benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Serikali imeingia makubaliano na wawekezaji wa kiwanda cha Mbeya Cement ya kuboresha na kuongeza ufanisi wa uzalishaji wa kiwanda hicho ikiwa ni Pamoja na kufutwa kwa Deni la Shilingi Billion 170 ili kukiwezesha kiwanda hicho kutengeneza Faida.
Serikali inamiliki asilimia 35 ya hisa katika kiwanda hicho huku asilimia 65 ikimilikiwa na wawekezaji wengine wawili, Lafarge na Pan African Cement kutoka nchini Mauritius.
Kiwanda hicho cha Mbeya Cement kilikua hakizalisha faida kwa ipindi kirefu kutokana na kuelemewa na madeni ambapo akizungumzia makubaliano hayo msajili wa Hazina, Neemia Mchechu amesema hatua zilizochukuliwa ni kufanya Mabadiliko ya Muundo wa Uongozi Pamoja na kufuta Deni hilo la Billion 170 lililokua likidaiwa na mmoja wa wanahisa.
Pia Neemia amesema hatua iliyofanyika kufufua kiwanda hicho itafanyika pia kwa kampuni zingine ambazo serikali ina hisa chache ili kuziwezesha kufanya vizuri na kutoa gawio kwa Serikali.
Kiwanda hicho kilikua kikihudumia Mikoa 7 jirani ambapo Meneja wa kanda ya Afrika KMashariki na Kusini wa HOLCIM Group Rajesh Surana amesema kuwa makubaliano hayo yatawezesha kampuni kusonga mbele na kuwanufaisha wateja na wana hisa.