Serikali yafunga kesi ya Mramba na Yona

Mkuu punguza jazba, kufunga kesi na kuachiwa huru ni vitu viwili tofauti, kufunga kesi maana yake ni kuwa upande wa mashtaka umekamilisha ushaidi wake sasa kinachosubiliwa ni mahakama kuja na kauli kama watuhumiwa wana kesi ya kujibu au hawana kesi ya kujibu. huyo michuzi uliyemkoti kichwani bure kabisa inaonekana hata yeye hiyo habari kaipata kwa text msg. kama yeye ni mwandishi makini angalau angeandika kesi ya Mramba ushaidi wakamilika, hao ndio waandishi wetu hata akiwa chooni anataka yeye ndio aonekane ndio mtoa habari wa kwanza. pumba.

hata mie nilitaka kuuliza manake sikuelewa vizuri. ni kuwa wamefutiwa mashitaka, au kesi (ushahidi) i(u)mefungwa?
 
Nilivyosoma kwenye michuzi pia ilinishangaza na kunikasirisha sana. Lakini baadaye nikaelewa kwamba kesi haijafutwa ila kwa upande wa serikali ushahidi umekwisha sasa tunasubili amri ya mahakama kuamua kama watuhumiwa wana hatia ama la? huo ndo uelewa wangu jaman.
 
Kuna mzee mmoja alishawahi kuniambia kuwa hizi kesi za kina Yona na Mramba zimapelekwa ili kuwahadaa watanzania lakini si chochote si lolote wanasubiri uchaguzi ukishapita hizo kesi zitafungwa na kweli hatujamaliza hata January ishafungwa :frusty: tusibiri na wao wadai mabilion ya fidia...
inauma kichizi yani why!?????
 
Habari hii haijafanyiwa Utafiti kwa vile kesi badi inaendelea na imepangwa kuendele mwezi february, tusome ndani ya Mistari(read btwn lines and btwn words)
 
Mkuu punguza jazba, kufunga kesi na kuachiwa huru ni vitu viwili tofauti, kufunga kesi maana yake ni kuwa upande wa mashtaka umekamilisha ushaidi wake sasa kinachosubiliwa ni mahakama kuja na kauli kama watuhumiwa wana kesi ya kujibu au hawana kesi ya kujibu. huyo michuzi uliyemkoti kichwani bure kabisa inaonekana hata yeye hiyo habari kaipata kwa text msg. kama yeye ni mwandishi makini angalau angeandika kesi ya Mramba ushaidi wakamilika, hao ndio waandishi wetu hata akiwa chooni anataka yeye ndio aonekane ndio mtoa habari wa kwanza. pumba.

Ndo ntolee hii kaka dont expect something different ni ishu ilosukwa na mkulu yupo pembeni yao wanafanya hivi ili kupunguza kelele za watz ambazo hazijawahi kusikilizwa hata zikiwa na sauti ya juu.... usitegemee ki2 kingine tofauti na kuimaliza kesi kiaina huku wakiachiwa huru na kutudai fidia ya mabilion Just stay tuned..
 
Kama ni kweli basi nampongeza sana huyo aliyetoa maamuzi na pia nawapongeza akina Yona.... Kwani sasa wamezidi kuichimbia kaburi serikali ya chama "chetu".... Watawala wakumbuke kwamba kwa hali ya sasa, watanzania walihitaji mbuzi wa kafara kutoka tabaka tawala kwani tumechoka kuliwa sisi huku hao wenye nchi wakineemeka kupita kiasi

Gap ya walio nacho na wasio nacho inatisha, chuki baina ya watanzania wenyewe imefikia pabaya, hali ya maisha ni ngumu sana...

Wanasema vigezo vyote vya kaburi sa CCM viko wazi kwa sasa, sijui ni kipi walichobaki nacho kinawa-impress raia wa kawaida? kuwafunga vibaka wa kuku?
kuwachoma moto wanaoiba nokia ya tochi?
kuwapakata akina vithlani?
kuwakashifu wasema ukweli?
kuiba vocha za mbolea?
kubeza wenye uchungu na nchi?

LA HASHA, POER YA MEDIA NA HASA ELECTRONIC NI KUBWA BEYOND ANYONES RECOGNITIONS, IT HAS BUILT CHARACTER AND ASSASSINATE OTHERS

BYEBYE TANZANIA YENYE INTEGRITY
 
kwani nani amabye hakujua hii ni danganya toto? tangu lini vigogo wa tz wakafungwa?
au mmesahau hata Kikwete mwenyewe aliwahi kusema kuwa hawa matajiri wananguvu na wanaweza kuiyumbisha nchi? je alikuwa anamaanisha nini? ninyi acheni tu hii nchi sio yenu, bali ni ya kwao
 
Upande wa Serikali leo umefunga kesi inayomkabili Waziri wa zamani wa Wizara ya Fedha, Basil Mramba, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona na Katibu Mkuu wa zamani wa Fedha, Gray Mgonja.
Maelezo hayo ya kufunga kesi hiyo yametolewa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, na mwendesha mashtaka Wakili Mkuu wa Serikali Boniface Stanslaus alipotakiwa na kiongozi wa jopo la majaji watatu wanaosikiliza shauri hilo, Jaji John Utamwa kumleta kizimbani Shahidi wa 14 aendelee kutoa ushahidi wake.
Jaji Utamwa aliwataka mawakili wa pande zote mbili kuongea lolote kama wana hoja yoyote ya msingi kabla jopo halijatoa uamuzi wake.
Wakili wa Mgonja, Profesa Leonard Shahidi alidai kwa niaba ya mawakili wenzake upande wa utetezi hauna pingamizi juu ya hilo lakini aliiomba Mahakama kuwapatia nakala ya mwenendo wa kesi ili waweze kuongea kupitia majumuisho hayo.
Jaji Utamwa alikubali maombi hayo ambapo alisema shauri hilo litatajwa Februari 18, mwaka huu na kwamba kama uchapwaji wa nakala hizo utakuwa umekamilika itapangwa tarehe ya kusikiliza shauri hilo.
Hata hivyo, Prof. Shahidi aliutaka upande wa utetezi kuwapatia majumuisho ya ya hoja za mashahidi kwa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, ambapo alidai atawasilisha hoja kuitaka Mahakama iwaone wateja wao hawana kesi ya kujibu.
Kesi hiyo Namba 1200 ya mwaka 2008, ilianza kusikilizwa Novemba 2009, imefungwa baada ya kupitiwa kwa vielelezo 26 na mashahidi 14 kukamilisha ushahidi wao mahakamani hapo.
Katika kesi hiyo, mawaziri hao wa zamani kwa pamoja wanatuhumiwa kuingia mkataba na kuisamehe kodi kinyume cha sheria kampuni ya Alex Stewart jambo linalodaiwa kuisababisha Serikali hasara ya Sh bilioni 11.
 
I retire my case, there is little we can do. I never thought i'm a quiter, but for this case goodluck my friends, i bow out.

The problem are so complex in Tanzania, there is no doubt everything is hot to touch. Udini is strengthening in our community, corruptions is skyrocket, the gap between rich and power is getting wider and wider every morning.

Jakaya is acting like a teenager who got her first orgasim. Everyone in CCM is dice and slice Tanzanian about Dowans, ufisadi and everything. God bless the land of my mother and God bless Tanzanian. I rest my case to Allah, hope He will take a wheel because we can't drive anymore.
 
Back
Top Bottom