzania,

Siku chache baada ya Mheshimiwa Luhaga Mpina kuzungumza hadharani na kulaumu au kutoa shutuma zinazoonyesha matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kununua vifaa vya kuongeza makalio badala ya kutumia pesa hizo kutoa huduma kwa wananchi.

Serikali kupitia naibu waziri wa afya mheshimiwa Godwini Mollel imejitokeza hadharani na kutoa ufafanuzi wa kina wa kusikitishwa sana na habari za Luhaga Mpina ambazo kwa kiasi kikubwa zilikuwa za upotoshaji na zenye kukosa ukweli.

Mheshimiwa Naibu waziri amesema kuwa siyo kweli kuwa serikali ilitoa pesa kwa ajili ya kununua vifaa kwa ajili ya kurekebisha au kufanyia watu huduma kama alivyodai Mh Luhaga Mpina.bali huduma hiyo ya plastic surgery ipo na imekuwepo muda tangia serikali ya CCM ilipoamua kuwekeza pesa za kutosha kwa ajili ya kununua vifaa tiba pamoja na kuandaa wataalamu wa kutosha.

Amesema ya kuwa plastic surgery hufanyika pale mtu anapokuwa amepata matatizo yanayotokana na kuumia sana kunakoweza kuwa kumetokana na kusababishwa na ajali .mfano mtu anaweza akapata ajali halafu akajikuta mkono wote umetoka nyama zote na kubaki mifupa tu au mtu ameumia ambapo eneo la lipsi za juu za mdomo imetoka yote na kubaki meno tu.hivyo kinachofanyika ni kumsaidia mhusika kurejea katika hali yake ya awali kwa kumfanyia plastic surgery kwa kuchukua nyama kutoka sehemu nyingine za mwili wake na kuweke eneo lililopata jeraha .

Amesema huduma hizi awali wagonjwa wa aina hii walikuwa wanakwenda kupata huduma huko uturuki au india na maeneo mbalimbali nje ya nchi.jambo ambalo lilikuwa linapunguza hata hazina yetu ya pesa za kigeni. Hivyo serikali yetu katika kutatua changamoto hiyo ikaona ifanye uwekezaji wa kununua vifaa tiba ili huduma hizo zipatikane hapa hapa nchini na watu watibiwe hapa hapa kwa gharama rafiki hasa kwa wanyonge wanaotokea maeneo mbalimbali nchini.na hivyo pesa kubakia hapa hapa nchini kwaajili ya kuwasaidia Watanzania wanyonge wengine.

Amefafanua kuwa hata huduma ya kuongeza au kurekebisha au kurejesha katika hali ya awali makalio ni sehemu ya huduma ambayo inapatikana na kufanyika kwa kutumia vifaa tiba hivyo hivyo vilivyokuwepo na siyo kwamba kuna pesa iliyotolewa wakati huu kwa ajili ya kununua vifaa maalum kwa ajili ya kazi hiyo ya kurekebisha makalio..

Rai yangu ni kuwa ningemuomba na kumsihi Mheshimiwa Luhaga Mpina kuacha kuleta Taharuki na kuichonganisha serikali yetu na wananchi kwa maneno na takwimu zinazokuwa hazina ukweli wowote .mfano suala na madai yake ya kusema kuwa kuna wizi au ufisadi wa zaidi ya Trilioni 30 ni jambo ambalo haliingii akili hata kidogo.yaani bajeti yetu ni Trilioni 44 halafu kufanyike ufisadi na wizi wa Trilioni 30?

Hivi serikali ingewezaje kuendelea kulipa mishahara kwa watumishi wa umma? Ingewezaje kujenga miradi ? Ingewezaje kutoa ajira? Ingewezaje kulipa wakandarasi madai yao? Ingewezaje kukamilisha mradi wa bwawa la mwalimu Nyerere? Ingewezaje kutoa na kugharamia elimu bure hapa nchini? Ingewezaje kujenga shule mpya, zahanati na vituo vya afya kila kona ya nchi yetu?

