Serikali yakwaa kisiki Hospitali binafsi!

hospitali x .....kama selikali inaweza kulipia wagonjwa huku private kwanini wasitumie pesa hizo kulipa madaktari? :
hospitali y ......andiken contract vinginevyo no, hospitali hizi zinajiendesha kibiashara.
Hospitali z........haijatoa jibu

acha uongo, hiyo point ya kwanza nakwambia hakuna management ya hospitali yoyote hapa tanzania inaweza kuijibu serikali hivyo, kama una ushahidi lete! Kama hawajarudishwa kwao india, unafanya mchezo nini?"
 
Lakini inakubidi utambue ya kuwa, hao waliopo private ndiyo walewale wa serikalini. Wengi katika muda wao binafsi huwa wanapractiz huko private. Na walio private jumla ndiyo kina Dr.Ulimboka. Sasa wameamua kubana kotekote.


Unaongea kitu ambacho hukijui, madaktari wa Muhimbili wanaenda Private Hospitals wakati wa Clinics zao. Wao si Wamiliki. lete ushahidi. Kwani Hujui kuwa Regency ni ya Dr. Kanabhai, Agakhan ni ya Aga Khan Group, TMJ, Kairuki si unajua? Tumaini ndo ya madaktari wachache walioungana na kuanzisha ile hospital. NAkwambia tena, hakuma hata Management Moja ya Hospitals za BINAFSI ZINA GUTS ZA KUIJIBU SERIKALI HIVYO.
 
Una uhakika Rwanda inafanya vizuri? Fanya utafiti kwanza acha hisia za kibubusa

Rwanda wanaiba madini ya kongo drc kwa fujo na wanachochea vita na kuingizas majeshi yao kubeba dhahabu na almasi wala si watu wa kusifia maendeleo ya ujambazi hapa
 
I was waiting to see the miracles!! Watajinyanyua, kama vipi wazifutie vibali hospitali binafsi ili waoneshe ubabe wao vizuri.

Hahaha wakifuta vibali kweli ndio watadhihirisha udhaifu wao...maana mwisho wa siku hakutakua hata na hizo hospitali chache.
Kimsingi Kikwete na serikali yake kashikwa pabaya, kiplotokali hawezi kukubali hili ila huo ndio ukweli.
Hii ishu hivi kwa nini wale wana Kidjo-Bisimba wasimsemelee huyu kilaza kwa wahisani kuwa anakiuka haki za binadamu?
Walau awekewe vikwazo , wenye nchi tuamue hatma yetu.
 
Wakurugenzi wa hospitali binafsi wamegoma kubeba mzigo wa serikali wa kuchukua wagonjwa kutoka hospitali za Public zilizoathiriwa na mgomo.

Serikali yapata jibu la kejeli... "Kama mnaweza kuwalipia wagonjwa private kwanini fedha hizo msitumie kuwalipa madaktari?"

bora wameiambia serikali ukweli!
Kuishi chini ya serikali inayoongozwa na dhaifu ni balaa tupu!
 
Wakurugenzi wa hospital hizo binafsi wakikubali tu wameingia mtego, serikali yenyewe pesa itatoa wapi za kuwalipia wagonjwa wote nchi nzima ukizingatia gharama za hospital hizo ziko juu? watakopwa mwisho wa siku kulipana itakuwa kimbembe. Hata hao madaktari wa kigeni wanadhani watakubali kulipwa madafu wakati wao ni experts(TX)..

Hebu oneni jinsi mwisho wakufikiri wa magamba ulipofikia mwisho, yaani raisi alikaa na baraza la mawaziri suluhisho wakaona ni kuagiza madaktari kutoka nje na kupeleka wagonjwa hospitali za binafsi? Jambo ambalo hata mtendaji wa kijiji ukimuuliza anaona mgomo unaweza kumalizwa vipi atakupa majibu swafi..Ama kweli sasa hivi nchi hii inahitaji AKILI YA JUU ZAIDI AMBAYO HAIPATIKANI MAGAMBA kuweza kutatua matatizo yake.


hapo kwenye red hivi hawa madaktari wa kigeni wanajua kiswahili? achilia mbali lugha zetu zingine? Yangu macho
 
kuna kitu kinakosekana kwa nini madakitari wasifanye press release waseme kila kitu ni ini wanataka na sisis wananch tuelewe kwa sababu hapa kuna ishu moya madakitari wanamgogoro na serikari alafu tunasikiliza upande mmja tu mi ningeona busara madakitari wajibu hutuba ya raisi kwa jinsi wanavyo dai then waombe matangazo kwenye media ili wananchi waelewe vizuri kuhusu madai yao .

Pili kuna kitu ambacho wananchi wanatakiwa wajue kuwa wao wanahitaji matibatu na mtu wa kuprovide hizo serivice ni serikali kupitia hospitali zake kwa hiyo wananchi tunatakiwa tudai haki yetu ya kutibiwa kutosa serikalini au viongozi tuliowachagua
 
Wakurugenzi wa hospitali binafsi wamegoma kubeba mzigo wa serikali wa kuchukua wagonjwa kutoka hospitali za Public zilizoathiriwa na mgomo.

Serikali yapata jibu la kejeli... "Kama mnaweza kuwalipia wagonjwa private kwanini fedha hizo msitumie kuwalipa madaktari?"

Hapo kwenye Red ni pa kubold chungu lakini dawa!Shabash!
 
Si kweli kwamba serikali haina uwezo wa kuboresha mazingira ya utoaji huduma za afya. Shida ni kasumba ya kufanya siasa za kibabe, siasa za ki-mungu mtu. Wangejishusha na kuwa kama binadamu wa kawaida (no one is perfect) na kusiliza kwa dhati maoni ya walio chini yao tungeepuka hii kadhia.

Nakubaliana nawe 100%
 
mimi nawaambiaje damu ya dr Ulimboka itawatesa sana dhaifu na liwalo na liwe, hawatakuwa at peace. Dhaifu kama mtoto vile yaani hajui nini kinahitajika wakti huu wa mgomo, yeye anaendekeza ma propaganda tu. Liwalo na liwe ndo goigoi kabsaa
 
Habari za kuunda hizi, private wanataka hela tu wao, siasa wamewaachia hao wa muhimbili.

Ingekua Busara ukashirikisha ubongo wako kidogo, hivi ni hospitali gani uya private utakayoenda useme serikali imesema tuje huku kutibiwa? nnaya....fu
 
Habari za kuunda hizi, private wanataka hela tu wao, siasa wamewaachia hao wa muhimbili.

Madebelele serikali ipi yenye hela za kuwalipia wagonjwa kwenye hospitali binafsi wakati huduma zote za afya ni maamuzi tu ya kuelekeza rasilimali?
 
Inaweza kuwa ni kweli kwani Serikali inachelewa sana kuwalipa hususan wale wa Bima ya afya (NHIF) wengine hawajalipwa bill ya mwezi wa tatu hadi sasa kwa hivyo wataendeshaje shughuli zao bila ya kulipwa
 
Back
Top Bottom