Serikali yakwaa kisiki Hospitali binafsi!

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
Wakurugenzi wa hospitali binafsi wamegoma kubeba mzigo wa serikali wa kuchukua wagonjwa kutoka hospitali za Public zilizoathiriwa na mgomo.

Serikali yapata jibu la kejeli... "Kama mnaweza kuwalipia wagonjwa private kwanini fedha hizo msitumie kuwalipa madaktari?"
 
I was waiting to see the miracles!! Watajinyanyua, kama vipi wazifutie vibali hospitali binafsi ili waoneshe ubabe wao vizuri.
 
Si kweli kwamba serikali haina uwezo wa kuboresha mazingira ya utoaji huduma za afya. Shida ni kasumba ya kufanya siasa za kibabe, siasa za ki-mungu mtu. Wangejishusha na kuwa kama binadamu wa kawaida (no one is perfect) na kusiliza kwa dhati maoni ya walio chini yao tungeepuka hii kadhia.
 
Mkuu kama taarifa hii ni kweli basi safi sana,lakini swali moja ni nini source ya taarifa hii.
 
Mkuu kama taarifa hii ni kweli basi safi sana,lakini swali moja ni nini source ya taarifa hii.

usiulize source wewe meza.unajuaje huyo aliyeleta hii taarifa ni mmojawapo ya wakurugenzi wa private hospitals?
 
Habari za kuunda hizi, private wanataka hela tu wao, siasa wamewaachia hao wa muhimbili.
 
Sasa hivi ndio peak ya uongozi wa awamu ya nne...presha zinapanda na kushuka...magroup ndani ya chama yanahujumiana...siri zinawekwa wazi wazi na hadharani....yaani serikali sasa hivi inatumia nguvu zake zote iweze kuvuka salama 2015 maana mambo siyo mambo. Imechokwa
 
Hiyo habari ya kweli mkuu? Yaani private hospitals zikatae kufanya biashara?????. Labda hizo hospitali hazipo TZ ninayoifahamu!!.
 
hakuna cha klujifunza hapo kwa serikali kama vp iwapoze kimtindo izo nyongeza ila kwa kweli nchi yetu kulipa mishahara mikubwa hiyo wanayoitaka ni kama kumpigia mbuzi gitaa haiwezekani
 
Wakurugenzi wa hospitali binafsi wamegoma kubeba mzigo wa serikali wa kuchukua wagonjwa kutoka hospitali za Public zilizoathiriwa na mgomo.

Serikali yapata jibu la kejeli... "Kama mnaweza kuwalipia wagonjwa private kwanini fedha hizo msitumie kuwalipa madaktari?"

Exactly.
 
Sasa hivi ndio peak ya uongozi wa awamu ya nne...presha zinapanda na kushuka...magroup ndani ya chama yanahujumiana...siri zinawekwa wazi wazi na hadharani....yaani serikali sasa hivi inatumia nguvu zake zote iweze kuvuka salama 2015 maana mambo siyo mambo. Imechokwa
Sema wewe ndio una omba iwe hivyo. Chadema utawajua tu.
 
Ilikuwa ni propaganda tu. Watanzania wengi wanaishi vijijini. Hospitali za binafsi na za jeshi nyingi zipo mjini. Serikali inawaangalia walioko mijini tu na walioko vijijini wangepata wapi huduma? Mtu mzima anapoongopa mbele ya umma ni jambo la aibu. Angetoa hotuba ile mbele ya waandishi wa habari na aruhusu wamuulize maswali aone.
 
It is a good move. Kama wanafahamu kwamba mwisho wa siku wataambiwa asantani kwa huduma nzuri ila serikali haina pesa. Kitakachofuata kama huna mtaji mkubwa unaweza kufunga hospitali
 
Si kweli kwamba serikali haina uwezo wa kuboresha mazingira ya utoaji huduma za afya. Shida ni kasumba ya kufanya siasa za kibabe, siasa za ki-mungu mtu. Wangejishusha na kuwa kama binadamu wa kawaida (no one is perfect) na kusiliza kwa dhati maoni ya walio chini yao tungeepuka hii kadhia.

ubabe sio utatuzi.kama alipotoshwa atajiju!!
 
Wakurugenzi wa hospital hizo binafsi wakikubali tu wameingia mtego, serikali yenyewe pesa itatoa wapi za kuwalipia wagonjwa wote nchi nzima ukizingatia gharama za hospital hizo ziko juu? watakopwa mwisho wa siku kulipana itakuwa kimbembe. Hata hao madaktari wa kigeni wanadhani watakubali kulipwa madafu wakati wao ni experts(TX)..

Hebu oneni jinsi mwisho wakufikiri wa magamba ulipofikia mwisho, yaani raisi alikaa na baraza la mawaziri suluhisho wakaona ni kuagiza madaktari kutoka nje na kupeleka wagonjwa hospitali za binafsi? Jambo ambalo hata mtendaji wa kijiji ukimuuliza anaona mgomo unaweza kumalizwa vipi atakupa majibu swafi..Ama kweli sasa hivi nchi hii inahitaji AKILI YA JUU ZAIDI AMBAYO HAIPATIKANI MAGAMBA kuweza kutatua matatizo yake.
 
Back
Top Bottom