Ingetoa wapi hizo pesa za kufanya yote hayo wakati Trilioni 30 zimeibiwa? Kwanini yeye kama mbunge na mtu aliyewahi kuwa waziri asingeomba ufafanuzi kwa serikali ambapo anayo nafasi ya kuonana na waziri yeyote yule kuomba majibu ya jambo lolote lile? Hili suala la plastic surgery Kama angewasiliana na serikali na kuomba muongoza si angekuwa amepata majibu na kutokuleta upotoshaji kwa umma?

Kwanini anapenda muda wote kutoa maneno yenye dhamira ya kutaka watu waichukie serikali yetu na kuonekana kana kwamba rushwa na Vitendo vya rushwa vimeshamiri sana wakati huu? Kwanini anakuwa anatoa takwimu na vitu visivyo na ukweli na vinavyoleta sintofahamu katika jamii? ieleweke kuwa mimi sipingi kuwa asikosoe serikali bali napinga kuzungumza vitu bila kuwa na uhakika na ushahidi wa kutosha na wenye ukweli .

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Mkuu utetezi wa mollel ni dhaifu sana angekaa kimya kuficha aibu!
 
Kivipi ni dhaifu na ni dhaifu katika hoja zipi. Vifaa vya plastic surgery vilivyokuwa vinatumika awali ndio hivyo hivyo vinatumika katika au kwa watu wanaohitaji kurekebisha makalio yao iwe ni kwa kuyaongeza au vyovyote vile watakavyo.
 
Tumia akili kuelewa kuwa huduma hiyo sasa inapatikana lakini kwa kutumia vifaa tiba ambavyo tayari vilikuwepo na vinatumika katika masuala yote ya plastic surgery .na siyo kwamba kuna vifaa vipya vilivyonunuliwa maalum kwa ajili ya kazi hiyo ya kurekebisha makalio.
Kwa hiyo makalio kwanza mengine baadae? Wazazi wetu wanajifungulia sakafuni ila serikali ikaona kuliko kununua vitanda ni heri kuwekeza kwenye matako?
 
Kivipi ni dhaifu na ni dhaifu katika hoja zipi. Vifaa vya plastic surgery vilivyokuwa vinatumika awali ndio hivyo hivyo vinatumika katika au kwa watu wanaohitaji kurekebisha makalio yao iwe ni kwa kuyaongeza au vyovyote vile watakavyo.
Tumeona wengi walifanyiwa hizo surgery huku mtaani maarufu walikuwa wanasema kawekea nyama ya tako walifanyiwa hapa hapa nchini ila mollel kusema watu walikuwa wanakwenda india au uturuki si kweli labda wenye pesa,
Na wenyewe serikali ndio walioanza promo wenye kutaka kurekebishwa shepu sasa huduma ipo hapa hapa nchini mbona hatujuyasikia hayo kabla wawe wakweli baada ya kusikia watu wanalipa pesa ndefu kuweka makalio serikali kupitia wizara ya afya wakaona watumie fursa kwa kununua vifaa wafanye biashara nashangaa Mollel anatoa maelezo meeeengi!
 
Ndugu zangu Watanzania,

Siku chache baada ya Mheshimiwa Luhaga Mpina kuzungumza hadharani na kulaumu au kutoa shutuma zinazoonyesha matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kununua vifaa vya kuongeza makalio badala ya kutumia pesa hizo kutoa huduma kwa wananchi.

Serikali kupitia naibu waziri wa afya mheshimiwa Godwini Mollel imejitokeza hadharani na kutoa ufafanuzi wa kina wa kusikitishwa sana na habari za Luhaga Mpina ambazo kwa kiasi kikubwa zilikuwa za upotoshaji na zenye kukosa ukweli.

Mheshimiwa Naibu waziri amesema kuwa siyo kweli kuwa serikali ilitoa pesa kwa ajili ya kununua vifaa kwa ajili ya kurekebisha au kufanyia watu huduma kama alivyodai Mh Luhaga Mpina.bali huduma hiyo ya plastic surgery ipo na imekuwepo muda tangia serikali ya CCM ilipoamua kuwekeza pesa za kutosha kwa ajili ya kununua vifaa tiba pamoja na kuandaa wataalamu wa kutosha.

Amesema ya kuwa plastic surgery hufanyika pale mtu anapokuwa amepata matatizo yanayotokana na kuumia sana kunakoweza kuwa kumetokana na kusababishwa na ajali .mfano mtu anaweza akapata ajali halafu akajikuta mkono wote umetoka nyama zote na kubaki mifupa tu au mtu ameumia ambapo eneo la lipsi za juu za mdomo imetoka yote na kubaki meno tu.hivyo kinachofanyika ni kumsaidia mhusika kurejea katika hali yake ya awali kwa kumfanyia plastic surgery kwa kuchukua nyama kutoka sehemu nyingine za mwili wake na kuweke eneo lililopata jeraha .

Amesema huduma hizi awali wagonjwa wa aina hii walikuwa wanakwenda kupata huduma huko uturuki au india na maeneo mbalimbali nje ya nchi.jambo ambalo lilikuwa linapunguza hata hazina yetu ya pesa za kigeni. Hivyo serikali yetu katika kutatua changamoto hiyo ikaona ifanye uwekezaji wa kununua vifaa tiba ili huduma hizo zipatikane hapa hapa nchini na watu watibiwe hapa hapa kwa gharama rafiki hasa kwa wanyonge wanaotokea maeneo mbalimbali nchini.na hivyo pesa kubakia hapa hapa nchini kwaajili ya kuwasaidia Watanzania wanyonge wengine.

Amefafanua kuwa hata huduma ya kuongeza au kurekebisha au kurejesha katika hali ya awali makalio ni sehemu ya huduma ambayo inapatikana na kufanyika kwa kutumia vifaa tiba hivyo hivyo vilivyokuwepo na siyo kwamba kuna pesa iliyotolewa wakati huu kwa ajili ya kununua vifaa maalum kwa ajili ya kazi hiyo ya kurekebisha makalio..

Rai yangu ni kuwa ningemuomba na kumsihi Mheshimiwa Luhaga Mpina kuacha kuleta Taharuki na kuichonganisha serikali yetu na wananchi kwa maneno na takwimu zinazokuwa hazina ukweli wowote .mfano suala na madai yake ya kusema kuwa kuna wizi au ufisadi wa zaidi ya Trilioni 30 ni jambo ambalo haliingii akili hata kidogo.yaani bajeti yetu ni Trilioni 44 halafu kufanyike ufisadi na wizi wa Trilioni 30?

Hivi serikali ingewezaje kuendelea kulipa mishahara kwa watumishi wa umma? Ingewezaje kujenga miradi ? Ingewezaje kutoa ajira? Ingewezaje kulipa wakandarasi madai yao? Ingewezaje kukamilisha mradi wa bwawa la mwalimu Nyerere? Ingewezaje kutoa na kugharamia elimu bure hapa nchini? Ingewezaje kujenga shule mpya, zahanati na vituo vya afya kila kona ya nchi yetu?

Ingetoa wapi hizo pesa za kufanya yote hayo wakati Trilioni 30 zimeibiwa? Kwanini yeye kama mbunge na mtu aliyewahi kuwa waziri asingeomba ufafanuzi kwa serikali ambapo anayo nafasi ya kuonana na waziri yeyote yule kuomba majibu ya jambo lolote lile? Hili suala la plastic surgery Kama angewasiliana na serikali na kuomba muongoza si angekuwa amepata majibu na kutokuleta upotoshaji kwa umma?

Kwanini anapenda muda wote kutoa maneno yenye dhamira ya kutaka watu waichukie serikali yetu na kuonekana kana kwamba rushwa na Vitendo vya rushwa vimeshamiri sana wakati huu? Kwanini anakuwa anatoa takwimu na vitu visivyo na ukweli na vinavyoleta sintofahamu katika jamii? ieleweke kuwa mimi sipingi kuwa asikosoe serikali bali napinga kuzungumza vitu bila kuwa na uhakika na ushahidi wa kutosha na wenye ukweli .

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.

View: https://youtu.be/CwuDTuTXLS8?si=gk59OFFIcZwntzZi

Pia soma Luhaga Mpina: Pesa za Kununua Mashine za Kuongeza Makalio Mloganzila zimetoka wapi?

Huyu tumesha malizana nae Kisesa ,anajua ubunge mwisho 2025 ,hivyo basi mfa maji kutapatapa lazima.
 
Back
Top Bottom